Kwa nini serikali haipati wazo la kuanzisha miji mipya ya kimkakati ya maendeleo jumuishi?

Kwa nini serikali haipati wazo la kuanzisha miji mipya ya kimkakati ya maendeleo jumuishi?

Ww mwenyw tukikupa urais hilo wazo hutakua nalo

Kwahyo kula nyama nyamaza ndo kanuni ya mbogamboga
Idea nzuri ila hatuna viongozi wenye maono kama hayo,wengi wao wanachofikiria 2040 huko watoto wao na wenyewe waje kuwa watawala
 
Ni wazo zuri sana lakini nikukumbushe tu wazo kama hili si geni ,kwani case study yake imefanywa kwenye kilimo ( BBT) limeishia kumtajirisha Bashe na viongozi wengine na madudu makubwa yanaendelea tu! Pata muda fuatilia hii miradi ya kilimo, kwahiyo wazo lako ni zuri lakini ni kwa uongozi wenye commitment ya uadilifu na kuwatumikia watu sio huu.

Otherwise utaenda kuwatajirisha watu bila sababu za msingi na matokeo yawe hamna na wananchi kodi zao kupotea.
 
Hapa ndipo serikali inatakiwa kuelekeza kodi zetu. Kuliko kununua magari ya kifahari ya mabilioni kwa ajili ya viongozi wa kiutawala, fedha hizo zikitengwa kwa miaka 5 hadi 10 zinaweza kujenga miji hii ya kanda na kubadilisha kabisa maisha ya vijana wanaotafuta fursa mtaani.
Asante kwa maoni haya , kwa kweli viongozi wetu wanaishi kifahari sana kati kati ya umaskini , sijui kwa nini hawajisikii vibaya kujifaharisha kiasi hiki ikiwa taifa na wananchi wake wako chini mno.
 
Asante kwa maoni haya , kwa kweli viongozi wetu wanaishi kifahari sana kati kati ya umaskini , sijui kwa nini hawajisikii vibaya kujifaharisha kiasi hiki ikiwa taifa na wananchi wake wako chini mno.
Mkuu, hapo umeuliza swali la msingi sana linaloumiza mioyo ya wananchi wengi. Ni picha ya kusikitisha sana kuona kiongozi anapita na msafara wa magari ya kifahari ya mabilioni ya shilingi, huku akiongozana na vumbi na kupita karibu na watoto wanaosoma wakiwa wamekaa chini kwenye madarasa yaliyochakaa, au akina mama wanaokosa huduma za msingi za uzazi hospitalini.

Swali la kwamba 'kwa nini hawajisikii vibaya?' lina majibu makuu matatu ya kimfumo na kisaikolojia:

1. Ugonjwa wa Kisaikolojia wa 'Disconnect' (Mseto wa Tabaka)​

Viongozi wetu wengi, mara wanapoingia madarakani, wanatengenezewa mazingira ya kuishi kwenye 'Bubble' (dunia ya pekee).

  • Matibabu yao yanagharamiwa nje ya nchi au kwenye hospitali binafsi za hadhi ya juu, watoto wao hawasomi shule hizi za kata, na maji na umeme kwenye makazi yao havikatiki kwa sababu kuna majenereta ya nguvu.
  • Kwa sababu hawayagusi wala kuyasikia matatizo ya mwananchi wa kawaida kila siku kwenye maisha yao binafsi, wanapoteza uwezo wa kuguswa kihisia (empathy) na shida za watu wa chini. Maumivu ya wananchi kwao yanakuwa ni takwimu tu za kwenye makaratasi ya bajeti, sio uhalisia wa maisha.

2. Utamaduni wa Kikoloni wa 'Mtemi' (The Legacy of Colonial Administration)​

Mifumo yetu ya kiutawala bado imerithi vinasaba vya kikoloni ambapo kiongozi hakuwekwa ili kuwatumikia watu, bali kuonekana kama 'mungu mtu' au 'mtawala' aliyepo juu ya sheria na jamii.

