Kwa nchi zinazotegemea misaada hali inazidi kuwa ngumu, Elon Musk aanzisha mpango wa kuiua USAID

Kwa nchi zinazotegemea misaada hali inazidi kuwa ngumu, Elon Musk aanzisha mpango wa kuiua USAID

Kwa wasiojua, siku mbili kabla ya Trump kuingia madarakani ilikuwa itangaze kufikisika au kuongeza ukomo wa ukopaji ifikie dollar trillion 37. Ikabidi wasitishe malipo yote mpaka Trump aingie madarakani afanye uamuzi.

Baada ya Trump kuingia amelazimika kupunguza matumizi ya serikali badala ya kukopa. Na Kila mwaka wanapaswa kupunguza kati ya dollar trillion 1 -2. Ndio wataweza kukaa vizuri.

Sasa njia pekee na haraka funga misaada (USAID) bakisha Ile TU yenye tija na badili mfumo na muundo wa shirika.

Funga program zisizo na maana kama DEI na zinginezo. Jitoe WHO, jitoe program ya mazingira(Paris accord) etc

Kwa Sasa wabasave dollar billion mbili Kila siku.

Hali ni mbaya zaidi Kwa umoja ulaya kwanza wanapaswa kuisadia Ukraine kifedha na kijeshi wakati uchumi wao unapumilia mashine ni Spain peke yake uchumi wake unakuwa Kwa zaidi ya 2%. Wengine wote 0.2% -1.6%.

Trump kawaambia waongeze budget ya ulinzi mpaka 5% ya GDP zao vinginevyo anajitoa.

Ia anaondoa wanajeshi wake 20,000 ulaya(NATO) ulaya ijilinde yenye isitegemee sana US.

Mbaya zaidi Trump anataka kuwekea umoja ulaya vikwazo(25% tariif) Kwa bifhaa zote zinazoingia marekani. Canada na Mexico tayari wamesha tangaziwa kama Chao.

Kwa mazingira haya yote Kwa Sasa ni ngumu kutabiri hali ya Uchumi wa US na hata ulaya.

Manufacturing hub ya Dunia Kwa Sasa ni China, India nae ananyemelea na hao wawili TU wanapopulation ya 40% plus ya watu wote duniani.

Hivyo USA inahitaji kujiunda upya kushindana na maifa hayo na ualaya Kwa ujumla.

Kwetu Africa ni muda Sasa kuunda viwanda vyetu wenyewe Sasa pharmaceuticals, communication gadgets na viwanda vya mahitaji kama nguo, n.k Kwa wakati huu ni muhimu sana. Nje ya hapo tutalipa na kusagia meno.
 
Mi ninachoona hapa US imeamua kuonyesha kwa wazi yeye ni nani, nchi za Africa tumekuwa na ukaribu mkubwa na China katika ushirikiano wa kiuchumi n.k barani Africa, China sasa ni partner mkubwa kibiashara na Africa, Ramaphosa mwenyewe alishasikika akisema 'Africa should not suffer because of America’s “jealousy” of what China can offer the continent..

US na China ni kama mabwana wanaogombea mwanamke.

US nadhani imeona licha ya misaada na pesa wanazozitoa Africa lakini bado hawathaminiki na China bado inakuwa na ushawishi Africa.

Kuna kipindi US walikiri kwamba China inazidi kuwapita kiushawishi barani Africa, lengo likiwa nchi za Africa kuisusia China. Hadi leo nchi za Africa tunatumia bidhaa za huawei, kuanzia transmitters n.k...

Kenyatta mwenyewe alishazungumza, Africa si bara la kupiganiwa kama tuzo, hivyo waiache Afria yenyewe ichague..

KInachofanyika ni kama kuishinikiza Africa ichague upande, ni kama vikwazo tunawekewa sasa..

Mkuu, mbona umefocus Africa tu! Unajua misaada ya USAID ilivyozagaa Ulimwenguni? Target sio Africa .......Sipendi kukupoteza muda wako, tafuta list ya nchi zinapokea pesa za USAID...angalia Asia, Latin America utachoka!
 
View attachment 3223211

Elon Musk ameanza kutekeleza mpango wa kuliua Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID). Amesema anaamini USAID ni "shirika la kihalifu" ambalo linapaswa "kufa."

Kupitia mtandao wa X Musk alisema “USAID ni shirika la uhalifu. Ni wakati wa kufa”

Hii ni baada ya taarifa iliyosema kuwa maafisa wakuu wa USAID walijaribu kuwazuia watu kutoka bodi mpya ya ushauri iliyo chini ya Elon Musk iitwayo "Idara ya Ufanisi wa Serikali," (DOGE) kupata taarifa zilizomo ndani ya mifumo ya taasisi hiyo.

NBC News iliripoti kuwa utawala wa Trump umelenga kufanya mabadiliko makubwa yatakayoiathiri USAID.

Shirika hilo hutoa misaada kwa nchi nyingi zilizoathiriwa na migogoro na kusaidia nchi zinazoendelea kwa njia mbalimbali.

