Kwa nini jeshi la mtandaoni la JPM waliacha kusapoti awamu ya sita ya mama?

Kwa nini jeshi la mtandaoni la JPM waliacha kusapoti awamu ya sita ya mama?

Hamna mtu mgumu kumtetea kama huya Maza...hata kama wewe ni mfata mkumbo huwezi jitokeza maana huna point.

Ukpgwa swali 1 tu unaweza nyamaza na usiongee milele
 
Kadi za wajawazito kulipiwa ni sawa tu, kama unazaa lazima ushiriki kubeba gharama. Hata elimu ilitakiwa kuchangia, sikubaliani na elimu bure.
Umeuliza tofauti ya wakati wa Samia na JPM.
Kwa hivyo nikakutajia mojawapo hiyo.
Suala la kukubaliana na kutokubaliana juu ya hizo huduma za bure ni mjadala mpana. Na Mimi nimesema mwanzo ni mjamaa.
Hiyo ni Sera ya kijamaa.
Na ndiyo sababu nilimuunga mkono mjamaa JPM.
Nawewe ulikuwa haumuungi mkono sababu siyo muumini wa ujamaa.
 
KUongoza nchi kwa kufata alichokua akifanya mwingine bila kuwa na mikakat ni kujimaliza.

Uyu mama anapewa bichwa aongoze kimabavu maana yeye ndio TOP ila anashndwa elewa huwez kuongoza kimabavu kama kuna watu huwez wagusa.

Ili uwe mbabe inatakiwa watu wote makundi yote yawe chini yako, sasa huyu ana act n mbabe wakat kuna watu wamemueka mfukoni.

Naamini huyu ndio rais wa kwanza matajiri wa hii nchi wana namba yake ya simu direct kuliko rais yyte.. kama mtu anaweza inua simu akapga direct kwa Rais na mko nae Mtaani, hii n nini??

Apge aongee chamaana basi eti SALAMU tu... sijawahi ona hii kitu

Watu wamemueka Mfukoni yani nchi inaendeshwa na jirani ako mtaa wa pili kama wewe hujui...

Maana kila mwenye wazo lake analipeleka direct na linafanyiwa kazi papo hapo, Liwe bovu liwe zuri as long mtoa wazo Kamueka kimama mfukoni, Utaskia "Usijali Fredrick watalishughulikia hilo" dk 5 sio nyingi Simu inaingia unaambiwa Bwqna Fredrick endelea na ulichokua unafanya kibali kitakuja...

Ngojea kwanza wakope na B.O.T pesa ziishe pyuuuuu tuwe kaam uganda ndo tutaongea lugha 1...

Bi maza kama sio ule ulinzi alio nao aaanh tungeshaimba parapanda Mudaaaaa
 
Umeuliza tofauti ya wakati wa Samia na JPM.
Kwa hivyo nikakutajia mojawapo hiyo.
Suala la kukubaliana na kutokubaliana juu ya hizo huduma za bure ni mjadala mpana. Na Mimi nimesema mwanzo ni mjamaa.
Hiyo ni Sera ya kijamaa.
Na ndiyo sababu nilimuunga mkono mjamaa JPM.
Nawewe ulikuwa haumuungi mkono sababu siyo muumini wa ujamaa.
Suala la elimu bure mnayofikiria ni bure huyu mama si amefanya hadi kidato cha sita, sasa kwa nini humuungi mkono??
Mimi sipingi elimu au matibabu bure, napinga propaganda za elimu bure, huwezi kusema elimu ni bure kisa tu umeondoa elfu ishirini kwa mwaka halafu wanafunzi wanachangishwa michango sijui ya chakula, ulinzi, tuition na makorokoro mengine Kibao.
 
... piga picha vurugu alizofanyiwa Samia ndo angefanyiwa JPM! ... HAIELEZEKI MAANA JAMAA ALIWEKA WAZI ZAIDI .............!
Ingekuwa massacre mara mbili zaidi.
JPM kiasi fulani alikuwa na washauri sahihi kwa baadhi ya mambo.
Uliona Lissu na akina Heche waliachwa wagombee na hawakuwa kizuizini.
Sasa awamu iliyofuata Nini kilitokea?
Kwa hivyo so kweli dhana yenu kwamba JPM angetoa amri au angeruhusu mauwaji ya kikatili vile.
Na Mimi nina uhakika Samia yeye binafsi haikuwa hiyari yake kuachia watu wauwe kiasi kile.
Kuna watu wa hovyo wahuni walimuingiza mtegoni.
Yeye namlaumu kwa kukosa ujasiri kukataza jambo lile au kushindwa 'kujiudhuru' (resign).
 
Kusema ukweli enzi za JPM alikuwa na watu mtandaoni haswa. Kama hapa JF alikuwa na Kijiji kweli cha watu, wanaanzisha nyuzi mpya kila dakika, wanashambulia nyuzi kujibu mashambulizi, wanaripoti accounts au nyuzi zifungiwe au ziondolewe na wanatishia watu ikibidi.

