GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Huu ni mfumo wa 99.9% kujilinda (Defensive) hasa ukiwa na historia kuwa ikicheza kwao huwa inakuwa na kasi na inafunguka sana tu.
Wanasimba S.C. tusijidanganye, hawa waangola ni watamu (wazuri) hakuna mfano, hasa wakiwa kwao nchini Angola na wanapiga pasi nyingi nyingi na za haraka haraka. Kitu ambacho kama wachezaji wa Simba S.C. hawatobadilika kwa mpira wao wa nyoro nyoro (ubishoo), zile hamsa hamsa (tano tano) za Congo DR kwa AS Vita na Al Ahly za kipindi kile naziona wikiendi hii siku ya Jumapili.
Twendeni na huu mfumo wa 'Kikatili' wa 4-5-1 (mtindo wa kupaki basi), ambapo tunajaza mabeki wanne nyuma, tunajaza viungo tupu watano katikati na kule mbele tunawategeshea mshambuliaji mmoja tu Phiri, awahenyeshe na wahangaike naye.
ONYO: Simba S.C. na kocha Mgunda chonde chonde tusiende kufunguka mazima Angola tutakufa (tutapigwa) nyingi, ila twende tukajihami sana (too defensive) huku tukishambulia kwa mkwara (kushtukiza), ili kazi tuje kuimalizia kimkakati Dar es Salaam, Tanzania kwa Mkapa na tufuzu rasmi katika Makundi ya CAFCL.
Ukiona hadi GENTAMYCINE natoa ushauri huu wa kiufundi, jua nimeshawatazama 'Waangola' na kwa jicho langu kali la kimpira na kiufundi. Nimeamua kuwapa ukweli ili muanze kuchukua tahadhari mapema kabla ya dhahama (hatari).
Poti wangu (kutoka mkoani Mara), Crescentius Magori (mshauri mkuu wa mwekezaji, CEO na benchi la ufundi Simba S.C.) najua kuwa huwa unanisoma mno GENTAMYCINE hapa JamiiForums, hivyo nakuomba lichukueni hili na mlifanyie kazi upesi kwani hawa 'Waangola' siyo wepesi kama ambavyo tunajidanganya na kujipa moyo mitaani.
Ninaitakia kila la kheri tu Simba S.C.!