Kwa nini tukikutana na mwanaume ana jina la kike unakuwa mjadala wa kitaifa?

ilianza kwa watu simba kuwasema yanga kuhusu jina la joyce lomalisa, nadhani ni mazoea tu yaliyochanganyika na utani wa jadi.

mkuki kwa nguruwe eh, joyce mlimuanzishia mpaka thread hapa, mkasema haitwi lomalisa bali anaitwa joyce lomalisa mutambala, nami nasema haitwi debora anaitwa debrah.
Hiyo ya Joyce ingekuwa sababu tosha ya watu wa Yanga kutoikejeli Simba kwa sababu ya Debora kwa sababu kwanza Joyce alionyesha vitendo uwanjani vilivyozima kejeli zote ikatoa fundisho kwa wote.

Hata ule mshuti wa Debora kwenye Simba Day ulishaanza kufifisha kejeli zake.
 
tatizo lako ushabiki maandaz umekupofusha macho na umekufanya umekuwa mnafiki kuliko mwanamke wa kiswahili, hata andiko lako limejaa unafiki mtupu.
 
Mtanisamehe kwa makala ndefu ila hili inabidi leo tuliongelee.

Mimi ni mmoja wa watu ambao kuna kipindi nilikuwa nashangaa nikikuta mwanaume ana jina la kike. Kyrie, Shannon, Courtney, Lindsay, Klay yote ni majina yalikuwa yananishangaza kukuta amepewa mwanaume. Nikaja kukutana na Joyce ndiyo nikashtuka kabisa.

Baada ya kuelewa kuwa kwanza kuna issue ya tofauti za tamaduni, hauwezi ukalazimisha mambo kwa wengine kisa kwako haujayazoea kuyaona. Pili nadhani ni trend ya uwepo wa single mothers ambao wamejipa au wamelazimika kuwapa majina watoto wao, jukumu ambalo kihistoria lilibebwa na mwanaume. Sidhani kama kuna mwanaume atamuita mtoto wake wa kiume jina ambalo kimazoea ni la kike.

Alipotambulishwa mchezaji wa Simba anayeitwa Debora Fernandez Mavambo, maneno na kejeli yamekuwa mengi sana. Juzi nilikuwa naangalia mpira banda umiza, nikasikia watu wanasema wao ni wanaume wanacheza na mademu, mwingine anasema Debora ana mimba (sijawahi kuelewa kejeli za mimba, njia ambayo wote tumetokea ila hilo tuliache kwanza). Huwa najiuliza hawa wanaotania si walikuwa na Joyce Lomalisa (siyo jina moja la kike, bali mawili) kwa misimu kadhaa, mbona wanakuwa wasahaulifu?

Kuna kipindi Mzamiru alibadili jina katika jezi yake akaweka jina la Mama yake. Bernard Morrison naye alibadili jina katika jezi yake akaweka la Bibi yake. Mbona watu waliheshimu maamuzi yao na sikumbuki kuona wanakejeliwa?

Nimalizie kwa kuuliza, hivi kuitwa jina la kike kunampunguzia nini mwanaume kuwa mwanaume kamili? Baadhi ya hawa wanaume wenye majina ya kike wana nguvu ikiwemo za kiume kukushinda wewe, sasa unajisifu nini? Wewe unaweza kupambana uwanjani na kina Pacome, Aziz Ki na Aucho kwa lisaa lizima?

Kuna jambo nilijifunza kuhusu majina. Haijalishi una jina gani, suala ni umefanikiwa katika nini katika haya maisha? Kuna mkuu mmoja ni daktari bingwa, angekuwa mtu wa kawaida angepata tabu sana na jina lake. Kina Arnord Schwarzenegger, watu hawapati shida kutamka wala kuandika majina yao kwa sababu wamefanya kitu hapa duniani. Wewe mwenye jina perfect una nini cha kujivunia? Nani anakujua?

Nahisi kuna kaushamba fulani inabidi tukaache.
Mwanao wa kiume muite Hadija kama ni vizuri
 
Hiyo ya Joyce ingekuwa sababu tosha ya watu wa Yanga kutoikejeli Simba kwa sababu ya Debora kwa sababu kwanza Joyce alionyesha vitendo uwanjani vilivyozima kejeli zote ika

Hata ule mshuti wa Debora kwenye Simba Day ulishaanza kufifisha kejeli zake.
hata onana alifunga bonge ya goli kwenye simba day, kilichofuata baada ya hapo hata wewe unakijua.

na mshuti umefifishaje kejel wakt wewe ndo umekuja na uzi kuwa debrah mechi na yanga alikuwa anakejeliwa ana mimba.
 
Sijaelewa Onana anaingiaje kwenye mada hii. Hiyo ya mimba sikuisikia kwenye derby, ni kabla.
 
wao ni wanaume wanacheza na wanawake, mashabiki wa apr ndo walikuwa wanasema hvo siyo?

huwa najiuliza mbona nao walikuwa na joyce, joyce alikuwa mchezaji wa zile timu za misri mlizocheza nazo siyo?

watu wote sio viazi kama wewe mkuu.
 
