Wakubwa hawataki nchi itembee mwendo wa haraka katika kuleta maendeleo ya mtu wa kawaida.
Kubadili jambo hili inawezekana,yaani hii siri wanabaki nayo wenyewe.
Kama unataka kujua ,wanyonge wanaingizwa chaka,ni kiongozi gani ambaye mtoto wake hasomi shule za "english medium",jibu ni hakuna.
Na ndio maana shule za kawaida hakuna anayeleta ufumbuzi endelevu wa kutatua tatizo la upungufu wa madarasa na madawati, wanaishia kutoa matamko kila mwaka:"ole wake ambaye shule yake watoto watakaa chini","watumishi hakuna kwenda likizo mpaka tatizo la upungufu wa madawati na madarasa liishe"
"Utafikiri,tatizo la upungufu madawati na madarasa ni dharura,wakati kuna taasisi za takwimu,kuna makadirio ya ongezeko la vizazi na vifo kila mwaka!