Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Tulisikia taarifa ya Kamati ya Maadili ya Tume ya Taifa ya uchaguzi, katika kikao chake ilichoketi Jana, ikitoka na uamuzi wa kumfungia Tundu Lissu, kutofanya mikutano ya kampeni kwa wiki moja, kuanzia tarehe 3 hadi tarehe 9 ya mwezi huu wa 10
Wasidhani hiyo Kamati ya Maadili ya Tume ya uchaguzi itakuwa "imemkomoa" Tundu Lissu, badala yake ndiyo imezidi kumpa umaarufu mkubwa, ambao haumithiliki, katika uchaguzi mkuu unaotegemewa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Ni dhahiri sasa wananchi tutakuwa tumedhithibitisha pasipo shaka yoyote kuwa hii Tume ya uchaguzi iko "biased" na inafanya kazi kwa maagizo toka juu na inafanya upendeleo wa dhahiri kwa CCM!
Kwa kuwa kama alivyoeleza Tundu Lissu katika kikao chake na waandishi wa habari hapo jana kuwa yeye kama mgombea Urais kwa kupitia chama chake cha CHADEMA, wameshawaandikia barua 3 za malalamiko, kupeleka kwa Tume hiyo ya uchaguzi, dhidi ya vitendo vinavyokiuka Maadili ya uchaguzi, vikiwemo vitendo vya utoaji rushwa vya waziwazi katika kampeni za huyo mgombea wa CCM, John Magufuli, hata hivyo Tume hiyo, imepata "kigugumizi" na kutotaka kabisa angalau kueleza kuwa wamezipokea, barua hizo za malalamiko!
Ukiangalia historia ya mgombea huyu wa CHADEMA, amekuwa akionewa mno na vyombo vya dola vya hapa nchini.
Jaribu ku-imagine ni Tundu Lissu huyo huyo, ambaye zaidi ya miaka 3 hivi sasa, alishambuliwa kwa kimiminiwa risasi 16 mfululizo, katika jaribio la kutaka kumuua, ambapo lilimlazimu akimbizwe nje ya nchi, ambako amekuwa akipata matibabu kwa kipindi chote hiki.
Katika kipindi chote hicho cha miaka zaidi ya 3 Jeshi letu la Polisi, halijamkamata hata mtuhumiwa mmoja ili kumhoji kwa tukio hilo la kinyama kabisa!
Cha ajabu zaidi ni kitendo kilichofanywa na Spika wa Bunge, Job Ndugai cha kutompa stahiki zake za matibabu, ambapo ni kwa mujibu wa sheria, lakini kilichowasononesha zaidi watanzania, ni cha kumvua ubunge wake, kwa madai ya kuwa yeye Spika Ndugai, kwa madai yake kuwa Tundu Lissu ni mtoro na hajui alipo!
Kuna kawaida ya ubinadamu, ku-sympathize na binadamu mwenzako ambaye unaamini kabisa kuwa kuna mlolongo wa kumwonea kupita kiasi, ndiyo maana naona kwa vitendo anavyoendelea kufanyiwa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu, vinaendelea kumpa nguvu na kuungwa mkono na Umma wa watanzania na naviona vitendo hivyo sawasawa na kumpiga chura mateke, kwani ndiyo umavyozidi kumuongezea mwendo!