Kwa niliyoyaona Burundi, itoshe kusema Tanzania ni nchi tajiri sana

Alilipa gharama nyingi za yule mgonjwa Masikini aliekosa msaada, sio kuhisi ni kweli alikua Tajiri

Soma vizuri hio hadithi Luka 10:30-37 au ukitaka kuelewa vizuri anzia kusoma Luka 10:23

Soma vizuri Luka 10:34 alitumia mafuta na divai kutibu majeraha yake ya yule mgonjwa, vitu ambavyo sio vya gharama ndogo gharama ilianzia hapo, unaambiwa akampandisha juu ya Punda wake, yaan hadi hapo unabaini kabisa bila shaka yoyote huyu mtu hakua kapuku, enzi hizo Punda ni sawa sawa na Harrier New Model au Toyota Pride TX (chuma kikali) kwa sasa,

Tajiri alimpandisha juu ya Punda wake alafu akampeleka nyumba moja ya wageni, NI sawa Leo umuokote mtu sehemu ambapo hakuna hospital umpelekee hotel ya Nyota 3/5 kumuuguza au hata Lodge apate sehemu nzuri ya kulala Ila unamlipia chumba Cha kulala wageni (gharama hii) huyu mtu hakua Masikini,

Ukisoma Luka 10:35 Yesu mwenyewe narudia Yesu mwenyewe anaendelea kusimulia anakuambia, Kesho yake (huyu Tajiri Mapesa) akatoa Pesa/Fedha kiasi Cha Dinari Mbili narudia akatoa Fedha kiasi Cha Dinari Mbili (unaelewa unachoambiwa) alitoa fedha Dinari Mbili (kwa sasa unaweza linganisha na Million 2) maana yake huyu hakua kapuku hakua Masikini hakua chokambaya huyu alikua ni Taita Tajiri Mapesa Mzee wa Vibunda, akachukua hio Dinari Mbili huyu Tajiri Mapesa akampa yule mwenye nyumba, akamwambia, Muuguze mtu huyu; na chochote utakachotumia zaidi, nitakulipa nitakaporudi,

Tajiri Mapesa akasema kwa kujiamiini na Chochote kikizidi kwenye kumuuguza huyu kwa hii Million 2 (Dinari Mbili) Cha ziada nitakulipa nitakaporudi, alisema hivyo akimaanisha Mimi ni Tajiri sio Masikini akimaanisha Mimi sio kapuku nina Pesa za kutosha za kuweza kulipa hadi gharama za ziada, hayo ni maneno ya Yesu mwenyewe

Ukiendelea Luka 10:37 Yesu akahoji ni Nani aliemuonea huruma ? Wakajibu ni huyu Tajiri Mapesa aliemuuguza na kumpa Matibabu pamoja na hifadhi yule masikini bila kudai chochote kiasi Cha kulipa mpaka gharama za ziada ndie aliemuonea huruma nae Yesu akamwambia basi 'Nenda ukafanye vivyo hivyo'

Elewa Logic & Moral of the Story
 
Maana kutoka Mkuranga hadi Kibaha, Kerege, Pugu pote huko pameendelea
Hapajaendelea kivile, lakini toka Kigali nenda nje kidogo tu tena sio mbali pamechoka balaa na udongo wao mwekundu, kelele nyingi lakini majority ni maskini wa kutupa. Juzi wamesombwa na mafuriko huko ukiona ule umaskini unaweza kulia.
 
Hapajaendelea kivile, lakini toka Kigali nenda nje kidogo tu tena sio mbali pamechoka balaa na udongo wao mwekundu, kelele nyingi lakini majority ni maskini wa kutupa. Juzi wamesombwa na mafuriko huko ukiona ule umaskini unaweza kulia.
Ni sawa na majiji mengi ya Tz ukisogea KM 10 utashangaa mf Mbeya, Dodoma, Arusha
 
Wewe unaonekana unaabudu mali ila hujajijua tu. Moral of the story zinaelezea utoaji wewe unazungumzia utajiri yani unatafuta kitu cha kukutoa kanisani au kukufurahisha. Yesu alisem uza mali zako zote gawia masikini kama alimtolea mfano huyo tajiri je una uhakika gani kuwa huyo mtu hakujtoa mali yake yote.
 
Unaelewa hio maana ya Uza Mali zako zote Gaia masikini au na wewe umekurupushwa usielewe alimaanisha nini ?

Sio matajiri matapeli wauwaji waporaji wa masikini wezi majambazi km wanaojifanya manabii huko Kenya Ezekiel Odero & Paul Mackenz
 
Unaelewa hio maana ya Uza Mali zako zote Gaia masikini au na wewe umekurupushwa usielewe alimaanisha nini ?

Sio matajiri matapeli wauwaji waporaji wa masikini wezi majambazi km wanaojifanya manabii huko Kenya Ezekiel Odero & Paul Mackenz
Mimi nimeelewa ndiyo kuwa uza mali zako gawia masikni au hichi ni kiingereza. Sas wewe sema wapi wameandika wanaotakiwa kusali ni matajri peke ake?
 
Upo sawa. Kama mtu hajawahi kutoka nje ya mipaka ya nchi yetu, atakuwa akikomenti Kimanzese manzese, Kivingunguti nguguti, Kimatogole gole n.k
 
Aliyenacho ataongozewa. Asiyenacho atapokonywa hata kile kidogo alichodhani anacho
 
Aliyenacho ataongozewa. Asiyenacho atapokonywa hata kile kidogo alichodhani anacho
Umemaliza mkuu

Hayo ni maneno ya Yesu mwenyewe anasema 'Mwenye nacho ataongezewa, asienacho hata kile kidogo alichonacho atanyang'anywa'
Mathayo 25

Hio maana take ni kwamba Pesa, Fedha, Manukato, Mavumba huwatembelea wenye Pesa au lugha rahisi michongo/deals huwatembelea wenye michongo/deals tu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…