Pendaelli
JF-Expert Member
- Feb 13, 2014
- 13,075
- 38,625
Wazo lika nijia, kama kipindi kile cha mwalimu nyerere kulianzishwa vijiji na mashamba ya ujamaa kwa nini sasa tushindwe kufanya kwa namna tofauti kidogo
Hii si mfumo wa vijiji vya ujamaa, bali ni pendekezo la kujenga miji mipya ya uzalishaji kwa kutumia miundombinu ya kisasa, ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi, na mipango ya muda mrefu ya maendeleo."
Naomba kujenga hoja yangu hivi
Kusini mwa Tanzania kama lindi, mtwara sehemu ya mkoa wa pwani na sehemu ya mkoa wa Morogoro na mkoa wa ruvuma ni maeneo ambayo unaweza kutenga heka 10,000 zisizo na mgogoro wowote, Serikali ifanye upembuzi yakinifu (feasibility study) ili kubaini eneo lisilo na migogoro ya ardhi, lisilo kwenye hifadhi za misitu au wanyamapori, lenye maji ya kutosha na miundombinu inayoweza kuendelezwa.
Kwa mtazamo wangu, Liwale na Nachingwea ni wilaya ambazo ningeziangalia kwanza katika utafiti, kwa sababu zina ardhi kubwa, shughuli za kilimo na misitu, na msongamano mdogo wa watu. Baadaye ungeunganisha eneo hilo na barabara kuu na Bandari ya Mtwara au Bandari ya Lindi ili bidhaa zisafirishwe kwa urahisi.
Bajeti ya Serikali ya Tanzania ya mwaka wa fedha 2026/2027 ni takribani TSh trilioni 56.49.
Mgawanyo wake kwa ujumla ni huu
Malipo ya mishahara ya watumishi wa umma takribani TSh trilioni 7.2
Malipo ya deni la serikali (riba na marejesho) takribani TSh trilioni 14.3
Matumizi mengine ya kawaida (uendeshaji wa serikali na taasisi zake) takribani TSh trilioni 16.5
Miradi ya maendeleo takribani TSh trilioni 18.5
Hapo kwenye miradi ya maendeleo ikatolewa trilioni kama 3 kwaajili ya mradi huu .
Ndani ya huo mji jumuishi kuwe na vitu vya kuuchochea , kwa mtazamo wangu kukawa na kambi ya jeshi, magereza, shule za msingi na sekondari, vyuo vya ufundi, vyuo vya kati na cha juu.
Eneo la nyumba za ibada, viwanja vya michezo, kumbi , nyumba za makazi za watumishi wa afya, elimu, jeshi magereza polisi na taasisi nyingine za za kiserikali.
Kuwe ma eneo la viwanda vya kuchakata mazoa ya mifugo na kilimo, kuwe na ranchi, kuwe na mashamba ya miti kama mitiki mikaratusi nk , kuwe na mashamba ya mazao kama korosho mahindi mpunga kunde nk kulingana na eneo husika linastawisha mazao ya namna gani.
Kuwe na viwanja vya makazi ya watu huko mbeleni, mabenk, maduka ya ujenzi na bidhaa za chakula nk.
Wakati napata wazo hilo nikajaribu kufuatilia kwenye mitandao kama kuliwahi kufanyika kitu kama hiki kwenye taifa lingie nikagundua nchi kadhaa kama
china wana Shenzhen
Malaysia wana putrajaya
Saud Arabia wana Neom
Nk.
Naomba kumaliza namna hio hoja yangu na mtazamo wangu huu kwa kutumia mfano wa wilaya ya liwale.
Liwale ina sifa nyingi zinazoweza kuifanya iwe eneo zuri la kuanzia.
Ardhi kubwa isiyoendelezwa kikamilifu.
Mvua nzuri kwa kilimo.
Misitu mingi inayoweza kuendelezwa kwa upandaji wa miti ya biashara.
Karibu na Mtwara na Bandari ya Lindi kwa usafirishaji wa bidhaa.
Msongamano mdogo wa watu hivyo upangaji ni rahisi zaidi kuliko maeneo mengi ya Tanzania.
Hatua ya Kwanza (Miaka 1–3)
Serikali itenge takribani ekari 10,000 (au zaidi kulingana na upembuzi yakinifu).
Ijenge:
Barabara za lami.
Maji safi.
Umeme.
Intaneti.
Hospitali ya Wilaya.
Shule za msingi na sekondari.
Chuo cha VETA.
Kituo cha Polisi.
Kambi ya JWTZ.
Magereza.
Mahakama.
Ofisi za Serikali.
Hatua ya Pili (Miaka 3–8)
Kuanzisha uzalishaji mkubwa.
Kilimo, Mahindi, Mpunga, Maharage, Alizeti, Korosho, Ufuta.
Mifugo
Ng'ombe, Mbuzi, Kondoo, Kuku.
Misitu
Mitiki,Mivinje, Mikaratusi.
Viwanda
Kiwanda cha ngozi, Kiwanda cha, mafuta ya alizeti, Kiwanda chakusindika maziwa, Kiwanda cha kusaga nafaka.
Kiwanda cha samani.
Kiwanda cha kuchakata korosho.
Kiwanda cha mbolea (ikiwa gesi ya Kusini itatumika).
Taasisi zitakazoshiriki
JWTZ, Magereza, SIDO, NARCO, TFS, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo, TAMISEMI.
Sekta binafsi.
Makazi, viwanja 1,000 vya mwanzo.
Nyumba za wafanyakazi, Hostel, Soko, Benki, Maduka, Kanisa, Msikiti.
Miaka 10 baadaye
Lengo liwe:
Wakazi 50,000–100,000.
Ajira zaidi ya 20,000.
Mji unaojitegemea.
Kodi nyingi kwa Serikali.
Mauzo ya bidhaa ndani na nje ya nchi.
Miaka 20
Lengo:
Wilaya mpya yenye uchumi mkubwa.
Chuo Kikuu.
Hospitali ya Rufaa.
Uwanja mdogo wa ndege.
Dry Port.
Mji wa kisasa.
Shukurani kwa kusoma mada hii.
Ila nimevutiwa sana na eneo la kusini .
Kila nikiangalia watu hususani vijana walivyo rundikana pale mbagala rangi 3 wakiuza vitu duni sana vya kichina ambavyo ni zaidi ya taka taka na huku serikali haina namna ama haitaki ama haina mpango wa kuwa na kitu kinacho weza kuleta tija si kwa leo bali kesho na kesho kutwa nk.
Baada ya mradi huu kufanikiwa hata kwa kiwango kidogo wangeweza kwenda miji ama mikoamingine kulingana na frusa husika za huko.
Picha ya mwanzo ni kwa msaada wa AI.