Nguvu moja
JF-Expert Member
- Oct 20, 2017
- 3,371
- 2,713
Utamchukua kutoka kwao kijijini, kumleta mjini hana ndugu wala hamfamu mtu, mbaya zaidi ajui lolote si ajabu....akachukua viatu akaweka ndani ya fridge, na mkeo akawa anamfundisha kupika mapishi, baada ya siku kadhaa kupita, kashakuwa mwerevu, zaidi ya nyie wenyeji wake mliomleta na mbaya zaidi hata kariakoo hapajui, sasa kaingia mjini kajua kupaka matope yao usoni, na marafiki wa nje, kaota masikio ashikiki wala haambiliki, wewe mwenye nyumba umuogope yeye, na uchoyo juu, kwenye chakula wewe mnunuzi, siku umekuja na nyama ya kuku firigisi na minofu anajiwekea yeye, nyinyi anawawekea shingo kichwa, na kipapatio kama si miguu, na mengineyo mengi si ajabu na uchawi au wanga juu, hizi zote changamoto azikosekaniki kwa hawa viumbe kwa nini lakini wanajisahau....na hawakumbuki walikotoka!