Uchaguzi 2020 Kwa nilichokiona na kukisikia leo katika Misafara ya Gwajima na Mdee Kawe huenda Mshindi akatangazwa angani na Mtangazaji akatokomea Kusikojulikana

Mkuu GENTAMYCINE umetupa yale uliyoyasikia tupe na mtazamo wako ukoje?

Hivi sijui kwa nini Mch anahangaika kuwa Mbunge wakati jukumu hilo tu la uchungaji ni shughuli pevu?

Mtazamo wangu Mimi kwa huku Kawe nipo 'Neutral' kwani 'Hasira' zangu zote nimezimalizia Kigamboni kwa Mtu 'nisiyempenda' na amekosa kweli.
 
Ni aibu kuwakilishwa na mtu kilaza kama Gwajima anayetegemea story za YouTube kuendeshea maisha yake
 
Kauli muhimu niliyosikia kutoka katika Msafara wa Gwajima ni hii nainukuu hapa chini:
"Yaani CCM na Mwenyekiti wetu hawajajifunza kutoka kwa Wagombea wa huko nyuma na bado tu wameendelea na Upuuzi wao ule ule wa Kututeulia wale tusiowataka hapa Kawe. Kwakuwa tunajua huyu ana Hela na hata Mwenyekiti wake na Chama chake kitampa Pesa ila Sisi tutakachofanya tutamlia Pesa zake, tutamsifikia Kinafiki ili kumjaza Upepo ajiaminishe na tarehe 28 Oktoba 2020 kama Kawaida yetu wana CCM wa Kawe tutamuonyesha kuwa ndiyo Mabingwa wa Kusaliti na Kupiga Kura za Maruhani ( za Kukomoa ) tu"

Kauli muhimu niliyoisikia kutoka katika Msafara wa Mdee ni hii nainukuu hapa chini:
"Tunachojua tu ni kwamba Mdee ni bonge la Mbunge ila anakomolewa na kuhujumiwa sana tu na Serikali Kuu ili aonekane hafai na CCM waweze Kutumia huo mwanya na Kumtoa. Kama kuna Mtu ambaye CHADEMA tulikuwa tunamuogopa Kawe kutoka CCM alikuwa ni Yule Kijana wao Furaha kwakuwa Kwanza tulikuwa hatumjui vyema ila wana CCM Kawe ndiyo alikuwa Chaguo lao Kubwa.

Kwa kutuwekea huyu Mchungaji, Muhuni na Mnafiki CHADEMA tunajua tunashinda Asubuhi na tayari kuna Wanachama wengi tu wa CCM wametuambia kuwa kwa sasa watajifanya kuwa karibu na Mtu Wao ila Kura zao kwa 85% watampigia Mdee
"

Msafara wa CCM ulikuwa ni mkubwa, ila Watu wake walikuwa wakishangiia huku Wamenuna, lakini wa CHADEMA walikuwa ni wachangamfu sana.
😀😀😀😀😀😀😀😀😀 unaandika hivyo ili kujisafisha, Mdee amepoteza ajira yake ya Ubunge.
Stay tuned
 
Kuna watu hapa jukwaani mtu unatamani kuwafahamu in person! GENTAMICINE, hupindishagi, unaandika unachoamini, unamshinda kwa mbali pasco na John Baptist ambao, asilimia 99 ni full mapambio tu, 1% wakilewa wanakosoa chama chao!
Pili ambayo siyo muhimu sana kwa hapa, asante sana Wewe na kamati yako ya roho mbaya kule inakoendaga pantoni!
 
Mtajitekenya sana this time.

Jimbo la Kawe linarudi CCM
Thubutu.
Mimi mpiga kura wa Kawe. Gwajj boy hapiti. Wanaccm wengi nilionao kwenye makundi ya whatsapp hawatamchagua kwa sababu kubwa mbili. Moja ni kumkashifu Kadinali Pengo. La pili ni kuwakashifu Waislamu.
Lipo hili pia la ile video ya ngono, japo halisemwi sana.
 
Kuna watu hapa jukwaani mtu unatamani kuwafahamu in person! GENTAMICINE, hupindishagi, unaandika unachoamini, unamshinda kwa mbali pasco na John Baptist ambao, asilimia 99 ni full mapambio tu, 1% wakilewa wanakosoa chama chao!
Pili ambayo siyo muhimu sana kwa hapa, asante sana Wewe na kamati yako ya roho mbaya kule inakoendaga pantoni!

Kuwa Kwangu mwana CCM ( Shabiki Lia Lia ) hakunizuii Mimi ama Kuwakosoa au Kuwapongeza CCM kwani sina pia Msamiati wa Unafiki na Uwoga.
 
Kauli muhimu niliyosikia kutoka katika Msafara wa Gwajima ni hii nainukuu hapa chini:
"Yaani CCM na Mwenyekiti wetu hawajajifunza kutoka kwa Wagombea wa huko nyuma na bado tu wameendelea na Upuuzi wao ule ule wa Kututeulia wale tusiowataka hapa Kawe. Kwakuwa tunajua huyu ana Hela na hata Mwenyekiti wake na Chama chake kitampa Pesa ila Sisi tutakachofanya tutamlia Pesa zake, tutamsifikia Kinafiki ili kumjaza Upepo ajiaminishe na tarehe 28 Oktoba 2020 kama Kawaida yetu wana CCM wa Kawe tutamuonyesha kuwa ndiyo Mabingwa wa Kusaliti na Kupiga Kura za Maruhani ( za Kukomoa ) tu"

Kauli muhimu niliyoisikia kutoka katika Msafara wa Mdee ni hii nainukuu hapa chini:
"Tunachojua tu ni kwamba Mdee ni bonge la Mbunge ila anakomolewa na kuhujumiwa sana tu na Serikali Kuu ili aonekane hafai na CCM waweze Kutumia huo mwanya na Kumtoa. Kama kuna Mtu ambaye CHADEMA tulikuwa tunamuogopa Kawe kutoka CCM alikuwa ni Yule Kijana wao Furaha kwakuwa Kwanza tulikuwa hatumjui vyema ila wana CCM Kawe ndiyo alikuwa Chaguo lao Kubwa.

Kwa kutuwekea huyu Mchungaji, Muhuni na Mnafiki CHADEMA tunajua tunashinda Asubuhi na tayari kuna Wanachama wengi tu wa CCM wametuambia kuwa kwa sasa watajifanya kuwa karibu na Mtu Wao ila Kura zao kwa 85% watampigia Mdee
"

Msafara wa CCM ulikuwa ni mkubwa, ila Watu wake walikuwa wakishangiia huku Wamenuna, lakini wa CHADEMA walikuwa ni wachangamfu sana.
Umeona uandike mawazo yako kisha useme umeyasikia kwa watu.😂😀
 
Je, na Wewe JamiiForums imekuzuia Kutuandikia Fikra zako tena zilizo tofauti kabisa na hizi zangu zikiwa ni za 'Kumfagilia' Gwajima wako Uridhike?
 
Back
Top Bottom