Kwa nini simu ya mume iogopwe kama ukoma?

Kwa nini simu ya mume iogopwe kama ukoma?

nani kakuambia siwaaheshimu wanawake, au heshima gni uayozungumsia?

mi nazungumza fact. dunia ndiyo ilivyo msipotia akili kichwani, mtang'ang'ana na kupekua simu za wenzi wenu weeeeeeeeeee kumbe mambo iko kwingine na inaendelea................tena inaendelea sawa kabisa........

tena we DC unaweza kukuta mke wako anajifanya kukuamini kwa kuwa anapekua simu yako apendavyo kumbe mambo yoooote haitumii simu!!!!!!! yuko na ntu isiyo na simu..................inatuma nt0to ianaleta kanoti au anamsubiri njiani........!!!!!! kalaghabaho!!!

AK, usichukulie mambo personal. Kinachoendelea hapa ni mjadala wa kubadilishana mawazo. Na msingi wa majadiliano tunayofanya ni uzoefu wetu. Kama wewe unaongelea nadharia basi uko kwenye wrong thread. Tueleze unayamudu vipi mahusiano yako badala ya kuleta wish list. Kila mtu alikuwa na wish lists zake, lakini hapa tunaongelea yale tunayoyatenda kila siku. Halafu simu siyo kipimo cha uaminifu hata kidogo. Pia kuna wengine wamechanganya. Access to your partner's phone is not the same as mandatory inspection/search. We are talking about free access to phone, e-mail etc. Don't mix real life and theories. Those are two different worlds!
 
@Dark city nafikiri msg sent..mi mwenyewe nilitamani kuacha kuandika niongee..mana tumegusa maeneo ambayo kweli yana mengi ya kuongea..tumejaribu kusimamia tulichokua tunaongea badala ya kutoka nje ya mada kama wengine ambvyo wamekuwa wakifanya!! ndo mana napenda signature moja humu ya bht kama sikosei...Trust everyone until they give u a reason not to trust!... Mie naheshimu na kutrust kila mtu achilia mbali mume wangu! And iam sure is the same to most of the other ladies..the moment tunapewa a reason not to trust kila mtu ana mipaka yake kuhusu action atayochukua!?..otherwise ciao guys...!
 
Mwenye mada . Hongera sana kwa kuwa na mke mwminifu. Inawezekana ukawa the only person.Hata hivyo umeshawahi kupekuwa hivyo vipima joto vyao ukakosa cm nyingine au chip za mitandao yote wakati wewe unajua moja tu?

Ninavyofahamu mimi, anazo simu 2 tu. Kama anazo nyingine basi zimefichwa mbali kwa hiyo siwezi kuzipata. Lakini kama anaficha kiasi hicho ni poa tu kwani siyo sawa na kuwekewa embargo ya kugusa simu yake. Pochi zake naweza kuzifungua wakati wowote na kuchukua kitu chochote na hajawahi kunizuia nisiguse. Kwa hiyo kama kuna sababu ya msingi nafungua tu kipima joto cha wife wangu.

Umesema ana tabia ya kufuta msg na calls made. Kwa hiyo hadi hapo huoni hataki ujue mambo yake ? Kukupa wewe cm yake inaweza ikawa pretence tu ili wewe umpe ya kwako akucontrol anavyotaka . Yaani , tuseme wewe humwachia msg zako zote anajisomea tu anavyotaka ? You must be very very extraordinarly exceptional MAN in that case.

Pamoja na kuwa wife alikuwa na tabia ya kufuta messeges and calls, hilo tumeshaliongea na siyo tatizo tena. Inawezekana hataki mimi nione mambo yake lakini sababu yake ni kuwa hapendi simu ijae sms na calls za nyuma. Hata pale ninapozikuta, sijawahi kuona sms au call ambayo inatia shaka!

Wala hamna binadamu asiyependa privacy. Kwa hiyo ana njia zake za kufanya mambo yake privately na hicho kinokia chake unachoaccess ni toi tu bro. The bottom line is ' Your palm phone is yours and not mine' even if it was in the honey moon. Period.

