Shule zetu zinafungwa na kufunguliwa siku moja nchi nzima. Inawezekana wazo hili lina nia njema na manufaa.
Hata hivyo, naona utaratibu huu una changamoto ambazo zina athari kubwa mno kwa wanafunzi na wazazi.
Baadhi yake ni changamoto ya usafiri, malazi na chakula safarini. Vyombo vya usafiri vinashindwa kumudu kubeba abiria wote kutokana na wingi wao unaotokana na ongezeko la abiria wanafunzi. Tatizo hili ni kwenye mabasi, pikipiki, bajaji, meli na gari la moshi (treni).
Sijui hali ikoje huko angani. Fikiria shule za Mwanza na Mara zenye wanafunzi wanaokwenda Kagera kwa kutumia Meli. Itawamudu? Fikiria wanafunzi wanaotoka Dar kwenda Bara. Mabasi na treni vinawamudu?
Wingi huo unalemea pia hoteli na migahawa wanakohitaji chakula. Pia ndivyo inavyokuwa kwenye nyumba za kulala wageni.
Natamani kufahamu manufaa makubwa yanayopatikana kwa kufunga na kufungua shule siku moja kwa nchi nzima.
Vile vile, kuna faida gani kuwa na sare moja nchi nzima?