Kwa nini tuwaombee waliokufa?

Kwa nini tuwaombee waliokufa?

Is it serious au joke?

Hivi nyinyi muambiweje mjue kuwa vitabu hivyo viliondolewa na Martin Luther...? Na baada ya kuviondoa aliviwekka kama Index mpaka alipokuja kuviondoa moja kwa moja...

Kwataarifa yako hakuondoa vitabu hivyo tuu pia alitaka kuondoa kitabu cha Yakobo na Ufunuo...Tumshukuru Mungu Reformer mwenzake Calvin alimkataza...

Ngoja nikuulize...Hivi kama angefanikiwa kuviondoa vitabu vya Yakobo na Ufunuo na leo mngekuja kulalalma...?
 
Mkuu hebu nieleze ni kwanini Martin Luther wakati anaondoa vitabu 7 avya Aggano la kale alitaka kuondoa kitabu cha Yakobo na Ufunuo......Hivi kama angefanikiwa kuviondoa vitabu vya Ufunuo na Yakobo leo ungekuja kusema vilikuwa havina uvuvio wa Roho Mtakatifu...????

Naomba pia nikusahihishe...Kanisa Katoliki halijawahi punguza wala kuongeza kitabu chochote katika Biblia....Oroginally Biblia ilikuwa na vitabu 73..

Kama unataka nikupe Historia ya Bbilia nitakupa...Mzozo kwanza hakuanzia kwa Martin Luther, ila ulianzia Karne za mwanzoni baada ya kufa kwa Yesu.....Vitabu hivyo viliachwa na Waisraeli kutokana na mapokeo yake yalikuwa katika Lugha ya Kigiriki....

Pole sana....rudi usome upya historia ya kanisa na tafuta kuhusu mkutano wa Nicea (425 AD kama sijakosea) enzi za Constantine (aliyeanzisha rosali ndani ya kanisa), ndipo utajua nani aliviondoa na ujue kuwa wakati huo kanisa lilikuwa moja tu. Wa kwanza kujitoa alikuwa Martin Luther (miaka ya 1500) kwa hiyo kusema si kanisa katoliki waliotoa nakusamehe bure, pengine hujui, make a research. Mkutano wa Nicea ndiyo uliweka msingi mkubwa wa imani ya ukristo kikanisa-katoliki ikiwa hujui (mwulize padri au mjuzi wa historia ya kanisa katoloki atakuthibitishia hili)

KITABU cha Yakobo kinahusu Neema....Mwanzoni Martin Luther hakuwa na uelewa kuhusu neema. Na ukisoma nyaraka (thesis) zake za baadaye anakiri kuwa alitaka kufanya kosa kubwa kwa sababu ya kutomwacha Roho Mtakatiifu kumfundisha hapo mwanzo kwa kukipuuzia kitabu hiki na katika vitu ambavyo anakiri kuwa mwanzoni vilimtatizo ni neema na hakutaka kuondoa kitabu hicho tu hata kitabu cha Warumi na vingine vinavyosisitiza neema/grace. Na mwishowe anakiri kuwa Kitabu cha Yakobo ni mojawapo ya backborne za NT kwa sababu kila mtu anaokolewa kwa neema. (SIYO MAOMBI YA WAFU KAMA ULIVYOAMINISHWA NA WAPAGANI WALIOLITEKA KANISA). SO is Ufunuo, mwanzoni Luther hakuwa na ufahamu kuhusu Eschatology na hiyo mpaka sasa mapadre wengi hawana ufahamu wa kutosha kuhusu eschatology hata sasa.

Usijaribu kuleta mjadala tuanze kujadiliana "if"

Na elewa kuwa huu mjadala si vita ya kidini.

Hivyo vitabu vya deutrocanony ulishavisoma? vitafute uvisome kwanza ndipo utajua ni kwa nini viliondolewa na ni kwa vipi vinaweza kummislead mtu asipokuwa mwangalifu. Ni vitabu vya historia tu za vita na mapinduzi (coup) vya Israeli na watawala katika kipindi cha miaka 453 kati ya kitabu cha Malaki mpaka kuzaliwa Kristo (Mathew). Hata katika tanack havimo. vipo katika nyaraka za historia ya waisraeli kama vitabu vya Yosephas/josefus...na wengine.
 
chief...kimsingi ukishakufa you olny face the creator, God's court ni court pekee ambayo wewe mwenyewe ni shahidi na prosecutor-your deeds.

