Kwa nini tuwaombee waliokufa?

Kwa nini tuwaombee waliokufa?

Mkuu umeelezea vema , hapo kwenye kipengele cha Roho Mtakatifu nafikiri karibu wote wanae Roho wa Bwana shida ipo kwenye tofauti zetu za madhehebu . Na kwa jinsi hii hatutaweza kufikia muafaka.

Mkuu, shida si madhehebu tu. Shida ni baadhi ya watu kuuogopa ukweli. Ibada za wafu ni upagani. watu wanaogopa kuacha mabaya wanayoyatenda wanategemea ibada za wafu kuwa zitawatoa motoni?......unless Mungu stops to be God ndipo nitaamini ibada za wafu. Kwangu ni sawa na uganga wa kienyeji ambapo unakwenda kumwomba mganga/mchawi akunyenyulie roho ya bibi au babu au ndugu wa karibu aliyekufa ili akukinge na mabaya.

Tuwe jasiri kuface mapungufu yetu, tulijue Neno la Mungu na tuishi katika kweli. Falsafa mfu za makanisa na madhehebu yetu zilizotungwa na watu kwa kuangalia na kuyapalilia mapungufu yao ambazo zinapishana na Maandiko hazitatusaidia chochote.

Waebrani 9:27.........Baada ya kifo ni hukumu. Au andiko hili linyofolewe litolewe kwenye Maandiko?
 
Ndugu pendael usijedhani unasoma uzi na michango ya wasiyomjua MUNGU..ibaya ya kuombea wafu na kutambika kwa wafu wakutatulie matatizo yako panamashaka makubwa kukubalika kwake,kama tu kumtegemea mwanadamu ni laana leo iwe mtu alieishatangulia mauti?

Hiki ndio kipengele ambacho shetani amewashika watu vibaya sana!
Kipengele cha Dini! !
Ndo maana nawaonea huruma wakristo wengi hawajui neno....cc charminglady
 
Mkuu umeelezea vema , hapo kwenye kipengele cha Roho Mtakatifu nafikiri karibu wote wanae Roho wa Bwana shida ipo kwenye tofauti zetu za madhehebu . Na kwa jinsi hii hatutaweza kufikia muafaka.

Mkuu kumbuka pia kuna roho wa upande wa pili nae huleta tafsiri akijifanya ni wa nuru! C unajua ht lucifer anaijua biblia so unaweza ukadhani unae kumbe sie....ndo maana Yakobo 4 inasema tujue kuzipambanua Roho
Na hapa ipo shida sn!
 
Utingo, Mkuu wa Chuo. ....thanks much huo ndo ukweli ambao baadhi ya madhehebu yamepotosha watu kwa makusudi au kwa kutojua maandiko. ....G'tax hawa ndo wa kuombewa ili waijue kweli!
...lkn hakuna kumuombea mtu aliyekufa anatakiwa atengeneze mwenyewe kabla na ndio maana ya wokovu, unless kuja kwa Yesu kutakuwa hakuna maana. ....huo ni upagani na ni kifungo ambacho shetani anakifanyia kazi vzr sana.
 
Nami nichangie walau kidogo, ukisoma Kitabu cha Mhubiri 9 kuanzia fungu la tano utaona haya

5For the living know they will die; but the dead do not know anything, nor have they any longer a reward, for their memory is forgotten. 6 Indeed their love, their hate and their zeal have already perished, and they will no longer have a share in all that is done under the sun.

Wafu hawajui lolote
 
wanafanikiwa ndio bila hivyo wangeacha kitambo sana.

Uliwahi kusoma simulizi ya tajiri na maskini Lazaro?.....ili waache kupractice upagani wanataka mtu atoke kwa wafu aje awaambie. Bahati nzuri ni kwamba Mungu hawezi kufanya hivyo ila amewapa Maandiko wasome na waache, lakini kwa sababu ya kupenda kutenda dhambi hawataki kutii Maandiko.

