...Baada ya yeye kuagiza bapa, nikaona isiwe tabu ngoja nami nijitutumue badala ya bia tunywe wote Konyagi, wakati mimi nakunywa kwa uoga uoga, maana huwa sinywagi mara kwa mara Konyagi, yaani haikuchukua round mzinga umekatika!
Nikaagiza mwingine tena, nikaona inaanza kunichukua, mrembo kwa kuwa ni mzoefu akatoa wazo tupate kongoro kwanza, then mbuzi choma.
Yaani mpaka mida ya saa nne usiku nikaona naanza kukata network, but uzuri ni kwamba alikuwa mstaarabu alinisindikiza mpaka Guesti nilipofikia maana nilianza kupotea njia tukaagana.
Asubuhi yake akanipitia (ilikuwa J1) but alifanya kazi ya ziada kunigongea mpaka nikaamka, baada ya kuoga tukaenda kupata supu, sprite baridi na maji meengi baridi ndo nikawa fresh kidogo. Kwa kweli kama angekuwa siyo mstaarabu angenikomba kila kitu maana tulikunywa Konyagi sanaa siku hiyo, na baadae akaja kuwa very close friend of mine na tukasaidiana mengi sana.