Na hii kitu ya kuombea wafu kama nilivyosema ni mojawapo ya sababu za kuparaganyika kanisa katoliki wakati wa Martin Luther.

Jambo lisilo kwenye Maandiko na haliwezi kuthibitishwa ni ushirikina. Hata kama anayelihubiri au kulitenda amevaa joho au kanzu iliyopambwa kwa dhahabu au almasi.
Mkuu kama kuna hukumu(God court) siku ya Mwisho: inamaana wako watakaoshinda kesi na wale watakaopaikana na hatia.? unaionaje hii?
Tuanze kujadili

Je kuna dhambi ya Ndogo na dhambi Kubwa. JE nini maan ya dhambi ya MAuti? Kwanini kuwe na dhambi ndogo na dhambi kubwa?
 
Hizo ni Ibada za Matambiko, wanaposema wanaenda kuwaombea marehemu basi ujue wao ndo wanapeleka hoja kwa marehemu ili wasafishiwe mambo yao.

Ni inahusu na Ibada za Mizimu, ni somo pana sana kuhusu Mizimu, hii huwa inaabudiwa kizazi hadi kizazi. Mungu alieumba Mbingu na Nchi kamwe hasikilizi maombi ya Wafu na kupitia Biblia Mungu hajaruhusu maombi ya Wafu.

Mbona huyo Mungu wenu mnayemuabudu kila siku kashindwa kutatua matatizo kibao ya dunia hii anayoadiwa kuiumba? Na kila siku mnajazana makanisani, misikitini na mahekaluni?
 
Mkuu hii habarinya kuwaombea wafu ni Madhehebu ya Kiprotestant tuu ambayo hayaamni...Ila Early Chruch zote zinaamni...Kuaanzia Catholic, Orthodox, Anglican High Church, Coptic, Armenian Catholic na mengine mengi....

Unaposema kanisa la awali ni kanisa la mitume na si hayo makanisa km ulivyoyataja.... Sasa swali ni kwamba Hao mitume waliamini ktk kuwaombea wafu? Kwanini hatuoni mfano wa mitume kuwaombea ata mmoja wa mitume mwenzao aliyetangulia kufa???
 
Mkuu kama kuna hukumu(God court) siku ya Mwisho: inamaana wako watakaoshinda kesi na wale watakaopaikana na hatia.? unaionaje hii?
Tuanze kujadili
Je kuna dhambi ya Ndogo na dhambi Kubwa. JE nini maan ya dhambi ya MAuti? Kwanini kuwe na dhambi ndogo na dhambi kubwa?

heheheheh....court ya Mungu ni matendo sijui na sidhani kama kuna mjadala. Kama Biblia inavyosema matendo yanakutangulia nadhani yanatangulia as evedence against au on behalf to pleed for you. Na hivyo ukishafika matendo yanakuwa yameshamaliza mambo. Na sehemu nyingine Biblia inasema, kila kazi ya mtu (matendo) itapimwa kwa moto, ikiungua ujue umekwenda.
 
Martin Luther and the 95 Theses - Facts & Summary - HISTORY.com
Pia kuna madai kama ilivyokuwa mwanzilishi wa Jehova witnes JW. Luther naye alikuwa freemanson???

Martin Luther
MArtin luther was a Jew and Musli hater .NA aliwaita Wayahudi anti-christ.

"
Know that no one can have indulged in the Holy Writers sufficiently, unless he has governed churches for a hundred years with the prophets, such as Elijah and Elisha, John the Baptist, Christ and the apostles... We are beggars: this is true.
"
 
Unaposema kanisa la awali ni kanisa la mitume na si hayo makanisa km ulivyoyataja.... Sasa swali ni kwamba Hao mitume waliamini ktk kuwaombea wafu? Kwanini hatuoni mfano wa mitume kuwaombea ata mmoja wa mitume mwenzao aliyetangulia kufa???

Ntuzu
Shukraan mno kwa ulizo jema ambalo lamfaa mwenye kujibu awe na maelezo ya kina na si aelewavyo yeye.

