Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 11,557
- 33,535
Elon Musk ameanza kutekeleza mpango wa kuliua Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID). Amesema anaamini USAID ni "shirika la kihalifu" ambalo linapaswa "kufa."
Kupitia mtandao wa X Musk alisema “USAID ni shirika la uhalifu. Ni wakati wa kufa”
Hii ni baada ya taarifa iliyosema kuwa maafisa wakuu wa USAID walijaribu kuwazuia watu kutoka bodi mpya ya ushauri iliyo chini ya Elon Musk iitwayo "Idara ya Ufanisi wa Serikali," (DOGE) kupata taarifa zilizomo ndani ya mifumo ya taasisi hiyo.
NBC News iliripoti kuwa utawala wa Trump umelenga kufanya mabadiliko makubwa yatakayoiathiri USAID.
Shirika hilo hutoa misaada kwa nchi nyingi zilizoathiriwa na migogoro na kusaidia nchi zinazoendelea kwa njia mbalimbali.
Shirika hilo lina bajeti ya zaidi ya dola bilioni 50 na liliundwa mnamo 1961.
Muda mfupi baada ya kuchukua madaraka, Trump alitia saini amri ya kiutendaji ambayo ilisimamisha kwa muda ufadhili kwa USAID.
Kwa sasa tovuti za shirika hilo zimefutwa na hazipatikani mtandaoni.
Hivyo zile nchi zinazotegemea misaada zijiandae na mabadiliko haya ya kudumu.