  • Ndio maana bado tuna utamaduni wa viongozi kupenda kunyenyekewa, kusimamiwa misafara mirefu, na kuonyesha utajiri kama ishara ya nguvu na mamlaka.
  • Katika nchi zilizoendelea na zenye utawala bora (kama nchi za Skandinavia), viongozi kama Mawaziri Makuu huenda kazini kwa baiskeli au usafiri wa umma, kwa sababu jamii yao imejengwa kwenye msingi wa 'Utawala ni Utumishi' na sio 'Utawala ni Ufalme'.

3. Upungufu wa Mifumo ya Uwajibikaji (Weak Oversight)​

Viongozi wanajifaharisha kwa sababu mifumo yetu haiwabani. Kama kodi ya mwananchi ingekuwa na nguvu ya kumuondoa kiongozi madarakani kwa haraka kupitia kura huru au mifumo imara ya uwajibikaji, kiongozi yeyote angeogopa kuonyesha anasa katikati ya umaskini wa wapiga kura wake. Lakini pale wanapojua kuwa uwepo wao madarakani hautegemei ridhaa ya moja kwa moja ya mwananchi bali nguvu ya mfumo uliopo, hawana sababu ya kujali hisia za walipa kodi.

Mwisho wa siku:Ndio maana huwa tunarudi kule kule; ubora wa nchi hauji kwa kuwaombea viongozi wawe na 'huruma', bali unakuja kwa kujenga mifumo thabiti ya kikatiba na kisheria inayowabana. Kiongozi akijua kuwa matumizi ya kifahari ya kodi za wananchi yatamfanya awajibishwe kisheria au apoteze nafasi yake, atanyooka tu bila hata kuhubiriwa. Kama Baba wa Taifa alivyotuonyesha, uongozi ni dhamana ya utumishi, si fursa ya kujitajirisha.
 
Mkuu, naomba nikupongeze kwa dhati kwa kushusha hoja yenye uzito mkubwa, mifano hai ya kihistoria, na takwimu thabiti za Sensa ya 2022 kutoka NBS. Huu ndio mjadala wa kizalendo na kisomi tunaoutaka!

Hoja yako imegusa ukweli mchungu kuhusu saikolojia ya Mtanzania na makosa ya kihistoria yaliyowahi kufanywa. Lakini naomba tuchambue kwa ukaribu tofauti ya kile unachokisema na kile kinachopendekezwa kiuchumi:

1. Somo la Vijiji vya Ujamaa na Ngorongoro (Forced vs. Voluntary)​

Uko sahihi kwa 100%: Mwananchi hawezi kulazimishwa kuishi mahali asipotaka.

  • Mwalimu Nyerere alitumia nguvu (forced relocation) kuwakusanya watu kwenye Vijiji vya Ujamaa, jambo lililoondoa uhuru wa kiuchumi na kuleta dhoruba ya njaa na uzalishaji duni.
  • Mgogoro wa Ngorongoro pia unathibitisha kuwa kutumia amri na sheria kuhamisha watu daima huzalisha migogoro ya kijamii na kiusalama.
Ndio maana Miji Mipya ya Kimkakati haitakiwi kujengwa kwa amri ya serikali wala kuhamisha watu kwa nguvu. Badala yake, inatakiwa kujengwa kwa Vivutio vya Kiuchumi (Economic Incentives). Watu hawahamishwi kwa bunduki au lori; watu wanajihamisha wenyewe kufuata fursa. Ukijenga miundombinu bora, ukatoa nishati ya bei rahisi, na ukaweka viwanda vinavyotoa ajira 50,000 mkoani, vijana kutoka mikoa jirani watahamia hapo wenyewe kwa hiari yao kufuata kipato—kama wanavyofanya sasa hivi wakikimbilia migodi ya Geita au fursa za Dar es Salaam.

