Kwa nini mti maarufu soko la Nyasho ukatwe ili kujenga soko? Kwa nini isiwe sehemu ya kuenzi historia? Wachora ramani mnafeli wapi kujumuisha nature?

Kwa nini mti maarufu soko la Nyasho ukatwe ili kujenga soko? Kwa nini isiwe sehemu ya kuenzi historia? Wachora ramani mnafeli wapi kujumuisha nature?

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Nikifika Mwanza eneo la kapripoint, nafurahishwa na namna jinsi wachora ramani walivyoyaweka majengo yakaishi na nature, bila kuharibu mazingira. Kuna tatizo la ubunifu. Ukiangalia majengo mengi nchini ni kama majengo yanafanana, hakuna utundu. Niliwahi kutoa challenge watu wajadili ubunifu katika majengo ya serikali pale Mji wa Mtumba. Nani alikuwa mound na mbunifu?

Sasa huko Musoma wanataka kukata mti wa kihistoria kisa wanajenga soko. Mbona pale mbuyuni barabara ya Alhassan Mwinyi Tanroad waliubakiza. Pale Mwanza roundabout ya CCM ule mti ulibaki kulinda historia kwamba wajerumani walitumia kunyongea?

Manispaa ya Musoma bado mna fursa ya kulinda na kutunza historia. Huo mti unaweza kuwa kivutio kikubwa na kuashiria utunzaji mazingira.

Screenshot_20250226-084401.jpg
 
Mti wa round about ya ccm mwanza si ulisha ondolewa ule na sasa walijenga kwa siment mfano wa mti ulokatwa.
 
Back
Top Bottom