chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Nikifika Mwanza eneo la kapripoint, nafurahishwa na namna jinsi wachora ramani walivyoyaweka majengo yakaishi na nature, bila kuharibu mazingira. Kuna tatizo la ubunifu. Ukiangalia majengo mengi nchini ni kama majengo yanafanana, hakuna utundu. Niliwahi kutoa challenge watu wajadili ubunifu katika majengo ya serikali pale Mji wa Mtumba. Nani alikuwa mound na mbunifu?
Sasa huko Musoma wanataka kukata mti wa kihistoria kisa wanajenga soko. Mbona pale mbuyuni barabara ya Alhassan Mwinyi Tanroad waliubakiza. Pale Mwanza roundabout ya CCM ule mti ulibaki kulinda historia kwamba wajerumani walitumia kunyongea?
Manispaa ya Musoma bado mna fursa ya kulinda na kutunza historia. Huo mti unaweza kuwa kivutio kikubwa na kuashiria utunzaji mazingira.