Kwa nini Mungu wa Biblia na Quran ana hulka za wanaume na tabia nyingi za mfumo dume (patriarchy) ?

Kwa nini Mungu wa Biblia na Quran ana hulka za wanaume na tabia nyingi za mfumo dume (patriarchy) ?

Ushahidi wa mwanaume mmoja ni sawa na ushahidi wa wanawake wawili. Mungu anajua vizuri hekima yake juu ya hili na kiuhalisia ni rahisi kwa mwanamke kutoa ushuhuda kwa mihemko kuliko mwanamume. Ndio maana tapeli Mwamposa hupenda kutumia wanamama kutoa shuhuda kuliko wanawake. Mwanamke anaweza kutumia machozi yake na jamii ikaamini anayoyasema kuwa ni ukweli tofauti na mwanamume.
 
Ukiangalia maandiko yanayohusu mungu wa Kiyahudi/ Abrahamic god ambaye ndiye wa Wakristo na Waislamu utaona k

10. Agano la kale Wanawake walihesabiwa kuwa sehemu ya mali na hawakujumlishwa katika idadi ya watu.
huyo Mungu wa kuanzwa kwa herufi ndogo (kimaandishi) huyo ni wa kwako huyo, Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo aandikwapo lazima aanzwe kwa herufi kubwa. Huyu ni Mungu wa miungu, Bwana wa mabwana, Mfalme wa wafalme. Yehova YWHW, Mungu wa Israeli.

tafsiri ya neno baba maana yake ni mwanzilishi au chanzo. Mungu ni baba kwa sababu yeye ndiye chanzo cha kila kitu- Vinavyoonekana na visivyoonekana.
 
huyo Mungu wa kuanzwa kwa herufi ndogo (kimaandishi) huyo ni wa kwako huyo, Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo aandikwapo lazima aanzwe kwa herufi kubwa. Huyu ni Mungu wa miungu, Bwana wa mabwana, Mfalme wa wafalme. Yehova YWHW, Mungu wa Israeli.

tafsiri ya neno baba maana yake ni mwanzilishi au chanzo. Mungu ni baba kwa sababu yeye ndiye chanzo cha kila kitu- Vinavyoonekana na visivyoonekana.
Vipi kwa lugha ambazo hazina herufi kubwa na ndogo? Utagundua hata weww kung'ang'ania herufi ni nonsense tu
 
Vipi kwa lugha ambazo hazina herufi kubwa na ndogo? Utagundua hata weww kung'ang'ania herufi ni nonsense tu
Akifika kwa Wachina na Mandarin yao watamuona amechanganyikiwa
 
  • Thanks
Reactions: Lax

Attachments

  • 1787410899140.jpg
    1787410899140.jpg
    99.9 KB · Views: 5
Mfumo dume haukutamalaki kama ajenda ya kisiasa au kiharakati, isipokua ulitamalaki kwa kufuata njia za asili. Kwa kipindi hicho hivyo vitabu vinaandikwa jamii zilikua zinaishi katika mfumo dume, hawakua wanajua chochote kuhusu masuala ya usawa wa kijinsia. Ndio maana Mungu akatengenezewa taswira ya mwanaume.

Mambo ya usawa wa kijinsia yamekuja kuibuka juzi juzi tu. Usawa wa kijinsia sio asili ya kimaumbile, ndio maana ni lazima ufanyiwe kampeni kuenezwa. Leo wazaliwe watoto wa kiume na wa kike, halafu waachwe mpaka wawe watu wazima bila kufundishwa chochote kuhusu feminism wala patriarchy. Wote fahamu zao zitawatuma kufuata mfumo dume. Hata, hivyo pamoja na kufanyiwa promotion bado kuna vipengere feminism haiwezi kutuondolea utata. Mfano provision na kwenda vitani.
 
Mfumo dume haukutamalaki kama ajenda ya kisiasa au kiharakati, isipokua ulitamalaki kwa kufuata njia za asili. Kwa kipindi hicho hivyo vitabu vinaandikwa jamii zilikua zinaishi katika mfumo dume, hawakua wanajua chochote kuhusu masuala ya usawa wa kijinsia. Ndio maana Mungu akatengenezewa taswira ya mwanaume.

