Kwa nini huwezi kula ugali bila Mboga?

Kwa nini huwezi kula ugali bila Mboga?

Blue Bahari

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2016
Posts
1,851
Reaction score
2,171
Wanajukwaa habari zenu!
Hivi umewahi kujiuliza, Kwa nini Mboga ni za lazima au muhimu unapokula ugali?
Je, umewahi kula ugali bila mboga yoyote ile? Inawezekana? Haiwezekani?
Kuna makundi makuu ya virutubisho ya vyakula: (1)wanga (2) protein (3) madini Chumvi (4) fibers/roughage (5) vitamins.

Ugali wa Mahindi uko katika kundi la wanga wakati Kwa upande wa Mboga inaweza toka katika kundi la protein au vitamini (mbogamboga) na roughage (Mbogamboga).
Ugali ambao unatoka katika kundi la wanga siku zote lazima Mboga ziwepo. Kwa nini Mboga za aina yoyote ile lazima ziwepo?

Nimeuliza swali hilo Kwa kuwa Kuna vyakula vingine Vya wanga ambavyo vinaweza kuliwa bila mboga. Kwa mfano, Mihogo ya kuchemsha, wali, viazi utamu (sweet potatoes), viazi ulaya (Irish potatoes), magimbi, maboga, ndizi , n.k. Vyakula vyote hivyo Vya wanga unaweza kula bila mboga, isipokuwa ugali. Kwa nini?
Je, ni utamaduni?
Je, ni mitazamo yetu?
Je, wewe ulishawahi kula ugali bila mboga?, ilikuwa poa?
 

Attachments

  • WhatsApp-Image-2023-03-22-at-1.41.21-PM-768x576.jpeg
    WhatsApp-Image-2023-03-22-at-1.41.21-PM-768x576.jpeg
    36.8 KB · Views: 11
  • Beef-Stew-Ugali-017-1.jpg
    Beef-Stew-Ugali-017-1.jpg
    1.8 MB · Views: 14
tamaduni tu na mazoea sio kwamba huwezi kula bila mboga unaweza sema itakuwa haijakaa kimasta sana nafikiri unaelewa!..
 
Hivyo vyakula vyote ulivyavitaja lazima ule na mboga mhogo ndizi na vyote ulivyotaja mboga yake ni kachumbali au chai soda na kadhalika ukikosa kabisa utakula na maji hata wali huwezi kula bila mboga
Sawa! lakini ni rahisi kula wali bila mboga lakini ugali bila mboga ni ngumu kidogo. Au we unasemaje?
 
Back
Top Bottom