Kama litajibiwa basi nami ntakuwa mefarsika kutia langu ulizo.

Ahsanta nipo kipembeni hapa.
 
Pole sana....rudi usome upya historia ya kanisa na tafuta kuhusu mkutano wa Nicea (425 AD kama sijakosea) enzi za Constantine (aliyeanzisha rosali ndani ya kanisa), ndipo utajua nani aliviondoa na ujue kuwa wakati huo kanisa lilikuwa moja tu. Wa kwanza kujitoa alikuwa Martin Luther (miaka ya 1500) kwa hiyo kusema si kanisa katoliki waliotoa nakusamehe bure, pengine hujui, make a research. Mkutano wa Nicea ndiyo uliweka msingi mkubwa wa imani ya ukristo kikanisa-katoliki ikiwa hujui (mwulize padri au mjuzi wa historia ya kanisa katoloki atakuthibitishia hili)

KITABU cha Yakobo kinahusu Neema....Mwanzoni Martin Luther hakuwa na uelewa kuhusu neema. Na ukisoma nyaraka (thesis) zake za baadaye anakiri kuwa alitaka kufanya kosa kubwa kwa sababu ya kutomwacha Roho Mtakatiifu kumfundisha hapo mwanzo kwa kukipuuzia kitabu hiki na katika vitu ambavyo anakiri kuwa mwanzoni vilimtatizo ni neema na hakutaka kuondoa kitabu hicho tu hata kitabu cha Warumi na vingine vinavyosisitiza neema/grace. Na mwishowe anakiri kuwa Kitabu cha Yakobo ni mojawapo ya backborne za NT kwa sababu kila mtu anaokolewa kwa neema. (SIYO MAOMBI YA WAFU KAMA ULIVYOAMINISHWA NA WAPAGANI WALIOLITEKA KANISA). SO is Ufunuo, mwanzoni Luther hakuwa na ufahamu kuhusu Eschatology na hiyo mpaka sasa mapadre wengi hawana ufahamu wa kutosha kuhusu eschatology hata sasa.

Usijaribu kuleta mjadala tuanze kujadiliana "if"

Na elewa kuwa huu mjadala si vita ya kidini.

Hivyo vitabu vya deutrocanony ulishavisoma? vitafute uvisome kwanza ndipo utajua ni kwa nini viliondolewa na ni kwa vipi vinaweza kummislead mtu asipokuwa mwangalifu. Ni vitabu vya historia tu za vita na mapinduzi (coup) vya Israeli na watawala katika kipindi cha miaka 453 kati ya kitabu cha Malaki mpaka kuzaliwa Kristo (Mathew). Hata katika tanack havimo. vipo katika nyaraka za historia ya waisraeli kama vitabu vya Yosephas/josefus...na wengine.

Unajichanganya sana...Nimekuuliza kama Calvin hakumzuia Martin kuondoa vitabu vya Ufunuo na Yakobo hivi leo ungekuja kumwaga povu hapa.....?

Ngoja nikwambie Kanisa Katoliki halijawahi ongeza wala Punguza kitabu chochote katika Biblia tokea mwanzao...

Unaleta mambo ya Rozari hapa ambayo hayhusiani na mada...Kwa taafifa yako Rozari imeasisiwa na St. Dominic na sio Mtaguso wa NICEA...MTaguso wa NICEA ulikuwa kwa ajili ya Kanuni ya Imani iliyopitisha UTATU MTAKATIFU...Sjui kwann unataka kupotosha hapa..

Naomba nikuambie kitu hiki kuhusu vitabu hivi 7 na historia yake na uache upotoshaji...

Vitabu hivi saba viliandikwa karne za mwishoni kablla ya ujio wa Kristo...
Ilikuwa hivi; Vitabu hivi viliandikwa na Waisraeli/Wayahudi walioishi Misri ...Kutokana na kipindi hiko Mgiriki ndo alikuwa Mkoloni lugha ya Mawasilano ilikuwa ia Kigiriki...Hivyo basi ilikwapasa hawa ayahudi/Waisrael waandike Vitabu huvi kwa Lugha ya Ya kigiriki na si Kiebrania...

Kumbuka Agano la Kale lote liliandikwa kwa Lugha ya Kiebrania na hivi vitabu 7 viliandikwa lugha ya Kigiriki...