Mambo ya usawa wa kijinsia yamekuja kuibuka juzi juzi tu. Usawa wa kijinsia sio asili ya kimaumbile, ndio maana ni lazima ufanyiwe kampeni kuenezwa. Leo wazaliwe watoto wa kiume na wa kike, halafu waachwe mpaka wawe watu wazima bila kufundishwa chochote kuhusu feminism wala patriarchy. Wote fahamu zao zitawatuma kufuata mfumo dume. Hata, hivyo pamoja na kufanyiwa promotion bado kuna vipengere feminism haiwezi kutuondolea utata. Mfano provision na kwenda vitani.
Misri ya Kale kulikuwa na kiwango kikubwa cha usawa wa kijinsia na mythologies za miungu ya kike yenye nguvu sana.
 
Misri ya Kale kulikuwa na kiwango kikubwa cha usawa wa kijinsia na mythologies za miungu ya kike yenye nguvu sana.
Andiko lako umetumia rejea ya hizi abrahamic religions ambazo ni Judaism, Christianity na Islamic.
 
Huu ni utata mkubwa sana
Kijakazi , unaweza kuona mambo ya sexual punishment hata hayajaanzia kwa Waarabu.

lkn hapo siyo wanaume kubakwa na kundi la wanaume wengine kama adhabu, nafikir kuna tofauti btw google Bacha bazi kama ukipenda uone ushetani unaofanyika huko muslim world ...

 
"The enemy of feminism isn't men."(It's patriarchy)
And patriarchy is not men(It is a system)

And women can support the system of patriarchy just as men can support the fight for gender and equality"

Sio maneno yangu,ex wa Elon Musk.. Joslin Musk
 
Wasioamini with the Bible again! ! !

Nyie ni kama mwanamke anayemkataa mwanamume kwa kumtoa kasoro zote halafu kutwa anamuongelea! ! ! !

Tabia ya kuchanganya Biblia na maandishi mengine muache.

Na MUNGU wetu msimfananishe na miungu mingine.


1) a) MUNGU sio kiumbe, sio mwanamume wala mwanamke.

Kaamua kujifunua kama mwanamume ili tumuelewe.

Ushawahi kujaribu kumuelezea mtoto hukusu topic ambayo unajua kwa akili yake hawezi kuelewa? Au sio wakati wake? Mtoto akiuliza mtoto wanaingiaje kwenye tumbo la mama tunawaambia mume na mke wakilala usingizi mtoto anaota tumboni!

Watoto wa MUNGU watakapopewa miili mipya watakuwa nao sio wanawake wala wanaume. Hawazai. Tutakuwa kama YESU aliyefufuliwa. Hafi tena milele.


b) Roho takatifu ambaye ni MUNGU ana sifa ambazo unaweza kusema ni za kike:

Anaitwa msaidizi
Anaitwa mfariji (Comfoter)
Anatuombea kwa MUNGU

Ruach, neno ya kiyahudi linalotafsiriwa kuwa roho wa MUNGU kwa kiyahudi, ni neno la kike kisarufi (feminine noun).

MUNGU anasema kama mama anavyomfariji mtoto ndivyo nitakavyokufariji. (Isaya 66:13)


c) Mambo ya Male female ukiachana na Mungu kuumba hivyo ili viumbe wazae, lakini ni issue niite ya "kilimwengu". Yaani ya kimwili. Ya kinyama. Kwa kiumbe wa kiroho including malaika huko juu ni issue ya hadhi ya chini. Sub par.

Kwasababu baada ya kutimiza lengo la tofauti hizo yani kuzaa, kinachobaki kwa binadamu ni Mungu wake!

(Topic ya kwanini Mungu awaumbe wa mwili wa kuzaa just to change them baadaye ni topic nyingine. Inshort MUNGU wetu yuko nje ya muda. All these revelations and learnings are for us not him.)

