Good observation! Sio vyema kulinganisha Tanzania na Burundi. Ni kama mbungu na ardhi kabisa. Kuanzia size ya nchi mpaka rasilimali. Ukichangia na chuki iliyojaa ndani ya nchi yao, ni kama ndimu kwenye mboga.
Hakuna kitu kibaya katika taifa kama vita. Inaweza kurudisha Taifa miaka 10 nyuma kiuchumi, Jamii na maendeleo. Burundi iliingia kwenye civil war nadhani kuanzia 93 mpaka katkati ya miaka ya 2000. Safari yao ni ndefu sana kuelekea kwenye maendeleo. Hawana bahati aliyokuwa nayo Rwanda, ambayo baada ya ile genocide, nchi za Dunia nzima ziliungana kusaidia kuijenga Rwanda upya.
Mfano, UK peke yake ilichukua jukumu la kulipa mishahara ya Rwanda's Civil Cervants kwa miaka 10. Bila shaka usimamiI mzuri wa Rasi Kagame kuhakikisha kwamba nidhamu ya hali ya juu inakuwepo ili kuzuia ubaadhirifu na wizi wa misaada iliyokywa inaletwa na nchi ulaya pamoja na mashirika ya kimataifa ilisaidia sana kuleta maendeleo haraka. Burundi kamwe hatapata hio nafasi. Safari yao bado ni ndefu sana.
Kabla hiyo nchi haijakumbwa na hayo matatizo, Burundi ilikuwa imetulia sana. Wakati huku kwetu tunakula Unga wa sembe wa msaada kutoka US (Unga wa njano) wao walikuwa mambo Safi. Bidhaa zilikuwa zimejaa madukani na kwenye masoko. Wafanyabiashara wengi walienda huko kunua mitumba Kuja kuuza bongo.
Kwetu vitu vilikuwa vinapatikana kwenye Maduka ya kaya tena kwa foleni, wao hakukuwa na hayo matatizo. Bongo Watu wakaambiwa wafunge mkanda kwa miezi 18 kukubali dhiki, ikaenda mpaka miaka zaidi ya 15. Fikiria, hayo ni madhara ya vita vya Tanzania/ Uganda ya mwaka 1 tu. Burundi wamepigana wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miaka 20.
Enzi hizo, Kuna Wafanyabiashara kutoka Burundi, walikuwa wanakuja Dar, mtaa ya Kinondoni na vitenge kutoka Holland, wanavikata saisi ya Kanga, Duh! Walikuwa wanakula dada zetu pale mjini mpaka roho inakuuma. Lakini mwenye kisu kikali ndie hula nyama.
Leo hii nchi yao imerudi nyuma miaka 30 kwa sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Nchi ndogo, population kubwa, rasilimali chache na geopolitically haina ushawishi wowote, Safari yao ni ndefu sana. Bado watakiona cha mtama kuni.