Kumbe burundi haina tofauti yoyote na rwanda.mimi nilippenda kigali mwaka jana nilitarajia kukuta bonge la maendeleo lakini sijaona lolote jipya.kuna watu wengi,tangu rusumo border hadi kigali miji ipo karibu karibu mno nakumbuka tulikoswa hata sehemu ya kupaki gari nikojoe.watu ni wengi mno barabarani wengi wao wakitembea kwa miguu kwa ajili ya kutafuta vibarua hasa vya kulima.watoto wa shule ndo usiseme sasa ni wengi mno na wengi wamevaa yeboyebo hata wale wa sekondari.gari za rwanda ni za kizamani mno inaonekana kuna sheria fulani kandamizi huruhusiwi kumiliki gari mpya,majengo yao ovyo sana mfano fisherboard zao ni bati linachanwa linatumika kama ubao..gari kutembea 40kph ukizidisha tu camera ina wewe maana zimefungwa kila baada ya kilomita kadhaa nchi nzima.daladala zao lazimA uwe na kadi maalum hulipi cash ndio maana watu wanashindw a kupanda magari wengi hutumia bodaboda na hata baiskel na miguu pia.
Yapo mengi sana niliyoyadharau rwanda