2. Takwimu za Sensa 2022 (Watu kuishi kila chocho)​

Ramani uliyoweka ya NBS inaonyesha jambo zuri sana: Mwanza (3.6M), Tabora (3.3M), Morogoro (3.1M), na Geita (2.9M) ina watu wengi sana. Hii inathibitisha kuwa Watanzania wako kila mahali nchini kufuata shughuli za uzalishaji (kilimo na madini).

Lakini swali la msingi ni hili: Je, miji ya mikoa hii inakua kwa mpangilio gani?Tabora, Geita, na Morogoro zinapata ongezeko kubwa la watu lakini kwa sababu hakuna mipango miji ya kisasa inayowahi kabla ya watu kujaa, maeneo haya yanageuka kuwa 'Kariakoo' na 'Mbagala' mpya za baadae—ujenzi wa kiholela usio na miundombinu ya majitaka, barabara za dharura, wala maeneo ya viwanda yaliyotengwa rasmi. Lengo la kuanzisha miji mipya au kanda maalum za kiuchumi (special economic zones) kwenye mikoa hii sio kuwalimbikiza watu kwenye maghorofa, bali ni kupanga ukuaji wa mikoa hii uwe wa kisasa kuanzia hatua za awali kabla uharibifu haujawa mkubwa mno.

3. Saikolojia ya NHC vs. "Chumba Kimoja"​

Mfumo wa NHC wa sasa umeshindwa kuvutia wananchi wengi kwa sababu mbili:

  • Gharama kubwa: Kodi au bei ya kununua apartment za NHC haiendani kabisa na kipato cha Mtanzania wa chini au wa kati.
  • Muundo usioendana na utamaduni yetu: Mtanzania wa kawaida ana extended family, anahitaji nafasi ya kufanya shughuli ndogo ndogo nje, na anathamini umiliki wa ardhi (kiwanja).
Miji mipya ya kimkakati haimaanishi kuwalazimisha watu kuishi kwenye 'apartments' za ghorofani pekee. Ina maana ya kupanga maeneo (master plans) ambapo hata ukitaka kujenga nyumba yako ya chini (single-family home), unajenga kwenye kiwanja kilichopimwa, chenye mfumo wa maji safi na taka, barabara pana inayopitika, na huduma za kijamii karibu.

Hitimisho:Hatutaki kuiga mifumo ya kikomunisti ya kulazimisha watu kuishi pamoja. Tunachotaka ni Serikali kutumia kodi zetu kupanga ardhi yetu vizuri na kuwekeza kwenye miundombinu ya kiuchumi ya mikoani, ili mtawanyiko wa watu ulioonyeshwa kwenye ramani ya NBS uwe mtawanyiko wenye tija, ustaarabu, na unaozalisha utajiri, badala ya kuzalisha mitaa mipya ya mabanda na umaskini nchini kote.
Mkuu umeiweka vizuri sana hoja yako hii, nimesoma mara mbili hakika umechambua vyema sana, ili faa hii ndio iwe uzi wenyewe.
 
Tunashindwa kupanga miji uliyopo ndio tutaweza kujenga miji mipya?
Si vibaya kuanza upya, na kuanza si kwa mtindo ulio zoeleka ila kwa mtindo wa mji wa kimkakati.
Mji utakao zalisha ajira, uchumi na pato la taifa na maendeleo ya moja kwa moja.
 
Si vibaya kuanza upya, na kuanza si kwa mtindo ulio zoeleka ila kwa mtindo wa mji wa kimkakati.
Mji utakao zalisha ajira, uchumi na pato la taifa na maendeleo ya moja kwa moja.
Hii nchi haiwezi
 
View attachment 3628852wazo hili limenijia baada ya safari yangu ya kusini mwa tanzanina kuona uwanda mkubwa usio na makazi ya watu wala hifadhi, ni pori kubwa maelfu ya heka yasio tumika kwa namna yoyote.


