SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Mtanisamehe kwa makala ndefu ila hili inabidi leo tuliongelee.
Mimi ni mmoja wa watu ambao kuna kipindi nilikuwa nashangaa nikikuta mwanaume ana jina la kike. Kyrie, Shannon, Courtney, Lindsay, Klay yote ni majina yalikuwa yananishangaza kukuta amepewa mwanaume. Nikaja kukutana na Joyce ndiyo nikashtuka kabisa.
Baada ya kuelewa kuwa kwanza kuna issue ya tofauti za tamaduni, hauwezi ukalazimisha mambo kwa wengine kisa kwako haujayazoea kuyaona. Pili nadhani ni trend ya uwepo wa single mothers ambao wamejipa au wamelazimika kuwapa majina watoto wao, jukumu ambalo kihistoria lilibebwa na mwanaume. Sidhani kama kuna mwanaume atamuita mtoto wake wa kiume jina ambalo kimazoea ni la kike.
Alipotambulishwa mchezaji wa Simba anayeitwa Debora Fernandez Mavambo, maneno na kejeli yamekuwa mengi sana. Juzi nilikuwa naangalia mpira banda umiza, nikasikia watu wanasema wao ni wanaume wanacheza na mademu, mwingine anasema Debora ana mimba (sijawahi kuelewa kejeli za mimba, njia ambayo wote tumetokea ila hilo tuliache kwanza). Huwa najiuliza hawa wanaotania si walikuwa na Joyce Lomalisa (siyo jina moja la kike, bali mawili) kwa misimu kadhaa, mbona wanakuwa wasahaulifu?
Kuna kipindi Mzamiru alibadili jina katika jezi yake akaweka jina la Mama yake. Bernard Morrison naye alibadili jina katika jezi yake akaweka la Bibi yake. Mbona watu waliheshimu maamuzi yao na sikumbuki kuona wanakejeliwa?
Nimalizie kwa kuuliza, hivi kuitwa jina la kike kunampunguzia nini mwanaume kuwa mwanaume kamili? Baadhi ya hawa wanaume wenye majina ya kike wana nguvu ikiwemo za kiume kukushinda wewe, sasa unajisifu nini? Wewe unaweza kupambana uwanjani na kina Pacome, Aziz Ki na Aucho kwa lisaa lizima?
Kuna jambo nilijifunza kuhusu majina. Haijalishi una jina gani, suala ni umefanikiwa katika nini katika haya maisha? Kuna mkuu mmoja ni daktari bingwa, angekuwa mtu wa kawaida angepata tabu sana na jina lake. Kina Arnord Schwarzenegger, watu hawapati shida kutamka wala kuandika majina yao kwa sababu wamefanya kitu hapa duniani. Wewe mwenye jina perfect una nini cha kujivunia? Nani anakujua?
Nahisi kuna kaushamba fulani inabidi tukaache.