zerominus10
JF-Expert Member
- Aug 25, 2022
- 8,142
- 13,721
Alilipa gharama nyingi za yule mgonjwa Masikini aliekosa msaada, sio kuhisi ni kweli alikua TajiriCONCERN YANGU NI HAIKUANDIKWA ALIPITA TAJIRI AKAFANYA JAMBO AU WALIPITA MASIKINI WAKAPITA PEMBENI, SIJAKATAA KWAMBA TAJIRI ALIFANYA JAMBO JEMA ILA NI KWAMBA HAYO MANENO ALIPITA TAJIRI UMEJIONGEZA LABDA KWA KUWA ALILIPA HOTELI NA MATIBABU NDIO MAANA UKAHISI NI TAJIRI
Soma vizuri hio hadithi Luka 10:30-37 au ukitaka kuelewa vizuri anzia kusoma Luka 10:23
Soma vizuri Luka 10:34 alitumia mafuta na divai kutibu majeraha yake ya yule mgonjwa, vitu ambavyo sio vya gharama ndogo gharama ilianzia hapo, unaambiwa akampandisha juu ya Punda wake, yaan hadi hapo unabaini kabisa bila shaka yoyote huyu mtu hakua kapuku, enzi hizo Punda ni sawa sawa na Harrier New Model au Toyota Pride TX (chuma kikali) kwa sasa,
Tajiri alimpandisha juu ya Punda wake alafu akampeleka nyumba moja ya wageni, NI sawa Leo umuokote mtu sehemu ambapo hakuna hospital umpelekee hotel ya Nyota 3/5 kumuuguza au hata Lodge apate sehemu nzuri ya kulala Ila unamlipia chumba Cha kulala wageni (gharama hii) huyu mtu hakua Masikini,
Ukisoma Luka 10:35 Yesu mwenyewe narudia Yesu mwenyewe anaendelea kusimulia anakuambia, Kesho yake (huyu Tajiri Mapesa) akatoa Pesa/Fedha kiasi Cha Dinari Mbili narudia akatoa Fedha kiasi Cha Dinari Mbili (unaelewa unachoambiwa) alitoa fedha Dinari Mbili (kwa sasa unaweza linganisha na Million 2) maana yake huyu hakua kapuku hakua Masikini hakua chokambaya huyu alikua ni Taita Tajiri Mapesa Mzee wa Vibunda, akachukua hio Dinari Mbili huyu Tajiri Mapesa akampa yule mwenye nyumba, akamwambia, Muuguze mtu huyu; na chochote utakachotumia zaidi, nitakulipa nitakaporudi,
Tajiri Mapesa akasema kwa kujiamiini na Chochote kikizidi kwenye kumuuguza huyu kwa hii Million 2 (Dinari Mbili) Cha ziada nitakulipa nitakaporudi, alisema hivyo akimaanisha Mimi ni Tajiri sio Masikini akimaanisha Mimi sio kapuku nina Pesa za kutosha za kuweza kulipa hadi gharama za ziada, hayo ni maneno ya Yesu mwenyewe
Ukiendelea Luka 10:37 Yesu akahoji ni Nani aliemuonea huruma ? Wakajibu ni huyu Tajiri Mapesa aliemuuguza na kumpa Matibabu pamoja na hifadhi yule masikini bila kudai chochote kiasi Cha kulipa mpaka gharama za ziada ndie aliemuonea huruma nae Yesu akamwambia basi 'Nenda ukafanye vivyo hivyo'
Elewa Logic & Moral of the Story