Kwa niliyoyaona Burundi, itoshe kusema Tanzania ni nchi tajiri sana

Kwa niliyoyaona Burundi, itoshe kusema Tanzania ni nchi tajiri sana

Asante Kwa taarifa,sijafika Burundi Wala Sina mpango wa kwenda huko.
Nilikuwa naamini Burundi ni kuchafu Sasa umenikazia maarifa .
By the way Africa Kuna nchi masikini sana ukifika tashangaa
1) central Africa
2)Togo
3) Mozambique ( hasa northern party)
4) Burkina Faso Kwa kina Aziz ki
5)Chad
6) DRC
7) Madagascar
8) Mali
9) Niger
10) Eritrea
11)congo Brazzaville
12) sudani kusini
13)Ethiopia ( usione Wana midege,ni malofa haswa)
14) Benin
15)Liberia
...........
Mozambique nimefika, unachosema ni kweli ni kama bado wapo miaka ya 90's hata usafiri shida tu
 
Sifa gani sasa,kigali mjini ni kuzuri ila foleni sasa ndo usipime bora hata ilivyokuwa morogoro road kabla ya fly over.,kingine kilichonitisha ni doria za wanajeshi mida ya jioni wakiwa na silaha kali na zile radio call kubwa wamezibeba migongoni utadhani wanaingia vitani.nilishukuru kurudi tz salama
Kigali nimefika, mji msafi ila ni mdogo, huwezi linganisha na dar, ila Nairobi iko juu sana, nilifika nikakubali imejengeka kuliko dar
 
Thibitisha wewe uliejitenga na dini umetoboa kwanza halafu ndo nifuate ushauri wako. Unatengenezewa mpaka toothpick unakuja kuleta story za dini hapa. Halafu mi navojia matheist wengi ni wavuta bangi na walevi wa kutupwa sasa lete data hapa kati ya walevi wavuta bangi na watumia madawa ya kulevya na data za kanisani wapi kuna umasikini mkubwa. Mwafrica hutoboi namba moja huna akili hata hiyo dini ina hasa kufanya kazi unasema eti nd inaleta umasikini. Hutaki kuzungumzia ufisadi elimu duni ulevi uvutaji wa madaw ya kulevya na uzinzi unaleta story za vijiweni kuwa dini inafelisha watu.Makanisani kuna masikini wengi sababu ndo sehemu pekee sauti zao husikila na kuthaminiwa na kuheshimiwa utu wao huonekana huko. Masikini akienda club anaishia kudharirika kuomba omba bia akienda kwenye siasa anaishia kunyang'anywa na alichonacho na hasikilizwi akienda kwenye uzinzi anadharaulika na hao wanawake shuleni anadhaurika ila kanisani anaheshimiwa na anasikilizwa anapata marafiki anaoneshwa upendo halafu anakuja mvuta bangi mmoja anapita dirishani anaenda kuhadithia wenzie fulani ni masikini sababu anashinda kanisani.
Amka usingizini, hiyo ilikuwa zamani sikuhizi makanisani kumejaa umbea na mtu anaangaliwa sadaka kama si mtoaji au hana cha kutoa anakosa sauti na anakuwa haheshimiki wala kushirikishwa kwenye maamuzi au vyeo hapati. Mtu anaangaliwa mafanikio huko makanisani mpaka maskini wanapata stress huko
 
Watu masikini wanaenda makanisani kutafuta faraja mmekazana kusema dini ndo imeleta umasikini sasa waliendaje kanisani wakiwa masikini bado. Hao machokoraa nao wanashinda makanisani emu acheni chuki binafsi na dini. We unaechukia dini unanua bando la mb 300 sasa nd umekomboka na nini hapo wakati kuna watu wanatoa sadaka milion 100 kanisani na wana marange rover.
Ukiona nchi au eneo flani la nchi lina wafuasi wengi wa dini jua vilevile kuna umasikini mwingi na hawana kazi ya kufanya zaidi ya kukesha makanisani kujiliwaza na neno la Mungu.Na ukitaka kuwa maskini kupindukia kuwa muimba kwaya wa kanisa.
 
Burundi kuwa koloni la Ufaransa?

Historia ya primary au secondary hiyo?
Burundi ilikua koloni la German East Africa pamoja na Tanzania na Rwanda, baada ya Ujerumani kushindwa vita vya 1, vya dunia, Burundi na la Rwanda zikaenda kwa Belgium iliokua ikitawala Kongo, kumbuka hao Wabelgiji wanaongea Kifaransa, kwahiyo ni sawa kusema Kongo, Rwanda na Burundi wametawaliwa na Ufaransa. N.B, Nchi ya Ubelgiji nusu ya Nchi wanaongea Kifaransa na nusu nyingine ni Kidachi.
 
Back
Top Bottom