Kwa nini huwezi kula ugali bila Mboga?

Kwa nini huwezi kula ugali bila Mboga?

Watu wa hali ya chini wengi wanakula ugali na mboga.
Wenye uwezo wanakula mboga na ugali.
Bila D mbili huwezi nielewa.
 
Porini kwenye kuwinda tulikua tunachoma ugali kwenye kuni unaiva na tunakula bila mboga na maji tunakunywa, Ugali na asali nayo pia tumekula sana , ugali na maziwa mgando tumekula sana, hata feitoto ashakula ugali na sukari sana tu
 
Watu wa hali ya chini wengi wanakula ugali na mboga.
Wenye uwezo wanakula mboga na ugali.
Bila D mbili huwezi nielewa.
Haya tufafanulie siye tuliorisiti form IV mara nne na bado tumeangukia pua.
 
Porini kwenye kuwinda tulikua tunachoma ugali kwenye kuni unaiva na tunakula bila mboga na maji tunakunywa, Ugali na asali nayo pia tumekula sana , ugali na maziwa mgando tumekula sana, hata feitoto ashakula ugali na sukari sana tu
Ugali na asali na mimi pia nimekula.
Asali Ina protein na glucose Kwa wingi. Haina tofauti na anayekula ugali na chai.
 
Wanajukwaa habari zenu!
Hivi umewahi kujiuliza, Kwa nini Mboga ni za lazima au muhimu unapokula ugali?
Je, umewahi kula ugali bila mboga yoyote ile? Inawezekana? Haiwezekani?
Kuna makundi makuu ya virutubisho ya vyakula: (1)wanga (2) protein (3) madini Chumvi (4) fibers/roughage (5) vitamins.

Ugali wa Mahindi uko katika kundi la wanga wakati Kwa upande wa Mboga inaweza toka katika kundi la protein au vitamini (mbogamboga) na roughage (Mbogamboga).
Ugali ambao unatoka katika kundi la wanga siku zote lazima Mboga ziwepo. Kwa nini Mboga za aina yoyote ile lazima ziwepo?

Nimeuliza swali hilo Kwa kuwa Kuna vyakula vingine Vya wanga ambavyo vinaweza kuliwa bila mboga. Kwa mfano, Mihogo ya kuchemsha, wali, viazi utamu (sweet potatoes), viazi ulaya (Irish potatoes), magimbi, maboga, ndizi , n.k. Vyakula vyote hivyo Vya wanga unaweza kula bila mboga, isipokuwa ugali. Kwa nini?
Je, ni utamaduni?
Je, ni mitazamo yetu?
Je, wewe ulishawahi kula ugali bila mboga?, ilikuwa poa?

Logic yako umeipindisha makusudi ili useme unachotaka, umetoa mfano wa mihogo unaweza kula ya kuchemsha tu, kwani mahindi ukichemsha mbona yanalika pasipo kitu chochote tu fresh.

Muhogo wenyewe ukiusaga unga wake ukapikia ugali huwezi kula ugali wa muhogo pasipo mboga.
 
Ndo mkubali ugali sio chakula tunaforce tu kujaza tumbo!
 
Logic yako umeipindisha makusudi ili useme unachotaka, umetoa mfano wa mihogo unaweza kula ya kuchemsha tu, kwani mahindi ukichemsha mbona yanalika pasipo kitu chochote tu fresh.

Muhogo wenyewe ukiusaga unga wake ukapikia ugali huwezi kula ugali wa muhogo pasipo mboga.
Ugali ni ugali haijalishi ni wa Mahindi, mihogo, mtama, uwele, ulezi, ndizi, n.k.
Je, kati ya ugali unaotokana na nafaka yoyote ile unaweza kula bila mboga?
 
Ugali ni ugali haijalishi ni wa Mahindi, mihogo, mtama, uwele, ulezi, ndizi, n.k.
Je, kati ya ugali unaotokana na nafaka yoyote ile unaweza kula bila mboga?

Katika hali ya kawaida (sio shida) ni ngumu kula ugali mkavu. Ni suala la utamaduni zaidi kuwa ugali huenda na mboga. Ila katika shida ya ukimbizi ama baa la njaa ugali mkavu unalika vizuri tu.
 
Mbona hata Mahindi unaweza ukala bila mboga unaweza kuchoma au kuchemsha. Ulivyotaja vinaweza liwa bila mboga ni kwasababu asilimia kubwa havikaondolewa uasili wake(kukobolewa).0

NB:ugali unatokana na mahindi,mtama,mihogo nk yaliyokobolewa
 
Dogo langu hapa maskani hua nmpa ugali free na anabomoa tu Bila kujal.
 
Back
Top Bottom