Simaanishi kwamba wife au mimi hatuna mambo ambayo ni private na tusingependa kuelezana. Yapo mengi tu. Kwa mfano, baadhi ya mambo ya nyumbani kwetu sipendi ayajue. Kwa hiyo inapotokea kuna sms ambayo sipendi aione naisoma na kuifuta mara moja.
 
Ni aje pale Mume au Mke ana simu mbili na moja anaificha bila mwenzie kujua kama mkewe/mumewe ana simu ya ziada!? Kwa maoni yangu kuwa na huru na simu ya mke au mume 24/7 haimaanishi kwamba mume/mke huyo hana shughuli za ziada nje ya ndoa yake. Binadamu ni wajanja sana katika kuruka viunzi kama wanataka kufanya lolote lile na siku hizi msisahau pia watu wanaweza kuwasiliana kwa namna nyingi tu ukiondoa hizo simu za mkono.

Njemba mmoja hivi karibuni alimuomba mkewe passwords za email addresses zake zote ambazo mume anazifahamu. Mke akakataa kata kata, basi akapata kipigo cha hali ya juu lakini hakutoa password hata moja. Bado wako pamoja sijui kama mume kanyoosha mikono juu au kipigo kitakuwa kinarudia rudia mpaka kieleweke.

Ukiwamo kwenye ndoa basi unachotakiwa kufanya ni kumuamini mkeo/mumeo, vinginevyo ukitaka kumpekuapekua kila siku iendayo kwa Mungu basi hukawii kukutana na ambayo hukuyatarajia.
 
BAK,

Sidhani kama kuna mtu anafagilia kupekuana. Ila mimi na baadhi ya watu tunashauri kutokuwepo vizuizi katika vitu tunavyomiliki. Hii ni pamoja na emails, wallets, vipima joto, bank accounts n.k. Kwa nini mtu ufanye naye kila kitu lakini umfiche vitu kama hivyo endapo huna agenda ya siri?
 
Mmh yaletale tu...kwanini asifute call record zake kwani wewe zinakuhusu nini?
 
Mmh yaletale tu...kwanini asifute call record zake kwani wewe zinakuhusu nini?

Nadhani hilo ndilo suala la muhimu. Kama mtu anaamua ku-cheat basi afanye hivyo responsively na siyo kutumia mabavu. Afiche kila kitu kinachohusu huo uchafu wake na asijifanye kutumia maguvu kwa mwenzake.
 
Unamaanisha shemeji kilonga longa chako huwa hagusi kabisa?

Kama hayo ni ya kweli basi tumpe pole dada yetu!! Ila itakuwa vizuri akimwomba amfiche kila kitu, hata ikibidi taa za chumbani ziondolewe ili giza litawale kila uwanja!!🙄🙄🙄
 
my wife wangu hutamba na simu yangu kwa kadrii apendavyo...!!!
simzuii kugusa simu yangu nami ninapokuwa na shida na simu humuomba ya kwake ili niitumie
wakati mwingine tumejikuta mmoja wetu akijisahau na kuondoka nasimu ya mwenzake kwenda kazini kwani simu zetu zinafanana na hakunashida yoyote iliyowahi kutokea...!!!

cha muhimu ni uaminifu kwa kila mmoja wenu...!!!
 
Safii sana ndugu yangu. Katika mazingira kama hayo ulishakutana na masahibu ya kumpanda mwanamke au msichana wa nje? Kama ndiyo, ulifanyaje kutunza siri?
 
Ahsnte sana dadangu. Kwanza nilihisi woga kidogo kwa kudhani kuwa labda sisi tuko peke yetu (mimi na wife wangu) na pia tuko miaka ile ya 47, kwa kuwa hatupeani privacy kwenye simu. Nimefurahi sana kwamba na wewe ni mdau wa "free trade zone", kwenye haya mambo ya mahusiano. Na ni kweli, naogopa zaidi mke wangu kumaliza pesa zangu kwenye simu kuliko kuona siri zangu kwani sina siri yoyote ya kuficha. Nawaomba wanawake waache upuuzi wa kuwavimbisha vichwa waume zao. Ni afadhali tuwe na couples 2 au 3 zinazoishi kwa amani kuliko kuwa na 100 zinazoishi kwenye tanuru la moto. Huwa natamani ningeweza kuwaoa dada zangu ili wasipate taabu. Unfortunately haiwezekani. Hata hivyo inaniuma kuona wanadhalilishwa na hao insecure men kwa kisingizio cha kulinda ndoa!