Ni wanaume wachache wenye akili ndo huwezi kuwawasikia wakikejeli mimba tena kwa mwanaume mwenzao.....
Ni vijanaume uchwara vinaishi maisha ya kuunga unga ndo wanafanya hivi...
 
wao ni wanaume wanacheza na wanawake, mashabiki wa apr ndo walikuwa wanasema hvo siyo?

huwa najiuliza mbona nao walikuwa na joyce, joyce alikuwa mchezaji wa zile timu za misri mlizocheza nazo siyo?

watu wote sio viazi kama wewe mkuu.
Ongea ueleweke. Naona unabwabwaja tu sijui hata unazungumza nini
 
Hiyo ya Joyce ingekuwa sababu tosha ya watu wa Yanga kutoikejeli Simba kwa sababu ya Debora kwa sababu kwanza Joyce alionyesha vitendo uwanjani vilivyozima kejeli zote ikatoa fundisho kwa wote.

Hata ule mshuti wa Debora kwenye Simba Day ulishaanza kufifisha kejeli zake.
kwa simba na yanga haya ni ya kawaida kama utakumbuka kejeli kwa kikuku cha shishimbi.
 
Somalia nilisikia mtt wakiumee akiitwa faudhia...alafu fresh tu
Huku kwetu mtu huyo tunamuita Faudh. Hata hivyo ni ushamba tu jina ambalo si la kabila lako kulicheka kuwa ni la kike au kiume. Mbona wenyewe poa kuwaita mbwa wao John, Salome, Omar nk. Itoshe kusema jina kama si la kabila lako au kiswahili kuli-judge
 
Mtanisamehe kwa makala ndefu ila hili inabidi leo tuliongelee.

Mimi ni mmoja wa watu ambao kuna kipindi nilikuwa nashangaa nikikuta mwanaume ana jina la kike. Kyrie, Shannon, Courtney, Lindsay, Klay yote ni majina yalikuwa yananishangaza kukuta amepewa mwanaume. Nikaja kukutana na Joyce ndiyo nikashtuka kabisa.

Baada ya kuelewa kuwa kwanza kuna issue ya tofauti za tamaduni, hauwezi ukalazimisha mambo kwa wengine kisa kwako haujayazoea kuyaona. Pili nadhani ni trend ya uwepo wa single mothers ambao wamejipa au wamelazimika kuwapa majina watoto wao, jukumu ambalo kihistoria lilibebwa na mwanaume. Sidhani kama kuna mwanaume atamuita mtoto wake wa kiume jina ambalo kimazoea ni la kike.

Alipotambulishwa mchezaji wa Simba anayeitwa Debora Fernandez Mavambo, maneno na kejeli yamekuwa mengi sana. Juzi nilikuwa naangalia mpira banda umiza, nikasikia watu wanasema wao ni wanaume wanacheza na mademu, mwingine anasema Debora ana mimba (sijawahi kuelewa kejeli za mimba, njia ambayo wote tumetokea ila hilo tuliache kwanza). Huwa najiuliza hawa wanaotania si walikuwa na Joyce Lomalisa (siyo jina moja la kike, bali mawili) kwa misimu kadhaa, mbona wanakuwa wasahaulifu?

Kuna kipindi Mzamiru alibadili jina katika jezi yake akaweka jina la Mama yake. Bernard Morrison naye alibadili jina katika jezi yake akaweka la Bibi yake. Mbona watu waliheshimu maamuzi yao na sikumbuki kuona wanakejeliwa?

Nimalizie kwa kuuliza, hivi kuitwa jina la kike kunampunguzia nini mwanaume kuwa mwanaume kamili? Baadhi ya hawa wanaume wenye majina ya kike wana nguvu ikiwemo za kiume kukushinda wewe, sasa unajisifu nini? Wewe unaweza kupambana uwanjani na kina Pacome, Aziz Ki na Aucho kwa lisaa lizima?

Kuna jambo nilijifunza kuhusu majina. Haijalishi una jina gani, suala ni umefanikiwa katika nini katika haya maisha? Kuna mkuu mmoja ni daktari bingwa, angekuwa mtu wa kawaida angepata tabu sana na jina lake. Kina Arnord Schwarzenegger, watu hawapati shida kutamka wala kuandika majina yao kwa sababu wamefanya kitu hapa duniani. Wewe mwenye jina perfect una nini cha kujivunia? Nani anakujua?

Nahisi kuna kaushamba fulani inabidi tukaache.
Kumbe inauma eh? Karma is a bitch!
 
Wale waliokuwa wanamdhihaki Debora Fernandez wanaendeleaje huko kiumeni?
 
Back
Top Bottom