Kama ibada za wafu zingekuwa na maana yoyote hakuna sababu ya kwenda kusali na kusingekuwa sababu ya Yesu kuja duniani na baada ya Yeye kuondoka, akamleta Roho Mtakatifu......waendesha ibada za wafu ni machampion wa kumpuuza Roho Mtakatifu maana kwa hakika anawashuhudia wasome Maandiko na waache upagani, lakini wanapuuza kwa sababu ya tamaa za miili yao katika kutenda dhambi.
 
Kwenye Blue: Suala la mtu kwenda mbinguni au kutokwenda...God has limited us to know as it is another dimension. Tafsiri yako ya mtu kuwa na hasira inawezekana ni ujinga wa wewe mwenyewe kutojua maana ya hasira? Kama unamhukumu mtu kuwa alikuwa na hasira wakati anakufa (which is awkward argument)...Nami nikuulize Yesu alipomfokea Petro hata akasema rudi nyuma yangu shetani, uungu wa Yesu ulikoma na hivyo Yesu alikoma kuwa mwana wa Mungu kwa sababu alifoka kuonyesha hasira yake?

Kwenye Red: nikujibu kirahisi....pengine hujui maana ya imani. imani ni kutarajia yajayo wewe binafsi ukiwa hapa duniani. Imani yako wewe uliye duniani haiwezi kubadili hukumu ya mtu aliyekwisha kufa na kuhukumiwa....soma Biblia uielewe. Fate ya mwanadamu iko mikononi mwake yeye mwenyewe na si kwa mtu mwingine. Ndiyo maana Biblia inasema atendaye uovu na azidi kutenda na atendaye haki azidi kutenda haki....maana kila tendo analolitenda mwanadamu awapo duniani lina malipo na hukumu...wewe huwezi kumshawishi Mungu abadili mshahara wa mtu, wakati mtu mwenyewe alisaini contract......ndiyo sababu tunashauriwa kumwomba Mungu atuwezeshe kushinda dhambi kila siku na atusamehe. If you cant do that ukitegemea sala za wafu...POLE
REMEMBER: You are the master of your own destiny, God only fulfills it.

Mkuu,

Naomba kuongezea kuwa hakuna uhusiano kati ya waliokufa na walio hai kama inavyosomeka katika Mhubiri 9:5-6; "kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lolote lililofanyika chini ya jua."

Tafakari.
 
kuanzia mleta mada na wote waliochangia kwa mtazamo pingamizi mnachotakiwa ni kujitafakari kama mna Roho wa Mungu wakati mnapo ya tafsiri maandiko matakatifu, sio kwa kufuata hisia zenu au mitazamo yenu mkajua ndivyo ilivyo, kumbukeni ya kuwa MUNGU ni mwenye huruma na upendo na hugairi hasira yake.kama mimi kwa imani ni tamuomba MUNGU kwa jina la YESU KRISTO ya kua kipindi kile atakaporudi BWANA marehemu baba yangu au mama yangu au mkristo mwenzangu nae akawe miongoni mwa wale wakumlaki BWANA, kwa kua nae aliamini kuwa KRISTO ni BWANA na akabatizwa katika maji na Roho,pale aliposhindwa kutimiza wajibu wake kwa namna yoyote basi kwa sadaka hii ya Misa takatifu akasamehewe. hapo mimi nitakuwa na kosa gani,ni wapi nilipomuomba huyo aliekufa au nivipi labda nimefanya matambiko kwa mzimu? kumbukeni MUNGU hughairi mabaya na humsikiliza yule amuombae kwa imani na pia mkijua ya kua huyo aliekufa hawezi kuomba tena sasa kuna ubaya gani mimi nilie hai nikimuombea? JITAFAKARINI JE MNA ROHO WA MUNGU?.

Biblia inasema 'Mwana hatabeba furushi la baba wala baba hata beba la mwana'. Na maandiko yanasema siku ya hukumu kila mtu atafuatwa na matendo yake mwenyewe. Laiti ingekuwa Mungu anasikiliza maombi kwa ajili ya marehemu basi kusingekuwa na Jehanum kwa wanadamu.

