Uchaguzi 2020 Kwa nilichokiona Mbeya Town, Sugu nakuomba urudi kwenye muziki wa kufoka foka, Dr. Tulia atakulaza asubuhi sana

Uchaguzi 2020 Kwa nilichokiona Mbeya Town, Sugu nakuomba urudi kwenye muziki wa kufoka foka, Dr. Tulia atakulaza asubuhi sana

Yeye hafanyi kampeni Wananchi wanamwomba agombee na pia Wananchi walimuomba asaidie yeye hakujipeleka

Sent using Jamii Forums mobile app

Muhimu mshagara wake haulinfani na tunayoyaona. Tulitarajia mtumishi wa serikali alete mawazo mbadala na sio pesa.

Waitara generous mwengine wa ccm alijatibu hicho anachokifanya huyo msichana na kaonywa. Sasa huyo msichana yuko juu ya sheria?!?!?!

Wanambeya wanaotaka sabuni, khanga karne hii inabidi tujiulize Mara mbili, mbili
 
Ndiyo maana ya uchaguzi Kuna kushinda na kushindwa.So haina haja ya kujitoa.Waache waingie ulingoni

Kila kona ya jiji wanaimba jina la Dr Tulia Ackson, wanasema huyu mama amejitolea kuwahudumia wana Mbeya

Amewezesha sacsos nyingi sana karibu kila kata ya Mbeya, hizo saccos kwa kiasi kikubwa zimewezesha wananchi kujikimu na mahitaji ya kila siku.

Mama moja katika soko la Mwanjelwa aliyejitambulisha kama Mama Tarumbeta anasema, Huyu binti Tulia ana miaka michache tu tena aingie kwenye siasa ila amekuwa ni chachu kubwa kwa maendeleo ya wananchi wa Mbeya.

Anaendelea kusema, anasaidia sio kwamba ni tajiri ila ana moyo wa kutoa tofauti na viongozi wengine wa kisiasa waliopo Mbeya.

Vijana wengi wamehamishia matumaini kwa huyu dada ambaye toka awe Naibu Spika amefanya maajabu makubwa Tanzania.

My take: Mh Sugu ili kuepusha aibu ya mwaka tunaomba ustaafu ubunge kwa heshima, wana Mbeya wanakufanyia mazoezi ya kukuchinja kwenye boksi la kura.

Huu muda ungerudia kwenye muziki wa kufokafoka tu, huku kwenye Siasa wana Mbeya wamepata mwanamama ngangari anayeenda kuleta mapinduzi katika mkoa wa Mbeya.

Tuipende Tanzania
 
Dr Tulia hajapelekwa alifuatwa na wana mbeya kuombwa

Amesaidia wana mbeya, ila mbunge wao hataki kuwasaidia

Back
Top Bottom