Ndomana hata lengo la ndoa ni utakatifu, yani upate mwenzako wa kukusaidia kumsogolea MUNGU ukiwa huku duniani: kwa kukusaidia kubaki msafi, kuwa kama kioo ili ujirekebishe, kwa kuambatana nawe kuitafuta na kuiishi Kweli.

Wengine wana bypass haya ya kimwili, wanakuwa watawa, they go straight to the main purpose.

Ndomana wakati watu wanakazana kuihubiri laana ya kuwa chini na kutawaliwa na mwanamume, YESU akaja akasema mpende mkeo kama unavyojipenda. Kuna tofutai kubwa ya mtu anayemuangalia mkewe kama yeye mwenyewe, na mwingine anayemuona mkewe kama mlaaniwa wa kutawaliwa! ! ! !

YESU kaja kuchora mstari kutofautisha mwanume mwenye roho yake na asiye nayo.

Kwa Kristo hakuna Male or Female. We're one in Christ.

Shetani amefanikiwa kugeuza hii fact kama kawaida yake na kufanya ionekana kuwa unaweza kuvuka mipaka ya kibayolojia. Madumejike.

THIS IS NOT WHAT THERE IS NO MALE NOR FEMALE MEANS!


d) Women teach. Women prophecy. Women preach.

Lakini kwenye haya majengo ya makanisa tumeshapewa muongozo wanaume ndo waongoze. Mpango ndio huo tunaenda kiitifaki. And I can think of many reasons why, sitoandika mambo mengi muda mchache.

Hata mimi siendi kwenye kanisa linaloongozwa na mwanamke. Sio kwasababu namdharau kwasababu ni mwanamke. Ni kwamba kama alivyokataa agizo clear kabisa na mimi namkataa. Itifaki zizingatiwe.

I follow a lot of women who share bible knowlege online na unaona kabisa theres is no way you figured this out by yourself inshort wana roho wa Mungu. But sio viongozi wa kanisa wanaosimama mbele ambapo hata wasioamini wanawaona.


i) Nabii Hulda mke wa Shalumu, alifuatwa na makuhani wa MUNGU na watumishi wa mfalme Yosia ili awafafanulie unabii. Akatangaza na hukumu ya MUNGU dhidi ya Yerusalemu. - 2 Wafalme 22:10-20


ii) Nabii Debora mke wa Lapidothi, alikuwa mwamuzi (hakimu). Aliongoza jeshi. Aliagizwa na MUNGU akamuambie Baraki aandae majeshi aende kupigana na Wakanaani. Baraki akamuambia Nabii Debora kama huendi na mimi na mimi siendi. Debora akasema sawa nitaenda nawe lakini hutopata heshima ya ushindi kwasababu maadui watatiwa mkononi mwa mwanamke. - Waamuzi 4:4-22.

iii) Priskila na mume wake Akila walimfundisha Apolo Myahudi aliyemuamini Kristo. Paulo aliwaita Priskila na mume wake "wafanyakazi wenzake katika utumishi". - Matendo 18:24-28, Rom 16:3, 1Kor 16:9, 2Tim 4:19


iv) YESU alivyofufuka alimtuma mwanamke ndo atangaze! Maria Magdalene.


iv) Wanawake kizazi cha mwisho watatangaza ujio wa YESU:

"Hata itakuwa, baada ya hayo, nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili. Wana wenu wa kiume na wa kike watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono.

Hata juu ya watumishi wangu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile nitamimina Roho wangu.

Nami nitaonesha maajabu katika mbingu na duniani: damu, moto na mawimbi ya moshi.

Jua litageuzwa kuwa giza na mwezi kuwa mwekundu kama damu, kabla ya kuja siku ya Bwana ile kuu na ya kutisha."

Yoeli 2:28-31.NENO2025


2) MUNGU amejifananisha na mwanamume na amejiita majina mengi ya kijemedari na ya kivita. Na ni bora iwe hivyo kwasababu ni MKUU wa yote kabla ya mengine yote.

Lakini sio hayo tu!


a) Katuzaa.

"Mkamwacha Mwamba, aliyewazaa ninyi; mkamsahau Mungu aliyewazaa."
Kumbukumbu.32.18.NENO2024


b) Ni kama mama anayenyonyesha asiyesahau mwanaye.