Ukisoma ule waraka wa Petro unasema hata baada ya kufa Yesu alishuka mpaka kwa wale waliokufa ili awape Injili waokoke, Je, hakukuwa na Ulazima Kanisa tukaingia kwenye maombi ili kuwaombea hao wafu wa zamani mpaka Yesu aende mwenyewe? Ni matendo yako na Imani yako ndio itakayokusaidia siku zako hapa duniani, mbali na hapo ukishakufa wewe subiri hukumu. Nakushauri, waombee watu wakiwa wazima wanajitambua na si wafu.
 
CC Eiyer, Ishmael, 2013, Kichwa Ndio Mtu, Mkuu wa chuo, Ablessed, Utingo

Pia naomba unisaidie iwapo mtu ameishi maisha yake ya uchaji wa Mungu kikamilifu na ikatokea wakati anakufa alikua na hasira au hakuweza kumsamehe mtu flani, je mtu huyo ataenda jehanamu?

Mathayo 5: 22 Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.

Luka 18:20 na MArko 10:19 Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako.20 Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu.

21 Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate. Waebrania 12: 14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; 15 mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.

Mathayo 5: 44 .lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.

46 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? 48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu. NAweza kusema jambo dogo sana kwetu laweza kumpeleka mwanadamu jehanum. Tusamehe ili tuweze kusamehewa.

Pia nikisoma neno hili hapa linamtaka mwanadamu kuupata ukamilifu. KWahiyo tusipuuze kidogo tusije tukapotea. Nikimwangalia yule tajiri alifanya kila kitu akaambiwa anapungufu moja, Pia Bibilia inatuambia kupitia sala ya baba yetu Utusamehe makosa yetu kama sisi tunavyo wasamehe wale waliotukosea. Kipimo tunachowapimia wengine tutapimia tena na kujazwa hata kumwagika..

Kuhusu swala la kumwombea mfu, Nakubaliana na Ablessed kuwa lipo neno nimeliwahi kuliona kwenye vitabu vya Deuterakanoni(Kanuni ya pili) likionyesha maombezi ya wafu yanaruhusiwa.

Pia nikapewa neno hili hapa chini wanalosema linaeleza kuwa kuna msamaha baada ya kufa. Ikiwa mtu ataombewa na watu huku duniani. Ila nashauri ikiwa hujaridhika na neno hili, ni heri ujiandae sasa hivi.. ni vyema zaidi.

MAthayo 12: 31 Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa.32 Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao
 
Bado ni mkanganyiko..hujasema kama kuna umaana wa kwenda kuwaomba wafu watutatulie matatizo yetu hapa duniani kama wengi wafanyavyo mala kadhaa makabulini kwa mababu,kama tu ilisemwa na alaaniwe amtegemeaye mwanadamu vipi amtegemeaye mtu alieisha kufa?

Kwa wa-Kristo, imekatazwa kabisa kuwaomba wafu.

Kumbukumbu la Torati 18: 10 - 12 ... inasema.....

10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.
12
Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.
 
wanafanikiwa ndio bila hivyo wangeacha kitambo sana.

indicator gani inakuthibitishia kuwa wanafanikiwa? kuna mmoja wao aliomba mtu atoke motoni na aende mbinguni na akathibitisha kuwa ametoka?.....!!!! Proof pekee iliyopo ni kuishi vema ukiwa hai na uwe mchaji wa Mungu tu. Mhubiri 9:5-6; "kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lolote lililofanyika chini ya jua."

Tafakari.
 
CC Eiyer, Ishmael, 2013, Kichwa Ndio Mtu, Mkuu wa chuo, Ablessed, Utingo

Mathayo 5: 22 Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.

Luka 18:20 na MArko 10:19 Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako.20 Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu.21 Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.

Waebrania 12: 14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; 15 mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.