Baada ya ujio wa Yesu na mambo makubwa aliyoyafanya na kupelekea Kifo chake, pamoja kuitwa kwake Mungu na ukiangali Biblia Agano la Jipya liliandikwa lote kwa Lugha Kigiriki Waisraeli waliogopa kuvipokea Vitabu hivi vilivyo andikwa kwa Lugha ya kigiriki wakiofia Imani yao juu ya Yesu Kristo isije ikachanganywa...

Mkuu Historia ilianzia hapo na sio upotoshaji huo ambao wewe umehadithiwa....
RGforever, isotope MTAZAMO @buzybugmy
 
Last edited by a moderator:
Martin Luther and the 95 Theses - Facts & Summary - HISTORY.com
Pia kuna madai kama ilivyokuwa mwanzilishi wa Jehova witnes JW. Luther naye alikuwa freemanson???

Martin Luther
MArtin luther was a Jew and Musli hater .NA aliwaita Wayahudi anti-christ.

"
Know that no one can have indulged in the Holy Writers sufficiently, unless he has governed churches for a hundred years with the prophets, such as Elijah and Elisha, John the Baptist, Christ and the apostles... We are beggars: this is true.
"

Mkuu Jehova witness walijitenga toka kwa Wasabato...Hawa Walijitenga kwa madai juu ya UTATU MTAKATIFU...Walisema UTATU MTAKATIFU ni muendelezo wa Upagani ulianzishwa na Wakatoliki na Hivyo SDA wametekwa na Upagani huo...Hivyo wakaamua kujitenga...

Maajabu haya..
 
Naomba na mimi kuchangia japo kwa kifupi.

Mwanzo wa historia ya Waisraeli marehemu walifikiriwa kuwa wamefungiwa katika shimo lenye giza nene, wamesahaulika, na hawezi kumsifu Mungu...Rejea Zab. 6. 6:5; 30:9-10 pia Zab 88:10-12)

Baadaye iliingia imani kuwa Roho za wenye HAKI zimo mikononi mwa Mungu Rejea (Hek 3:1-7) na kwamba wafu watfufuka na baadhi yao watapata utukufu na wengine aibu Rejea (Dan: 12:2)

Waliokufa wakiteteea Imani yao waliamini Mungu atawafufua wapate uzima wa milele Rejea (2Mak 7:9)
Katika hatua hiyo ulijitokeza umuhimu wa kuwaombea wafu ili Mungu aondoe zambi zao....Mungu ni mkuu na anaweza yote tunaamini hivyo.. Rejea kitabu cha 2Mak 12:38-46)

Sasa Msingi huu haupo katika vitabu ambavyo havijapokelewa na makanisa ya Kiprotestanti ndiyo sababu ya mvutano kati yao na Kanisa katoliki..

Ahsanta..
 
Unajichanganya sana...Nimekuuliza kama Calvin hakumzuia Martin kuondoa vitabu vya Ufunuo na Yakobo hivi leo ungekuja kumwaga povu hapa.....?

Ngoja nikwambie Kanisa Katoliki halijawahi ongeza wala Punguza kitabu chochote katika Biblia tokea mwanzao...

Unaleta mambo ya Rozari hapa ambayo hayhusiani na mada...Kwa taafifa yako Rozari imeasisiwa na St. Dominic na sio Mtaguso wa NICEA...MTaguso wa NICEA ulikuwa kwa ajili ya Kanuni ya Imani iliyopitisha UTATU MTAKATIFU...Sjui kwann unataka kupotosha hapa..

Naomba nikuambie kitu hiki kuhusu vitabu hivi 7 na historia yake na uache upotoshaji...

Vitabu hivi saba viliandikwa karne za mwishoni kablla ya ujio wa Kristo...
Ilikuwa hivi; Vitabu hivi viliandikwa na Waisraeli/Wayahudi walioishi Misri ...Kutokana na kipindi hiko Mgiriki ndo alikuwa Mkoloni lugha ya Mawasilano ilikuwa ia Kigiriki...Hivyo basi ilikwapasa hawa ayahudi/Waisrael waandike Vitabu huvi kwa Lugha ya Ya kigiriki na si Kiebrania...

