Kichwa cha habari hapo juu chajieleza!
Nimefanya utafiti usio rasmi, kwa sasa asilimia kubwa ya wazazi (karibu wote) wanatamani, au wanataka watoto wao wakasome shule za English Medium.
Asilimia kubwa (karibu wote) wazazi wenye kipato wamepeleka watoto wao English Medium. Sijajua kama kuna mtoto hata mmoja wa mtunga sera za elimu anasoma shule za msingi za serikali.
Ukikutana na mzazj hohehahe anayesomesha shule za msingi za serikali anatamani mtoto wake na yeye angekuwa anasoma English Medium, akipata hela lazima atampeleka huko!
Kinachowavutia zaidi wanajamii ni pale wanapokutana na mtoto wa English Medium akiongea Kingereza.
Sasa, kwa nini shule za msingi zote za serikali zisianze kufundisha kwa mtaala wa Kingereza? Kwa sababu naona wazazi hawazielewi kabisa shule za msingi za serikali zinazofundisha kwa Kiswahili.
Sidhani hata watoto wa wafanyakazi wa BAKITA (Baraza la Kiswahili Tanzania) wanasoma shule za msingi za serikali.