Wazo lika nijia, kama kipindi kile cha mwalimu nyerere kulianzishwa vijiji na mashamba ya ujamaa kwa nini sasa tushindwe kufanya kwa namna tofauti kidogo

Hii si mfumo wa vijiji vya ujamaa, bali ni pendekezo la kujenga miji mipya ya uzalishaji kwa kutumia miundombinu ya kisasa, ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi, na mipango ya muda mrefu ya maendeleo."

Naomba kujenga hoja yangu hivi
Kusini mwa Tanzania kama lindi, mtwara sehemu ya mkoa wa pwani na sehemu ya mkoa wa Morogoro na mkoa wa ruvuma ni maeneo ambayo unaweza kutenga heka 10,000 zisizo na mgogoro wowote, Serikali ifanye upembuzi yakinifu (feasibility study) ili kubaini eneo lisilo na migogoro ya ardhi, lisilo kwenye hifadhi za misitu au wanyamapori, lenye maji ya kutosha na miundombinu inayoweza kuendelezwa.


Kwa mtazamo wangu, Liwale na Nachingwea ni wilaya ambazo ningeziangalia kwanza katika utafiti, kwa sababu zina ardhi kubwa, shughuli za kilimo na misitu, na msongamano mdogo wa watu. Baadaye ungeunganisha eneo hilo na barabara kuu na Bandari ya Mtwara au Bandari ya Lindi ili bidhaa zisafirishwe kwa urahisi.

Bajeti ya Serikali ya Tanzania ya mwaka wa fedha 2026/2027 ni takribani TSh trilioni 56.49.

Mgawanyo wake kwa ujumla ni huu

Malipo ya mishahara ya watumishi wa umma takribani TSh trilioni 7.2

Malipo ya deni la serikali (riba na marejesho) takribani TSh trilioni 14.3

Matumizi mengine ya kawaida (uendeshaji wa serikali na taasisi zake) takribani TSh trilioni 16.5

Miradi ya maendeleo takribani TSh trilioni 18.5

Hapo kwenye miradi ya maendeleo ikatolewa trilioni kama 3 kwaajili ya mradi huu .

Ndani ya huo mji jumuishi kuwe na vitu vya kuuchochea , kwa mtazamo wangu kukawa na kambi ya jeshi, magereza, shule za msingi na sekondari, vyuo vya ufundi, vyuo vya kati na cha juu.
Eneo la nyumba za ibada, viwanja vya michezo, kumbi , nyumba za makazi za watumishi wa afya, elimu, jeshi magereza polisi na taasisi nyingine za za kiserikali.

Kuwe ma eneo la viwanda vya kuchakata mazoa ya mifugo na kilimo, kuwe na ranchi, kuwe na mashamba ya miti kama mitiki mikaratusi nk , kuwe na mashamba ya mazao kama korosho mahindi mpunga kunde nk kulingana na eneo husika linastawisha mazao ya namna gani.

Kuwe na viwanja vya makazi ya watu huko mbeleni, mabenk, maduka ya ujenzi na bidhaa za chakula nk.


Wakati napata wazo hilo nikajaribu kufuatilia kwenye mitandao kama kuliwahi kufanyika kitu kama hiki kwenye taifa lingie nikagundua nchi kadhaa kama
china wana Shenzhen
Malaysia wana putrajaya
Saud Arabia wana Neom
Nk.

Naomba kumaliza namna hio hoja yangu na mtazamo wangu huu kwa kutumia mfano wa wilaya ya liwale.

Liwale ina sifa nyingi zinazoweza kuifanya iwe eneo zuri la kuanzia.

Ardhi kubwa isiyoendelezwa kikamilifu.

Mvua nzuri kwa kilimo.

Misitu mingi inayoweza kuendelezwa kwa upandaji wa miti ya biashara.

Karibu na Mtwara na Bandari ya Lindi kwa usafirishaji wa bidhaa.