Jina la buku saba lilianzia kipindi hiko, sijui kama kweli walikuwa wanalipwa au hawailipwi ila walikuwa wanafanya kazi kwa kushambulia kama Nyuki. Alipoingia tu mama wote waliendelea kwa miezi michache ila wakaanza kupukutika kwa kasi sana, nusu wakigeuka wapinzani na nusu wakipotea kabisa jukwaani.

Sasa hivi akaunti za enzi za JPM zinazosapoti utawala wa mama hapa JF hazizidi hata tano zikiasiadiana na akaunti nyingine activu mbili tatu ingizo jipya ambazo hazina vibe, machachari na ile amshamsha kama enzi za JPM.
Interesting.

Wengine wamebadili majina na kujifanya watu wa hekima sana kinyume na wehu waliokuwa nao! Wengine wanajaribu kwenda na CCM ya mama dhidi ya CHADEMA lakini kinyonge kwa kuchechemea sana. Wakibanwa wanadai hawana chama eti wanasimamia ukweli tu!

Wengine wamehamia mazima kuwa wapiga debe wa nguvu wa CHADEMA hasa enzi za Lissu wakidai tatizo lao lilikuwa Mbowe tu.

Mimi binafsi nilitamani JPM aishi muda wote hadi akamilishe ajenda zake zote alizopanga. Kwani niliona kuna mambo mengi yaliyofichika ambayo yangeweza kubainika TU kwa kukamilika kwake. Nilisikitika sana alipofariki mapema vile akiwa "katikati" ya prime time ya Urais wake akiacha mambo mengi na ahadi "zinazoning'inia". Baadhi ya ndugu zangu hasa walioko serikalini, kwa kutonielewa, wananilaani sana kwa tamanio hilo. Wao wanaamini JPM angekaa hadi leo nchi ingekuwa kuzimu (Hell)!

Wakongo wana usemi maarufu kuwa siku zote ukweli hupanda ngazi. Pengine hii inaweza kuwasaidia Watanzania wengi kufunguka akili hasa katika masuala makuu ya kitaifa. Wangi hujifunza baada ya matokeo (consequences).

Leo hii nii ngumu sana kuwa na mjadala wa kimantiki na watu wengi nchini. Ni hisia, mapenzi (affection), imani na maslahi ndivyo vinavyotawala mitizamo ya wengi. Facts na ukwelii usioendana na yaliyo kwenye nafsi zao hawautaki! Wanaweza hata kukutangazia uadui kwa kuuonyesha ukweli wasioutaka!
 
Suala la elimu bure mnayofikiria ni bure huyu mama si amefanya hadi kidato cha sita, sasa kwa nini humuungi mkono??
Mimi sipingi elimu au matibabu bure, napinga propaganda za elimu bure, huwezi kusema elimu ni bure kisa tu umeondoa elfu ishirini kwa mwaka halafu wanafunzi wanachangishwa michango sijui ya chakula, ulinzi, tuition na makorokoro mengine Kibao.
Hakuna elimu bure kwa sasa.
Limebaki tamko Ila nyuma ya pazia mambo tofauti.
Kuna agizo vitu vingi wazazi wachangie.
Tumechangia printer, .insurator, PA music system, chakula cha mchana, n.k.
Michango mingi ikijumlishwa afadhali wangetoza karo (Ada) 400,000 au 500,000 kwa mwaka tungelipa.
Wangeajiri waalimu wa masomo yote, wangefuta ujinga wa remedial za kulipia.
Watoto wetu wangerudi mapema majumbani wajifunze na stadi za maisha sijui za kazi zingine nyumbani.
Tungewapa na tuition nyumbani.
Sasa hivi hali mbaya sana hasa miji mikubwa kama DSM.
Tumeletewa na waalimu wa hovyo toka Zanzibar wanauwa elimu yetu ifanane na Zanzibar.
 
Nahisi wewe haupo Tanzania kwa Sasa.
Unasikia na kusoma mitandaoni tu.
 
JPM kiasi fulani alikuwa na washauri sahihi kwa baadhi ya mambo.
Uliona Lissu na akina Heche waliachwa wagombee na hawakuwa kizuizini.
Sasa awamu iliyofuata Nini kilitokea?
Kwa hivyo so kweli dhana yenu kwamba JPM angetoa amri au angeruhusu mauwaji ya kikatili vile.
Na Mimi nina uhakika Samia yeye binafsi haikuwa hiyari yake kuachia watu wauwe kiasi kile.
Kuna watu wa hovyo wahuni walimuingiza mtegoni.
Yeye namlaumu kwa kukosa ujasiri kukataza jambo lile au kushindwa 'kujiudhuru' (resign).
Kwenye sakata la Korosho alisema alikuwa anasuburi huko Kusini waandamane aanze kupiga kwanza shangazi zao.
 
