Kwa nini Muslim University of Moro hawatumii Central Admission Syst (CAS)

Status
Not open for further replies.

M24 Headquarters-Kigali

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2012
Posts
8,199
Reaction score
8,186
Nimekuwa nikijiuliza kwa nn hiki chuo bado kinatumia system ya zamani ya kudahili wanafunz wake wenyewe bila kupitia Central Admission system (CAS) ya TCU kama vyuo vingine vya elimu a juu?Je ni kwamba w wapo juu ya TCU? Je TCU hawalioni hili? TAFAKARI
 

Kama kawaida....choko choko kila kitu cha waislam.....gubu la roho mbaya limeganda nafsi zenu...
 

mfumo wa TCU ulipokuja hiki chuo waliukataa na waliweka sababu za kuukataa,sababu kubwa waliyosema ni kwamba wanafunzi wengi watashindwa kujiunga na chuo hicho kwa sababu ya CUT OFF POINT ZA TCU katika kudahili wanafunzi ambazo zinatokana na universal eligibility ya mtu kusoma chuo kikuu,

hivyo wakasema hawako tayari kutumia mfumo huo,kifupi walilenga watoto wa kiislam ambao wengi wao huwa wanadahiliwa pale na kati ya hao wengi huwa hawana vigezo vya moja kwa moja kudahiliwa chuoni hapo mpaka kwanza wapewe kozi fupi na wakifaulu basi wanaruhusiwa kujiunga na chuo,na wao wanatumia mfumo ule wa kuchukua wanafunzi na kuwafundisha kwa muda maalumu ili wafanye mtihani na waweze kufikisha alama za kuingia chuo,sikumbuki utaratibu huu unaitwaje,ila ulikuwa unatumika na vyuo vingi na hata sasa DIT wanautumia kwa wanaotaka kusoma diploma ila marks zao haziruhusu,sasa wangeweka TCU wao hawatumii utaratibu huu katika system maana matokeo yanayohitajika ni ya NECTA O LEVEL NA NECTA ADVANCE,hayo ya mtu kwenda kupigwa kwanza msasa kabla HAWAYATAMBUI,kwa sasa unaweza kusema kuwa wao wanachukua hata wanafunzi wasio na sifa ya moja kwa moja kujiunga chuo,ila wanawadahili baada ya kuwafundisha kozi fupi na kuwapa mtihani na wakifaulu mtihani huo basi wanadahiliwa,

sema haya mambo ya udini ndio yanaharibu na serkali waliwaogopa sijui maana kila siku hawa watu wanalalamikia serikali kuwanyanyasa na waliwaacha huku vyuo vingine wakilazimishwa kuingia TCU.
 
Kama kawaida....choko choko kila kitu cha waislam.....gubu la roho mbaya limeganda nafsi zenu...

MBONA UNA MUNKARI HIVI?kwani ni vibaya kuuliza?wewe hauoni kama ni ajabu kuwa vyuo vingine vyote vinatumia mfumo wa TCU kasoro hicho?
je unajua kwa nini?kama unajua tuambie na kama hujui soma majibu ya wanaojua ni kwa sababu gani na kukurupuka tu kuanza kuona mnaonewa.
 
Ni utaratibu tu, hata wewe unaweza ukaanzisha chuo na kuwaandikia TCU kwanini hutaki kujiunga na system iliyopo kwa kutoa facts.

Hata hivyo unapewa muda fulani kwa ajili ya hizo claims zako na kisha kwa baadae unajiunga baada ya hizo claims kufanyiwa kazi.
 

St. Augustine pia hii system ya kudahili wasio na sifa ipo na inaitwa 'remedial' kwa wale ambao hawakufaulu vizuri huwahi chuoni na kusoma kwa miezi kadhaa na baada ya hapo hupewa mitihani na watakaofaulu basi hujiunga moja kwa moja na degree na kwa watakaofeli hushauriwa kujiunga na cheti.
 
Si kweli sababu ulizotoa. Usiaminishe jukwaa habari za uongo, na kama una yakini na uyasemao weka ushahidi hapa
 
Wewe umesema kweli ila huyo aliyesema eti ni kutokana na kudahili wanafunzi kwa njia ya remedial haiwezi kuwa kweli
 

asante sana mkuu kwa ufafanusi.kuna jambo nimebaini,ni kwamba utaratibu wao huo una wa favour watoto wao wa kiislamu ambao hawana sifa kudahiliwa na TCU.the opposite to this is,kama MUM kingekuwa kinapokea wanafunzi walio dahiliwa na TCU peke yake,wanafunzi wakristu wangekuwa wengi dhidi ya wale wa kiislamu ktk chuo cha kiislamu.lol
 

Wanaodahiliwa mum hawana sifa stahiki za kusoma university na hata kama wanazo hawawezi kuingia kwenye ushindani.
 


acha uongo
 

Sio vyote vpo tcu mkuu
 
Wanadahili wanafunzi kupitia madrasa
 
Aliyenayo tunaomba atuwekee sheria, mwongozo wa serikali, agizo au chochote kile palipoandikwa kwamba chuo cha elimu ya juu lazima kitumie Central Admission System.
 
Si kweli sababu ulizotoa. Usiaminishe jukwaa habari za uongo, na kama una yakini na uyasemao weka ushahidi hapa

sasa umejuaje kama siyo kweli?wewe ulikuwa unajua kama chuo cha kiislamu morogoro walikataa kuingia kwenye mfumo wa TCU?NA kama hujui unapataje nguvu za kusema ni uongo?ama kila kitu ni kutetea tu kama dini hata kama ni makosa?hii siyo mistari ya maandiko matakatifu.

mtu huelewi lolote alafu unakimbilia kukataa na kusema kuwa ni uongo.nadhani hunifahamu vizuri katika mijadala humu maana huwa sisemi mambo nisiyoyajua,huwa sisemi jambo kama halipo na huwa siongezi chumwi na huwa siongopi,nimeshiriki mijadala mingi sana humu ndani yenye hoja nzito lakini kamwe huwa sitii chumvi.

wakati chuo hiki wanakataa kuingia TCU walitoa taarifa na hazikuwa siri na hizi ndizo sababu walizotoa kama chuo.

wakati naandika maelezo haya najua fika kuwa kuna wanafunzi wamesoma pale,wapo wakufunzi wa pale na hata viongozi wa chuo wapo,na hata wakija hapa hawawezi kukanusha maelezo yangu kwa sababu ndio wao walitoa.

tatizo watu wengi ni wavivu wa kufatilia mambo na habari mbalimbali alafu hao hao wanajitia kujua kupita kiasi huku pengine hawajui kabisa,na kama sikosei swala hili lilitokea kati ya 2010 ama 2011.

WATU WALIOKUWEPO PALE CHUONI NAWANGOJEA WAJE HUMU NA HATA WAKUFUNZI WAKANUSHE KAMA SI KWELI.
lakini siwezi kuendelea kubishana na mtu anaengozwa na hisia sijui za nini.
 
Sheria ya Tcu ya mwaka 2005 inavitaka vyuo vyote vitumie mfumo huo. Tcu wanayo mamlaka ya kukifungia chuo chochote. Lakn zipo coz ambazo hawazitambui. Na zikifundishwa zinabaki kama ceremonial. Hzo za madrasa ni mojawapo. Nadhan hapo kuna jambo flan nyuma ya pazia,kwan vipo vyuo vilivyofungiwa na Tcu kwa kudahili wanafunz nje ya utaratibu.so mum nadhan wanabebeka tu mbeleko ikikatika basi inaweza kuwa nouma.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…