Kwa nchi zinazotegemea misaada hali inazidi kuwa ngumu, Elon Musk aanzisha mpango wa kuiua USAID

View attachment 3223211

Elon Musk ameanza kutekeleza mpango wa kuliua Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID). Amesema anaamini USAID ni "shirika la kihalifu" ambalo linapaswa "kufa."

Kupitia mtandao wa X Musk alisema “USAID ni shirika la uhalifu. Ni wakati wa kufa”

Hii ni baada ya taarifa iliyosema kuwa maafisa wakuu wa USAID walijaribu kuwazuia watu kutoka bodi mpya ya ushauri iliyo chini ya Elon Musk iitwayo "Idara ya Ufanisi wa Serikali," (DOGE) kupata taarifa zilizomo ndani ya mifumo ya taasisi hiyo.

NBC News iliripoti kuwa utawala wa Trump umelenga kufanya mabadiliko makubwa yatakayoiathiri USAID.

Shirika hilo hutoa misaada kwa nchi nyingi zilizoathiriwa na migogoro na kusaidia nchi zinazoendelea kwa njia mbalimbali.

Shirika hilo lina bajeti ya zaidi ya dola bilioni 50 na liliundwa mnamo 1961.

Muda mfupi baada ya kuchukua madaraka, Trump alitia saini amri ya kiutendaji ambayo ilisimamisha kwa muda ufadhili kwa USAID.

Kwa sasa tovuti za shirika hilo zimefutwa na hazipatikani mtandaoni.

Hivyo zile nchi zinazotegemea misaada zijiandae na mabadiliko haya ya kudumu.
NITA FURAHI SANA DAWA ZA UKIMWI ZIKIANZA KUUZWA DUNIANI KWA SABABU TUSIO NA UKIMWI TUNANYANYASIKA SANA KWA KUAMBIWA ETI TUNAOGOPA UKIMWI.....wanasema hivyo kwa sababu dawa ni bure ila zikianza kuuzwa dozi ya mwezi sh 30000 hiyo kauli itakufa
 
Uwezo hatuna ila sasa kwa sababu hawajali tena kuhusu US na yeye bila shaka hajali kuhusu Afrika tutashuhudia akina Museveni wengi maana sasa wanamwoga nani.
Mi ninachoona hapa US imeamua kuonyesha kwa wazi yeye ni nani, nchi za Africa tumekuwa na ukaribu mkubwa na China katika ushirikiano wa kiuchumi n.k barani Africa, China sasa ni partner mkubwa kibiashara na Africa, Ramaphosa mwenyewe alishasikika akisema 'Africa should not suffer because of America’s “jealousy” of what China can offer the continent..

US na China ni kama mabwana wanaogombea mwanamke.

US nadhani imeona licha ya misaada na pesa wanazozitoa Africa lakini bado hawathaminiki na China bado inakuwa na ushawishi Africa.

Kuna kipindi US walikiri kwamba China inazidi kuwapita kiushawishi barani Africa, lengo likiwa nchi za Africa kuisusia China. Hadi leo nchi za Africa tunatumia bidhaa za huawei, kuanzia transmitters n.k...

Kenyatta mwenyewe alishazungumza, Africa si bara la kupiganiwa kama tuzo, hivyo waiache Afria yenyewe ichague..

KInachofanyika ni kama kuishinikiza Africa ichague upande, ni kama vikwazo tunawekewa sasa..
 
Hii inaenda kuifanya Afrika ijitenge zaidi na US. Unadhani viongozi wa AFrika wanaadhriika wao kwa hili? Unadhani ukosefu wa dawa na upotevu wa kazi wao wanajali sana? WAngekuwa wanajali ungeshasikia mipango ya kukabiliana na hili na kupunguza matumizi.
WAkati US wakijaribu kupunguza amtumizi, viongozi wa Afrika wanaongeza matumizi.
So, sidhani kama hii mbinu itamsaidia sana isipokuwa nchi za AFrika zinajiweka zaidi na china na nchi za kiarabu maana hao hata huwa hawa question uongozi wao pia.
 
Miafrika tunatia aibu, miaka 60 ya uhuru bado tunatembeza mabakuli huku makusanyo tukitumia kwa mambo mengi ya ajabu ajabu na ufisadi.