Kumbuka Agano la Kale lote liliandikwa kwa Lugha ya Kiebrania na hivi vitabu 7 viliandikwa lugha ya Kigiriki...

Baada ya ujio wa Yesu na mambo makubwa aliyoyafanya na kupelekea Kifo chake, pamoja kuitwa kwake Mungu na ukiangali Biblia Agano la Jipya liliandikwa lote kwa Lugha Kigiriki Waisraeli waliogopa kuvipokea Vitabu hivi vilivyo andikwa kwa Lugha ya kigiriki wakiofia Imani yao juu ya Yesu Kristo isije ikachanganywa...

Mkuu Historia ilianzia hapo na sio upotoshaji huo ambao wewe umehadithiwa....
RGforever, isotope MTAZAMO @buzybugmy

tatizo lako unategemea wikipedi inayoandikwa na wenye uelewa finyu kama wewe...mwishowe unaanza kutukana. Kama ni povu weewe ndiye unaanza kulimwaga.....calvin na martin luther wapi na wapi? theolojia yako ina mushkeli mkubwa sana. kwa kuwa umeanza kutukana basi inatosha. tafuta mwenye akili timamu nitaendeleza mjadala naye si wewe
 
Kwataarifa yako huwa situmii Wikipedia kujua mambo...Ni kwa nadra sana natumia wikipedia..

Hebu wacha kunifurahisha wewe ndugu...We Theolojia yangu umeijuliwa wapi weye...?

Ni hatari kwa mtu kama unayejinasibu eti una theology angali watu maarufu wa Reformation huwajui...Yani unajifanya humjui John Calvin...? Wacha utani bana..

Kwanza nimekudharau sana pale uliposema Sala ya Rozari imewekwa kwenye Mtaguso wa NICEA...Shame on you
 
CC Eiyer, Ishmael, 2013, Kichwa Ndio Mtu, Mkuu wa chuo, Ablessed, Utingo

Mathayo 5: 22 Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.

Luka 18:20 na MArko 10:19 Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako.20 Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu.21 Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.

Waebrania 12: 14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; 15 mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.

Mathayo 5:
44 .lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
46 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? 48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

NAweza kusema jambo dogo sana kwetu laweza kumpeleka mwanadamu jehanum. Tusamehe ili tuweze kusamehewa.
Pia nikisoma neno hili hapa linamtaka mwanadamu kuupata ukamilifu. KWahiyo tusipuuze kidogo tusije tukapotea. Nikimwangalia yule tajiri alifanya kila kitu akaambiwa anapungufu moja, Pia Bibilia inatuambia kupitia sala ya baba yetu Utusamehe makosa yetu kama sisi tunavyo wasamehe wale waliotukosea. Kipimo tunachowapimia wengine tutapimia tena na kujazwa hata kumwagika..

Kuhusu swala la kumwombea mfu:

Nakubaliana na Ablessed kuwa lipo neno nimeliwahi kuliona kwenye vitabu vya Deuterakanoni(Kanuni ya pili) likionyesha maombezi ya wafu yanaruhusiwa.
Pia nikapewa neno hili hapa chini wanalosema linaeleza kuwa kuna msamaha baada ya kufa. Ikiwa mtu ataombewa na watu huku duniani. Ila nashauri ikiwa hujaridhika na neno hili, ni heri ujiandae sasa hivi.. ni vyema zaidi.

MAthayo 12: 31 Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa.32 Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.
Mkuu umeelezea vema nami nakubaliana na wewe, hapo kwenye bold kweli ni vema mtu akajiandaa sasa hivi na si kungoja maombi ya baadae. Na pia kama mtu inampa ukakasi kwenye kuombea waliotangulia basi aweza kuacha na sidhani kama kuna hukumu ya kutofanya hivyo. Once again thank you for a wonderful explanation.
 
Mkuu hebu nieleze ni kwanini Martin Luther wakati anaondoa vitabu 7 avya Aggano la kale alitaka kuondoa kitabu cha Yakobo na Ufunuo......Hivi kama angefanikiwa kuviondoa vitabu vya Ufunuo na Yakobo leo ungekuja kusema vilikuwa havina uvuvio wa Roho Mtakatifu...????

Naomba pia nikusahihishe...Kanisa Katoliki halijawahi punguza wala kuongeza kitabu chochote katika Biblia....Oroginally Biblia ilikuwa na vitabu 73..