Mathayo 5:
44 .lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
46 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? 48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

NAweza kusema jambo dogo sana kwetu laweza kumpeleka mwanadamu jehanum. Tusamehe ili tuweze kusamehewa.
Pia nikisoma neno hili hapa linamtaka mwanadamu kuupata ukamilifu. KWahiyo tusipuuze kidogo tusije tukapotea. Nikimwangalia yule tajiri alifanya kila kitu akaambiwa anapungufu moja, Pia Bibilia inatuambia kupitia sala ya baba yetu Utusamehe makosa yetu kama sisi tunavyo wasamehe wale waliotukosea. Kipimo tunachowapimia wengine tutapimia tena na kujazwa hata kumwagika..

Kuhusu swala la kumwombea mfu:

Nakubaliana na Ablessed kuwa lipo neno nimeliwahi kuliona kwenye vitabu vya Deuterakanoni(Kanuni ya pili) likionyesha maombezi ya wafu yanaruhusiwa.
Pia nikapewa neno hili hapa chini wanalosema linaeleza kuwa kuna msamaha baada ya kufa. Ikiwa mtu ataombewa na watu huku duniani. Ila nashauri ikiwa hujaridhika na neno hili, ni heri ujiandae sasa hivi.. ni vyema zaidi.

MAthayo 12: 31 Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa.32 Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.

Mkuu, kama nilivyosema hapo juu kuwa ibada hizi msingi wake ni vitabu vya Deutrocanon----kuna mambo unayopaswa kujua kuhusu vitabu hivi na hasa ibada za wafu zinatokana na kitabu cha wamakabayo:

1: Soma historia ya wamakabayo wakati baada ya elexander the gret kufa bila kuwa na mtoto (mrithi) ufalme wake ukagawanywa sehemu nne kwa majenerali wake. Jenerali antiochus epiphany aliyeitawala misri na Yudea akaamua kunajisi hekalu la wyahudi na masinagogi yote kwa kutoa nguruwe kama sadaka ya kuteketezwa ndipo kuhani mmoja na wanawe wakainuka kuanzisha vita na jeshi la epiphany, wakiwa vitani ndipo mmoja akawa anaomba kwa uhungu akimsihi Mungu ampokee mpiganaji mwenzake kwa sababu kazi waliyokuwa wanaifanya ni ya kutakasa hekalu na sinagogi.

2: Aliyeviondoa vitabu vya deutrocanoni kuwa havina uvuvio wa roho mtakatifu maana ni historia tu ya maisha ya israeli ikiwa ni pamoja na vitabu vya Ester (sehemu ya pili), Yuda bin sila, hekima za sulemani, tobiti, makabayo 1&2....etc ni kanisa katolic lenyewe......jiulize. Walipoviondoa kanisa katoliki lilikuwa kanisa la kiroho sana. Waliporejesha upagani huu martin luther akahoji wakakosa majibu kilichofuata unakijua.

niishie hapa lakini soma Mhubiri 9:5-6; "kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lolote lililofanyika chini ya jua."

Mkuu asante kwa kunijuza.... kuhusu neno la Mhubiri 9:5-9 nakubaliana na wewe ila nadhani neno hili linawalenga wale wenye mawazo kuwa Wafu wanaweza kumwathiri mtu aliyehai_hasa kwa wale wenye kuamini kuhusu Mizimu ya mababu, n.k. wengine wanaenda kumwaga pombe kwenye makaburi wakiamini wafu wanafufuka na wanajua kinachoendelea duniani n.k.

Swala gumu ni kujua iwapo upo msamaha baada ya Kufa ama katika ulimwengu ujao.
Binafsi nimewahi kusikia mahubiri ya Lusekelo akiziunga mkono zile taratibu za kuwaombea waliokufa wakati wa mazishi.

--------------
Kwa mfano niki-paraphrase yohana 12:31 hivi.. "
kila dhambi watasamehewa wanadamu katika ulimwengu huu na ule ujao isipokuwa ya kumkufuru roho mtakatifu" Nitakuwa nimekosea?? NAuliza
Pia kuna jambo moja najiuliza sana uhalali wake> swala La kuapa: mahakamani, Bingeni na sehemu nyingine ikiwa Yesu amekataza watu wasiape kwa mungu hata kwa kichwa chake mwenyewe..kwakuwa huwezi kutengeneza rangi ya nywele za kchwa chako.
 