Msongamano mdogo wa watu hivyo upangaji ni rahisi zaidi kuliko maeneo mengi ya Tanzania.


Hatua ya Kwanza (Miaka 1–3)

Serikali itenge takribani ekari 10,000 (au zaidi kulingana na upembuzi yakinifu).
Ijenge:

Barabara za lami.
Maji safi.
Umeme.
Intaneti.
Hospitali ya Wilaya.
Shule za msingi na sekondari.
Chuo cha VETA.
Kituo cha Polisi.
Kambi ya JWTZ.
Magereza.
Mahakama.
Ofisi za Serikali.


Hatua ya Pili (Miaka 3–8)


Kuanzisha uzalishaji mkubwa.
Kilimo, Mahindi, Mpunga, Maharage, Alizeti, Korosho, Ufuta.


Mifugo
Ng'ombe, Mbuzi, Kondoo, Kuku.

Misitu
Mitiki,Mivinje, Mikaratusi.


Viwanda

Kiwanda cha ngozi, Kiwanda cha, mafuta ya alizeti, Kiwanda chakusindika maziwa, Kiwanda cha kusaga nafaka.
Kiwanda cha samani.
Kiwanda cha kuchakata korosho.
Kiwanda cha mbolea (ikiwa gesi ya Kusini itatumika).


Taasisi zitakazoshiriki
JWTZ, Magereza, SIDO, NARCO, TFS, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo, TAMISEMI.


Sekta binafsi.

Makazi, viwanja 1,000 vya mwanzo.
Nyumba za wafanyakazi, Hostel, Soko, Benki, Maduka, Kanisa, Msikiti.


Miaka 10 baadaye

Lengo liwe:
Wakazi 50,000–100,000.
Ajira zaidi ya 20,000.
Mji unaojitegemea.
Kodi nyingi kwa Serikali.
Mauzo ya bidhaa ndani na nje ya nchi.

Miaka 20

Lengo:
Wilaya mpya yenye uchumi mkubwa.
Chuo Kikuu.
Hospitali ya Rufaa.
Uwanja mdogo wa ndege.
Dry Port.
Mji wa kisasa.


Shukurani kwa kusoma mada hii.

Ila nimevutiwa sana na eneo la kusini .
Kila nikiangalia watu hususani vijana walivyo rundikana pale mbagala rangi 3 wakiuza vitu duni sana vya kichina ambavyo ni zaidi ya taka taka na huku serikali haina namna ama haitaki ama haina mpango wa kuwa na kitu kinacho weza kuleta tija si kwa leo bali kesho na kesho kutwa nk.

Baada ya mradi huu kufanikiwa hata kwa kiwango kidogo wangeweza kwenda miji ama mikoamingine kulingana na frusa husika za huko.


Picha ya mwanzo ni kwa msaada wa AI.
This is great idea, kwanini tusijenge miji yetu kwa mifano hiyo?? Tutakuwa na huduma zote zinazotakiwa, hii itasaidia kuondosha watu kukimbilia Dar es Salaam tu. Pia ingewezekana kwenye miji mikubwa, huduma za ofisi ziwekwe nje ya miji ili kupunguza misongamano kwenda katikati ya miji hiyo. Itasaidia sana.
 
This is great idea, kwanini tusijenge miji yetu kwa mifano hiyo?? Tutakuwa na huduma zote zinazotakiwa, hii itasaidia kuondosha watu kukimbilia Dar es Salaam tu. Pia ingewezekana kwenye miji mikubwa, huduma za ofisi ziwekwe nje ya miji ili kupunguza misongamano kwenda katikati ya miji hiyo. Itasaidia sana.
Itasaidia sana kuliko tunavyo weza kueleza, ukiangalia vile nguvu kazi inapotelea pale dar es laam , kuke Mbagala temeke gongo la Mboto kariakoo nk , huwa naumia sana.
Ila serikali inaona kawaida tu
 
Back
Top Bottom