Shirika hilo lina bajeti ya zaidi ya dola bilioni 50 na liliundwa mnamo 1961.

Muda mfupi baada ya kuchukua madaraka, Trump alitia saini amri ya kiutendaji ambayo ilisimamisha kwa muda ufadhili kwa USAID.

Kwa sasa tovuti za shirika hilo zimefutwa na hazipatikani mtandaoni.

Hivyo zile nchi zinazotegemea misaada zijiandae na mabadiliko haya ya kudumu.

View attachment 3223309
kazi ipo
 
Let's wait for the 90 days transition period !! Perhaps it's being restructured. Nevertheless we expect for a massive reduction in aids if at all activities are going to be resumed. All in all, it isa wake up call for countries that were depending on USAID.
 
maafisa wakuu wa USAID walijaribu kuwazuia watu kutoka bodi mpya ya ushauri iliyo chini ya Elon Musk iitwayo "Idara ya Ufanisi wa Serikali," (DOGE) kupata taarifa zilizomo ndani ya mifumo ya taasisi hiyo.
Duh,
Hao maafisa walishindwa kusoma alama za nyakati. Hawakujua kuwa Elon Musk ni mshauri wa rais kwa sasa, na kwa utajiri alionao, ana sauti
 
Kumbe Rais ana nguvu sana hata nchi zilizoendelea sio Tz tu. Imagine Trump kaingia anabadili vitu upside down.

Mkuu, nadhani USAID iko chini ya Executive branch (Chini ya Raisi) ingawa ilikuwa ikijitegemea! Hata Mkuu wake anachgauliwa na Rais, tutaona waliokwenda Mahakamani kupinga matokeo yatakuwa ni nini.
 
Sawa tu.

Hio misaada ya USAID yenyew haiwafikii wahusika, hela zinaishia kwa wachache waliopo madarakani.

Hadi msaada umfikie mwananchi wa kawaida utafika imenjinjwa sana.

Mi naona sawa tu.
 
View attachment 3223211

Elon Musk ameanza kutekeleza mpango wa kuliua Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID). Amesema anaamini USAID ni "shirika la kihalifu" ambalo linapaswa "kufa."

Kupitia mtandao wa X Musk alisema “USAID ni shirika la uhalifu. Ni wakati wa kufa”

Hii ni baada ya taarifa iliyosema kuwa maafisa wakuu wa USAID walijaribu kuwazuia watu kutoka bodi mpya ya ushauri iliyo chini ya Elon Musk iitwayo "Idara ya Ufanisi wa Serikali," (DOGE) kupata taarifa zilizomo ndani ya mifumo ya taasisi hiyo.

NBC News iliripoti kuwa utawala wa Trump umelenga kufanya mabadiliko makubwa yatakayoiathiri USAID.

Shirika hilo hutoa misaada kwa nchi nyingi zilizoathiriwa na migogoro na kusaidia nchi zinazoendelea kwa njia mbalimbali.

Shirika hilo lina bajeti ya zaidi ya dola bilioni 50 na liliundwa mnamo 1961.

Muda mfupi baada ya kuchukua madaraka, Trump alitia saini amri ya kiutendaji ambayo ilisimamisha kwa muda ufadhili kwa USAID.

Kwa sasa tovuti za shirika hilo zimefutwa na hazipatikani mtandaoni.

Hivyo zile nchi zinazotegemea misaada zijiandae na mabadiliko haya ya kudumu.

View attachment 3223309
Ni muda wa hizo nchi kuamka na kujitegemea
 
Sawa tu.

Hio misaada ya USAID yenyew haiwafikii wahusika, hela zinaishia kwa wachache waliopo madarakani.

Hadi msaada umfikie mwananchi wa kawaida utafika imenjinjwa sana.

Mi naona sawa tu.
Mkuu, pesa inaanzwa kuchinjwa toka US kwenyewe! Mpaka ikifika bongo ndio usiseme!
 
Ni muda wa hizo nchi kuamka na kujitegemea

Ni vigumu mno, tuliofanya Mashirika hayo tunajua flow of money toka kwa donors mpaka ifike kwa walengwa! Naona moderater ameondoa baadhi ya posts zangu! Miradi mingi mno inasaidia wafanyakazi katika miradi hiyo indirectly kwa njia ya mishahara na marupurupu tu, lakini hizo semina nk. kwatika miradi mingi hazibadili maisha yao!
 
Kitakachofuata watafunga hadi barozi kwa nchi ambazo wanaona hazi faida kwao.
Wanaenda kupoteza influency

Influence kwa nani Mkuu? Unaweza kupoteza influence kwa Somalia, Comoro,Burundi, Malawi, Burkina Faso....The list is endless na unaweza ukajazia na wewe.Toka anagombea Urais, aganda kubwa American first...! Jamaa anatishia kujitoa NATO, kajitoa Paris Accord, kajitoa USAID.....Ni ni influence ipi unasema mkuu?
 
Back
Top Bottom