Kwa wa-Kristo, imekatazwa kabisa kuwaomba wafu.

Kumbukumbu la Torati 18: 10 - 12 ... inasema.....

10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.
12
Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.
thank you
 
Duh! Mkuu sio makabayo ni Matayo labda kama ulimaanisha kitabu nisichokijua lakini kama ni Matayo 12:43 hapa Yesu alikua anazungumzia pepo wachafu.tena anazungumzia pepo saba walio waovu,sasa ukweli tunaoutafuta wa kuwaombea wafu na kupeleka shida zetu kwa wafu upo wapi katika mistali hii?au umechukua kitabu kingine cha Mungu nisichokijua ndo maana nilitaka kusaidiwa kujua umaana wa kuwaombea wafu,bado hujanijibu nikakuelewa ndugu!

Hajakosea kabisa...Ni kitabu cha Wamakabayo mkuu...Huenda unatumia Biblia yenye vitabu 66...Ila kwa Wakatoliki na Anglicans High Church, All Orthodx denomination pamoja na Coptic Christian na wenzao Ethiopian Orthodox....

Hiyo Bible yako ni ile ambayo Martin Luther aliondoa vitabu Saba vya Agano la Kale na alishindwa kufanikiwa kuondoa kitabu cha Yakobo baada ya reformer mwenzake Calvin kumzuia na kumwambia hivyo alivyoviondoa vinatosha,,,
 
Mkuu, kama nilivyosema hapo juu kuwa ibada hizi msingi wake ni vitabu vya Deutrocanon----kuna mambo unayopaswa kujua kuhusu vitabu hivi na hasa ibada za wafu zinatokana na kitabu cha wamakabayo:

1: Soma historia ya wamakabayo wakati baada ya elexander the gret kufa bila kuwa na mtoto (mrithi) ufalme wake ukagawanywa sehemu nne kwa majenerali wake. Jenerali antiochus epiphany aliyeitawala misri na Yudea akaamua kunajisi hekalu la wyahudi na masinagogi yote kwa kutoa nguruwe kama sadaka ya kuteketezwa ndipo kuhani mmoja na wanawe wakainuka kuanzisha vita na jeshi la epiphany, wakiwa vitani ndipo mmoja akawa anaomba kwa uhungu akimsihi Mungu ampokee mpiganaji mwenzake kwa sababu kazi waliyokuwa wanaifanya ni ya kutakasa hekalu na sinagogi.

2: Aliyeviondoa vitabu vya deutrocanoni kuwa havina uvuvio wa roho mtakatifu maana ni historia tu ya maisha ya israeli ikiwa ni pamoja na vitabu vya Ester (sehemu ya pili), Yuda bin sila, hekima za sulemani, tobiti, makabayo 1&2....etc ni kanisa katolic lenyewe......jiulize. Walipoviondoa kanisa katoliki lilikuwa kanisa la kiroho sana. Waliporejesha upagani huu martin luther akahoji wakakosa majibu kilichofuata unakijua.

niishie hapa lakini soma Mhubiri 9:5-6; "kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lolote lililofanyika chini ya jua."

Mkuu hebu nieleze ni kwanini Martin Luther wakati anaondoa vitabu 7 avya Aggano la kale alitaka kuondoa kitabu cha Yakobo na Ufunuo......Hivi kama angefanikiwa kuviondoa vitabu vya Ufunuo na Yakobo leo ungekuja kusema vilikuwa havina uvuvio wa Roho Mtakatifu...????

Naomba pia nikusahihishe...Kanisa Katoliki halijawahi punguza wala kuongeza kitabu chochote katika Biblia....Oroginally Biblia ilikuwa na vitabu 73..