Nilikuwa mfuasi au shabiki wa CHADEMA nikachukizwa na kitendo cha CHADEMA kubadili gia angani na kumpitisha Lowassa kuwa mgombea uraisi.
Wakaanza kutetea mafisadi.
Wagogo tunasema "chili hamonga". Tuko pamoja.

Ni jambo jema ukiwa na msimamo. 2015 nililazimika kumpigia kura Magufuli japo nilikuwa mwanachama wa chadema, na mpaka sasa siwaelewi kabisa walioshabikia ujio wa lile tapeli.
 
Kwenye sakata la Korosho alisema alikuwa anasuburi huko Kusini waandamane aanze kupiga kwanza shangazi zao.
Kusema na kutenda vitu viwili tofauti.
Kupiga na kuuwa vitu viwili tofauti.
Mmoja alitishia kupiga mwingine aliuwa kabisa.
 
Hakuna elimu bure kwa sasa.
Limebaki tamko Ila nyuma ya pazia mambo tofauti.
Kuna agizo vitu vingi wazazi wachangie.
Tumechangia printer, .insurator, PA music system, chakula cha mchana, n.k.
Michango mingi ikijumlishwa afadhali wangetoza karo (Ada) 400,000 au 500,000 kwa mwaka tungelipa.
Wangeajiri waalimu wa masomo yote, wangefuta ujinga wa remedial za kulipia.
Watoto wetu wangerudi mapema majumbani wajifunze na stadi za maisha sijui za kazi zingine nyumbani.
Tungewapa na tuition nyumbani.
Sasa hivi hali mbaya sana hasa miji mikubwa kama DSM.
Tumeletewa na waalimu wa hovyo toka Zanzibar wanauwa elimu yetu ifanane na Zanzibar.
Hakujawahi kuwa na elimu bure Tanzania tofauti na enzi ya Nyerere tu.
 
Tuna deni la trion 114 miradi ya pesa zilizokopwa hatuzion unamteteaje huyu mama ! Ukiamka asubuhi ukifungua media unasikia mtu kanyakuliwa kama mwewe vilio kila kona watu wakiwatafuta ndugu zao bila majibu ! Kazi ya kumtetea huyu mama ni ngumu lucas mwashamba ndiye anaiweza
Mushuma
 
JPM kiasi fulani alikuwa na washauri sahihi kwa baadhi ya mambo.
Uliona Lissu na akina Heche waliachwa wagombee na hawakuwa kizuizini.
Sasa awamu iliyofuata Nini kilitokea?
Kwa hivyo so kweli dhana yenu kwamba
Watanzania tunasahau haraka sana. Kweli leo JPM aliyewatuma akina Bashite wamshindilie RISASI 16 mwilini Tundu Lissu akiwa Bungeni Dodoma mwaka 2017, amekuwa mbaya kuliko Samia aliyemweka Ukonga??.
 
Hakujawahi kuwa na elimu bure Tanzania tofauti na enzi ya Nyerere tu.
Kikwete, Mkapa na Mwinyi waliweka mchango mdogo sana sawa na elimu bure. Hakukuwa na michango lukuki ya awamu ya Samia.
Shuleni watoto walifundishwa kweli.
Sasa hakuna kitu.
 
Kusema na kutenda vitu viwili tofauti.
Kupiga na kuuwa vitu viwili tofauti.
Mmoja alitishia kupiga mwingine aliuwa kabisa.
Titicomb you are completely brainwashed na Magufulication. Aliyetufikikisha hapa ni Magufuli, laiti asingetokea mwaka 2015 akaja Rais mwingine tusingekuwa na haya matatizo tuliyonayo sasa. Try to use your grey matter positively if you have it
 
Kusema ukweli enzi za JPM alikuwa na watu mtandaoni haswa. Kama hapa JF alikuwa na Kijiji kweli cha watu, wanaanzisha nyuzi mpya kila dakika, wanashambulia nyuzi kujibu mashambulizi, wanaripoti accounts au nyuzi zifungiwe au ziondolewe na wanatishia watu ikibidi.

Jina la buku saba lilianzia kipindi hiko, sijui kama kweli walikuwa wanalipwa au hawailipwi ila walikuwa wanafanya kazi kwa kushambulia kama Nyuki. Alipoingia tu mama wote waliendelea kwa miezi michache ila wakaanza kupukutika kwa kasi sana, nusu wakigeuka wapinzani na nusu wakipotea kabisa jukwaani.

Sasa hivi akaunti za enzi za JPM zinazosapoti utawala wa mama hapa JF hazizidi hata tano zikiasiadiana na akaunti nyingine activu mbili tatu ingizo jipya ambazo hazina vibe, machachari na ile amshamsha kama enzi za JPM.
Assume hiyo kazi upewe wewe.

Utamsifia Samia kwa kitu gani, hana miradi ya maendeleo

Amekandamiza haki za kiraia pengine kuliko hata Somalia
 
Back
Top Bottom