Nisaidie ndoa yako ina umri gani? samahani sikuingilii kwenye home affairs zako, nataka nipate pa kuanzia
 
Nisaidie ndoa yako ina umri gani? samahani sikuingilii kwenye home affairs zako, nataka nipate pa kuanzia

Relationship yetu ina miaka 11 na ndoa ina miaka 9. Na katika hicho kipindi chote sijawahi kuhisi kuwa my wife anacheat, na mimi pia sijawahi ku-cheat. Ila kuteswa na tamaa kupo pale pale na wakati mwingine tunajadiliana/ kusimuliana. Hard to believe?
 
...kama nayeye ana msimamo huo hongereni sana bro.
 
...kama nayeye ana msimamo huo hongereni sana bro.

Hiyo ndiyo kanuni yetu ya imani. Mimi naiamini hiyo kanuni na sina shaka kwamba yeye haamini pia. Labda nikipata sababu ya kunishawishi vinginevyo. "Kwa sasa mambo ni mswano".
 
Hiyo ndiyo kanuni yetu ya imani. Mimi na aiamini hiyo kanuni na sina shaka kwamba yeye haamini pia. Labda nikipata sababu ya kunishawishi vinginevyo. "Kwa sasa mambo ni mswano".

...baada ya miaka 11 sababu za nini tena kaka? bahati ya mtende hiyo, kila la kheri.
 
Simu ni vitu binafsi jamani, sina time na simu ya mamsapu nategemea nayeye pia! mambo ya kuumizana roho ya nini?
 
Simu ni vitu binafsi jamani, sina time na simu ya mamsapu nategemea nayeye pia! mambo ya kuumizana roho ya nini?

Mkuu kuwa na time ni kitu kimoja na kuweka embargo ni kitu kingine. Sasa wewe unatumia ipi? Ya kuweka vikwazo kwamba akigusa tu unamshusha meno yote 32 kwa kumtandika kichwa kama kondoo?
 
Mkuu kuwa na time ni kitu kimoja na kuweka embargo ni kitu kingine. Sasa wewe unatumia ipi? Ya kuweka vikwazo kwamba akigusa tu unamshusha meno yote 32 kwa kumtandika kichwa kama kondoo?

Watu walikuwa wanacheat ndani ya ndoa zao kabla ya simu za mkono kuwepo na wataendelea kufanya hivyo hata kama mume au mke anakaa na simu ya mkewe 24/7. Kuwa na access na simu ya mkeo au mumeo saa yoyote unayotaka ili uipekuepekue simu na txt messages zilizoingia na kutoka haina maana kwamba huyo mwenzio hatoki nje ya ndoa hata kama hutaona lolote katika simu hiyo. Njemba aliyempiga mkewe kwa kukataa kumpa passwords za email addresses kwanza alianza kuichukua simu ya mkewe na kukaa nayo kwa masaa mengi tu lakini hakuambulia kitu ndipo alipoamua kuomba passwords za hizo addresses na mama kukataa katakata.

Kikubwa ni kuaminiana tu ukitaka kujipiga kifua eti nina access ya simu ya mke/mume wangu 24/7 hivyo hakufichi chochote na hatembei nje, basi unajidanganya sana.

Kuna mama mmoja hapa aliandika kwamba mumewe alikataa kata kata kwamba asiwe na simu ya mkono maana zinaongeza uwezekano wa kutembea nje ya ndoa. Mama huyo aliandika kwamba alinunua simu ya mkono bila kumtaarifu mumewe na huificha anakokua mwenyewe na mume hajaigundua kwa miaka sasa.
 
.....Kikubwa hapa ni kuaminiana, lakini mhhhh hata mimi nina tabia ya kupekua simu ya Mr.
 
Back
Top Bottom