mfumo wa TCU ulipokuja hiki chuo waliukataa na waliweka sababu za kuukataa,sababu kubwa waliyosema ni kwamba wanafunzi wengi watashindwa kujiunga na chuo hicho kwa sababu ya CUT OFF POINT ZA TCU katika kudahili wanafunzi ambazo zinatokana na universal eligibility ya mtu kusoma chuo kikuu,
hivyo wakasema hawako tayari kutumia mfumo huo,kifupi walilenga watoto wa kiislam ambao wengi wao huwa wanadahiliwa pale na kati ya hao wengi huwa hawana vigezo vya moja kwa moja kudahiliwa chuoni hapo mpaka kwanza wapewe kozi fupi na wakifaulu basi wanaruhusiwa kujiunga na chuo,na wao wanatumia mfumo ule wa kuchukua wanafunzi na kuwafundisha kwa muda maalumu ili wafanye mtihani na waweze kufikisha alama za kuingia chuo,sikumbuki utaratibu huu unaitwaje,ila ulikuwa unatumika na vyuo vingi na hata sasa DIT wanautumia kwa wanaotaka kusoma diploma ila marks zao haziruhusu,sasa wangeweka TCU wao hawatumii utaratibu huu katika system maana matokeo yanayohitajika ni ya NECTA O LEVEL NA NECTA ADVANCE,hayo ya mtu kwenda kupigwa kwanza msasa kabla HAWAYATAMBUI,kwa sasa unaweza kusema kuwa wao wanachukua hata wanafunzi wasio na sifa ya moja kwa moja kujiunga chuo,ila wanawadahili baada ya kuwafundisha kozi fupi na kuwapa mtihani na wakifaulu mtihani huo basi wanadahiliwa,
sema haya mambo ya udini ndio yanaharibu na serkali waliwaogopa sijui maana kila siku hawa watu wanalalamikia serikali kuwanyanyasa na waliwaacha huku vyuo vingine wakilazimishwa kuingia TCU.