“Je, mama aweza kumsahau mtoto aliye matitini mwake akinyonya, wala asiwe na huruma juu ya mtoto aliyemzaa? Ingawa anaweza kusahau, mimi sitakusahau wewe!"
Isaya.49.15.NENO2025


c) Yesu alitamani kuwatunza wayahudi kama kuku anavyotunza vifaranga vyake.

Utakuta lipepo linajifananisha na jogoo ili lipande kila tetea. Mungu wetu amejifananisha na kuku mwenye vifaranga.

“Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetamani kuwakusanya watoto wako pamoja, kama vile kuku akusanyavyo vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka!"
Mathayo.23.37.NENO


d) Ni kama mwanamke anayejifungua

"Kwa muda mrefu nimenyamaza; nimekaa kimya na kujizuia. Lakini sasa, kama mwanamke wakati wa kujifungua, ninapiga kelele, ninatweta na kushusha pumzi."
Isaya.42.14.NENO2025

Kwa kifupi MUNGU wetu atakuwa vile atakuwa. Ndomana alisema jina lake ni I AM. Mimi ndiye.

Usim limit
kwamba yuko juu hawezi kuja huku chini. Mbona alikuja.

Usim limit kwamba alienda huko kuzimu hatotoka. Alitoka akarudi juu alikotoka.

Usim limit kuwa akiwa hapa duniani atakuwa sehemu moja tu. Ndomana YESU alindoka ili Roho Mtakatifu anayeweza kuwa kila mahali aje.

Usim limit kuwa ni mwanamume jemedari wa vita. Ni comfoter na helper.

Usim limit kuwa ni mwanaume kwasababu ameoa kanisa. Amezaa. Hii ni misemo.

Usim limit kwamba ni mkali ndomaana hakucheka na wowote kwenye agano la kale ukamkimbia, ndiye huyo huyo alikuja kulipia makosa yako.


Usim limit
kwamba ni mpole ndomana akaacha watu wamuue na anaacha uovu leo, ndiye huyo huyo mnayemuogopa / mnayemchukia wa agano la kale, na anarudi kiagano la kale na Upanga.

Usim limit.

I AM - YHWH.


3) Kuhusu sheria za MUNGU nyie msioamini hamna utashi wa kuziongelea. Sio tu hamzijui zaidi ya kujitia ujuaji, mnapotosha kwa makusudi kumchafua Mungu wetu.


a) Kwa kifupi kusema sheria za uzinzi / uasherati ni kali kwa mwanamke ni UONGO.

Ukikamatwa na msichana bikra unamuoa.

Ukikamatwa na msichana asiye bikra mnauawa wote wawili.

Ukikamatwa na mke wa mtu mnauawa wote wawili. Ndomana yule mwmwanamke mzinzi aliyepelekwa kwa YESU alipona. Walimtuhumu anavunja sheria huku wao wenyewe wanavunja sheria, huyo mwanamume aliyekamatwa naye yuko wapi muwaue wote? Yakawashuka!


b) Hedhi sio haramu kwenye bibilia. Ni kutokuwa msafi. Na kutokuwa msafi sio hivyo mnavyoiona nyie kwamba wanatia kinyaa.

Maana hata majemedari yaliyotoka vitani kushinda vita vya Bwana nao walikuwa sio wasafi kwasabanu ya kumwaga damu na kushika maiti, kuna vitu hawakuruhisiwa kufanya kwa muda. Au mtu aliyetoka kushiriki mazishi naye alikuwa sio msafi.

Mwanamke anayetokwa damu hakupaswa kushika chochote. Anakaa kula bata wiki nzima. Hamna kupika, kulisha mifugo, kuchota maji.

Mwanamke gani leo hii akiambiwa akiingia period anapewa off hadi damu ziishe pote ofisini ma nyumbani atasema anadharauliwa! ! ! !

Kutokuwa msafi kwa mwanamke mwenye hedhi sio kuwa amekataliwa, bali amepishwa! Kimalkia kabisa yani.