Kama unataka nikupe Historia ya Bbilia nitakupa...Mzozo kwanza hakuanzia kwa Martin Luther, ila ulianzia Karne za mwanzoni baada ya kufa kwa Yesu.....Vitabu hivyo viliachwa na Waisraeli kutokana na mapokeo yake yalikuwa katika Lugha ya Kigiriki....

Shusha nondo mkuu kwa faida ya wote
 
Mkuu kumbuka pia kuna roho wa upande wa pili nae huleta tafsiri akijifanya ni wa nuru! C unajua ht lucifer anaijua biblia so unaweza ukadhani unae kumbe sie....ndo maana Yakobo 4 inasema tujue kuzipambanua Roho
Na hapa ipo shida sn!
Unakumbuka pia tumeambiwa tuzijaribu Roho kwa hiyo kwa kufanya hivyo ni rahisi kutambua malaika wa nuru na Roho wa Mungu. Lkn kwa mada iliyopo mezani ni ngumu kufikia muafaka sababu tuna misingi tofauti ya imani.

Ninachofarijika ni kwamba karibu wote tunaamini Kristo alikufa na kukufufuka na atakuja kuwahukumu wazima na wafu. Huu ndio msingi wa imani ya Kikristo haijalishi ni dhehebu gani lkn kwenye haya mengine tunatofautiana sana kutokana na waaasisi wa haya madhehebu kwani wengine wanaamini wakatoliki waliongeza vitabu na wengine wanajua wengine waliondoa baadhi ya vitabu . Na hawa wote wanachokisema wanaamini kuwa ni sahihi.
 
Ntuzu
Shukraan mno kwa ulizo jema ambalo lamfaa mwenye kujibu awe na maelezo ya kina na si aelewavyo yeye.

Kama litajibiwa basi nami ntakuwa mefarsika kutia langu ulizo.

Ahsanta nipo kipembeni hapa.

Ahsante sn Rafiki yangu mpendwa wabara
 
Last edited by a moderator:
thank you
Mkuu hebu eleza kwa uzuri pale ambapo Petro alipomuona Musa na elia mpaka akamwambia Bwana na tujenge vibanda vitatu. Ikiwa waliokufa hawana uhusiano kabisa na walio hai je ni kwanini tena hawa walionekana. Nafikiri waweza eleza vizuri ili tuweze kuelewa nahisi lina uhusiano kidogo na mada hii. Please!!!!!!!!!!!!!!!
 
Shusha nondo mkuu kwa faida ya wote

Fuatilia thread zangu kun vipengele nimegusia hilo..

Unajua watu wengi huwa wanjua KAnisa Katoliki limeongeza vitabu katika Biblia....Kumbe wanasahau kuwa vitabu 7 vya agano la Kale katika Biblia vilipunguzwa na attempt kama hiyo ilitaka kufanyika katika vitabu vya AJ vya Yakobo na Ufunuo....

Sasa kwakuwa Waprotestani baadhi hawana vitabu hivi ndio unaona huu msuguano wa kuwaombeav wafu....

Ahsanta
 
Unakumbuka pia tumeambiwa tuzijaribu Roho kwa hiyo kwa kufanya hivyo ni rahisi kutambua malaika wa nuru na Roho wa Mungu. Lkn kwa mada iliyopo mezani ni ngumu kufikia muafaka sababu tuna misingi tofauti ya imani.

Ninachofarijika ni kwamba karibu wote tunaamini Kristo alikufa na kukufufuka na atakuja kuwahukumu wazima na wafu. Huu ndio msingi wa imani ya Kikristo haijalishi ni dhehebu gani lkn kwenye haya mengine tunatofautiana sana kutokana na waaasisi wa haya madhehebu kwani wengine wanaamini wakatoliki waliongeza vitabu na wengine wanajua wengine waliondoa baadhi ya vitabu . Na hawa wote wanachokisema wanaamini kuwa ni sahihi.

Hapo kwenye RED

Wakatoliki hawajawahi na wala hawato kuja kujaribu kupunguza neno lolote katika Biblia....Biblia ilikuwa na vitabu 73 na itakuwa hivyo mpaka mwisho..
 
Back
Top Bottom