Pesa tunayonunulua magoli, hongo za pikipiki ili tushinde uchaguzi, tunazoigawia CCM, za kuzurura na wasanii, na zinazoishia kwenye ufisadi na anasa mbalimbali kama magari ya kifahari ziende zikagharimie afya. Maana pesa hizo ni zaidi ya trilioni 3.

Tukiweza kuiondoa CCM, fedha yetu we yewe inatosha kugharamia afya na huduma nyingine. Lakini CCM ikiendelea ni mateso matupu maana wao ni aheri watu wafe kuliko kukosa hela ya kuzurura na wasanii au CCM ikose mgao.
 
View attachment 3223211

Elon Musk ameanza kutekeleza mpango wa kuliua Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID). Amesema anaamini USAID ni "shirika la kihalifu" ambalo linapaswa "kufa."

Kupitia mtandao wa X Musk alisema “USAID ni shirika la uhalifu. Ni wakati wa kufa”

Hii ni baada ya taarifa iliyosema kuwa maafisa wakuu wa USAID walijaribu kuwazuia watu kutoka bodi mpya ya ushauri iliyo chini ya Elon Musk iitwayo "Idara ya Ufanisi wa Serikali," (DOGE) kupata taarifa zilizomo ndani ya mifumo ya taasisi hiyo.

NBC News iliripoti kuwa utawala wa Trump umelenga kufanya mabadiliko makubwa yatakayoiathiri USAID.

Shirika hilo hutoa misaada kwa nchi nyingi zilizoathiriwa na migogoro na kusaidia nchi zinazoendelea kwa njia mbalimbali.

Shirika hilo lina bajeti ya zaidi ya dola bilioni 50 na liliundwa mnamo 1961.

Muda mfupi baada ya kuchukua madaraka, Trump alitia saini amri ya kiutendaji ambayo ilisimamisha kwa muda ufadhili kwa USAID.

Kwa sasa tovuti za shirika hilo zimefutwa na hazipatikani mtandaoni.

Hivyo zile nchi zinazotegemea misaada zijiandae na mabadiliko haya ya kudumu.

View attachment 3223309

Yupo live now. Msikilieni
 
Huyu msouth Africa hajui anachezea bomu litamlipukia muda si mrefu!
Vyombo vya usalama vinamlia timing hataamini.
 
USAID kweli wahuni. Hela nyingi hurudi Marekani kihuni. Wana kampuni zao ambazo hupewa tenda kilazima. Kwa mfano ukipewa tenda na USAID ya ku-supply vifaa tiba itakulazimu hivyo vifaa ununulie Marekani kwenye makampuni waliyopendekeza. Hata tafiti zinazofadhiliwa na USAID zinakuwa na ukakasi sana. Pamoja na yote bado tunawahitaji.
Hata kama ningekua ni mm nisingekuruhusu....Yaani nikupe tenda afu utoke kwetu uende sijui china kununua midosho wakati kwetu kuna kila kitu tena quality kabisa.
 
Kuna mpumbavu mmoja aliwahi sema nchi yetu ni huru na ina haki ya kujiamulia mambo yake yenyewe.
Bila kuingiliwa na nchi nyingine.

Mzungu sio mswahili!
Hataki uchawa
Hataki mapambio ya kusifiwa na kutukuzwa.
 
Hata kama ningekua ni mm nisingekuruhusu....Yaani nikupe tenda afu utoke kwetu uende sijui china kununua midosho wakati kwetu kuna kila kitu tena quality kabisa.
Viwanda vyote viko China. Halafu kama ni msaada kwanini kuwe na masharti ya kipuuzi? Nina uhakika hela za USAID ni kama 10% tu huzunguka hapa nchini. Wakitoa tenda ya 100m lazima kama 70m irudi USA
 
Watajijua ambao wanaogopa kufa

Wengine tupo tayar,waktaka hata dawa za malaria wasilete
 
Viwanda vyote viko China. Halafu kama ni msaada kwanini kuwe na masharti ya kipuuzi? Nina uhakika hela za USAID ni kama 10% tu huzunguka hapa nchini. Wakitoa tenda ya 100m lazima kama 70m irudi USA
Sasa unataka zirudi wapi
 
Back
Top Bottom