Inageuka tatizo ikiwa kama yule aliyetokwa na damu miaka 12 akaja kuponywa na YESU. Sasa utaishije miaka 12 bila kufanya kazi. Ku socialize. Kwenda kuabudu.


c) Mwanammue aliyeoa hakuruhusiwa kwenda vitani mwaka mzima. Kwanini? Sheria inasema ili amfurahishe mke wake mpya! !

Na huyuo ndiye MUNGU wetu!

Honeymoon mwaka mzima. We umeona wapi?

"Kama mtu ameoa karibuni, kamwe asipelekwe vitani au kupewa wajibu mwingine wowote. Kwa mwaka mmoja atakuwa huru kubaki nyumbani ili amfurahishe mke aliyemwoa."
Kumbukumbu.24.5.NENO2025


4) Sadaka za agano la kale ni kivuli cha sadaka ya kamilifu ya YESU.

Matokeo ya dhambi ni kifo. Kulipia dhambi lazima uhai utolewe, damu imwagwe. Hiyo ni sheria ya haki ya milele.

Damu za wanyama haziwezi kutuondolea dhambi milele zaidi ya kuzifunika mwa muda. Imagine kuishi maisha yako yote na wasiwasi wa dhambi zako na kuua wanyama kila siku ili upate clear conscience ya kuishi.

Wanaoshindwa kuua wanyama wanaishi kumuua YESU kila siku. Inabidi wapite wanatangaza kila siku kuwa YESU hayupo. Wanapata satisfaction kwa muda lakini inabidi warudi tena kumuua baada ya wiki 😭.

Sadaka ya mwili wa YESU ndiyo sadaka pekee kamilifu, iliyotolewa mara moja kwa ajili ya binadamu wote, na wote wanaoikubali ni viumbe vipya. Hawaishi chini ya utumwa wa dhambi, wala wasiwasi wa dhambi, na kuua kila siku.


5) Hiyo ya kutohesabiwa wewe sijui unaichukuliaje. You see what you want to see.

Me naona strategy ya kijeshi na simplified math.

Hesabu the strongest point. Baba mama watoto wanne under five. Bora kujua kuna mtu mmoja tu hapo!

Hata kwenye kuhesabu resources. Wanaume mko wangapi 10. Tuna assume una wategemezi watano each. So we multiply that by the number of men.

Tunaongelea taifa teule lililoshuhudia Mkono wa Bwana huko Misri ukishughulikia watesi wao wa miaka 400 mpaka watesi wakawapigia goti,

Taifa lililoshuhudia mkono wa Bwana ukigawa bahari ili wapite, na kumezaadui nyuma yao,

taifa lililoshuhudia wingu kuu likiwangoza mchana na moto kubwa ukiwaongoza usiku,

lililoshuduia chakula kikishushwa kutoka mbinguni for 40years.

Jaribu sana kufocus hapo wakati unawasoma.

Sasa wewe wasome kama ni mtu aliyetokea kutoka kwa ndoa ya wazazi wanaogombana kila siku, kawa abused akiwa mdogo, ukubwani napo matukio ya kutosha halafu anaambiwa ale honeymoon mwaka mzima, au anaambiwa akiwa kwenye hedhi asishike chochote! ! ! ! !



Eh nimechoka
 
Sasa unataka Mungu awe na tabia za kikekike mkuu? Hebu kuwa serious bas
 
Andiko lako umetumia rejea ya hizi abrahamic religions ambazo ni Judaism, Christianity na Islamic.
Sahihi, inawezekana wao mungu wao hakuwapa akili za kuzingatia usawa na haki za wanaume kama vile miungu ya Misri ilivyowapa Wamisri huo uelewa.
 
Ameandikwa na wao.


Namba 10, ndio sababu ya kwanini huwa sitaki mtu afanye reference kwenye hivi vitabu katika mijadala fulani fulani.
Hata wakati mnaumbwa mmetoka kwenye ubavu wetu. Acha kujizima data mwili wako na strength zinatoa majibu yote
 
Hakika nimeamini mimi ni mtu mbaya sana mpaka jamiiforums inaniogopa😎
 
Back
Top Bottom