Kama unataka nikupe Historia ya Bbilia nitakupa...Mzozo kwanza hakuanzia kwa Martin Luther, ila ulianzia Karne za mwanzoni baada ya kufa kwa Yesu.....Vitabu hivyo viliachwa na Waisraeli kutokana na mapokeo yake yalikuwa katika Lugha ya Kigiriki....
 
Mkuu asante kwa kunijuza.... kuhusu neno la Mhubiri 9:5-9 nakubaliana na wewe ila nadhani neno hili linawalenga wale wenye mawazo kuwa Wafu wanaweza kumwathiri mtu aliyehai_hasa kwa wale wenye kuamini kuhusu Mizimu ya mababu, n.k. wengine wanaenda kumwaga pombe kwenye makaburi wakiamini wafu wanafufuka na wanajua kinachoendelea duniani n.k.

Swala gumu ni kujua iwapo upo msamaha baada ya Kufa ama katika ulimwengu ujao.
Binafsi nimewahi kusikia mahubiri ya Lusekelo akiziunga mkono zile taratibu za kuwaombea waliokufa wakati wa mazishi.

MAthayo 12: 31 Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa.32 Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.

--------------
Kwa mfano niki-paraphrase yohana 12:31 hivi.. "
kila dhambi watasamehewa wanadamu katika ulimwengu huu na ule ujao isipokuwa ya kumkufuru roho mtakatifu" Nitakuwa nimekosea?? NAuliza
Pia kuna jambo moja najiuliza sana uhalali wake> swala La kuapa: mahakamani, Bingeni na sehemu nyingine ikiwa Yesu amekataza watu wasiape kwa mungu hata kwa kichwa chake mwenyewe..kwakuwa huwezi kutengeneza rangi ya nywele za kchwa chako.

Mkuu hii habarinya kuwaombea wafu ni Madhehebu ya Kiprotestant tuu ambayo hayaamni...Ila Early Chruch zote zinaamni...Kuaanzia Catholic, Orthodox, Anglican High Church, Coptic, Armenian Catholic na mengine mengi....
 
Mkuu asante kwa kunijuza.... kuhusu neno la Mhubiri 9:5-9 nakubaliana na wewe ila nadhani neno hili linawalenga wale wenye mawazo kuwa Wafu wanaweza kumwathiri mtu aliyehai_hasa kwa wale wenye kuamini kuhusu Mizimu ya mababu, n.k. wengine wanaenda kumwaga pombe kwenye makaburi wakiamini wafu wanafufuka na wanajua kinachoendelea duniani n.k.

Swala gumu ni kujua iwapo upo msamaha baada ya Kufa ama katika ulimwengu ujao.
Binafsi nimewahi kusikia mahubiri ya Lusekelo akiziunga mkono zile taratibu za kuwaombea waliokufa wakati wa mazishi.

MAthayo 12: 31 Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa.32 Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.

--------------
Kwa mfano niki-paraphrase yohana 12:31 hivi.. "
kila dhambi watasamehewa wanadamu katika ulimwengu huu na ule ujao isipokuwa ya kumkufuru roho mtakatifu" Nitakuwa nimekosea?? NAuliza
Pia kuna jambo moja najiuliza sana uhalali wake> swala La kuapa: mahakamani, Bingeni na sehemu nyingine ikiwa Yesu amekataza watu wasiape kwa mungu hata kwa kichwa chake mwenyewe..kwakuwa huwezi kutengeneza rangi ya nywele za kchwa chako.

chief...kimsingi ukishakufa you olny face the creator, God's court ni court pekee ambayo wewe mwenyewe ni shahidi na prosecutor-your deeds.

Na hii kitu ya kuombea wafu kama nilivyosema ni mojawapo ya sababu za kuparaganyika kanisa katoliki wakati wa Martin Luther.

Jambo lisilo kwenye Maandiko na haliwezi kuthibitishwa ni ushirikina. Hata kama anayelihubiri au kulitenda amevaa joho au kanzu iliyopambwa kwa dhahabu au almasi.
 
Back
Top Bottom