Mkuu wa Chuo, hata wewe mwenyewe unavyoandika tayari unajichanganya. Na hii ni kwa sababu ya kukariri au kukaririshwa maandiko. Kwanza kama biblia ingekuwa "principled" na "consistent" isingehitaji au isingeacha mwanya wa kuleta tafsiri tofauti tofauti wala uelewa tofauti tofauti kwa kuwa ingekuwa inalenga kutoa ujumbe uleule kwa kila msomaji. Sasa hata wewe unakiri kuwa inategemea jinsi gani watu wanavyofasiri maandiko na kuelewa maandiko, na hii ndiyo sifa kuu ya andiko ambalo siyo principled au andiko ambalo ni "subjective". Hebu tazama kuna madhehebu mangapi duniani yaliyotokana na kutafsiri biblia kila mtu kivyake vyake? Kama biblia ingekuwa consistent na principled ingewezesha kuwepo kwa dhehebu moja tu ambalo linafuata kanuni za aina moja za kibiblia, lakini kwa kuwa iko subjective imeshindwa katika hilo na ndiyo maana kuna utitiri wa madhehebu na hakuna fomula ya kuamua lipi ni la kweli au la uongo kwa kuwa kila mmoja anatafsiri ukweli au uongo kadiri aonavyo yeye kwa kutafsiri maandiko ambayo hayana fomula kadiri aonavyo yeye. Tena kila mmoja anajigamba kuwa kuwa dhehebu lake ni la kweli zaidi na la kibiblia zaidi. Mifano mingine pia soma maandiko yafuatayo na useme hapa na watu wenye akili zao "great thinkers" pia wataona kiukweli kama yanaonyesha consistency yoyote. Pia umeongelea torati kana kwamba kwa sasa haihusiki tena lakini hayo ni mawazo ya kwako siyo ya biblia, soma pia maandiko hapa chini kuhusu ulazima wa torati hata sasa, au la ndiyo ushahidi zaidi wa biblia kukosa consistency. Vile vile umepinga kuhusu aina ya dhambi nayo ni mawazo ya kwako kwa kuwa biblia iko wazi soma pia hapo chini. Na hayo ni baadhi tu ya maandiko. Nakushauri uache kukariri maandiko na usikubali kukaririshwa maandiko, jisomee na kutafakari mwenyewe kwa makini ili upate ufahamu ulio huru na kweli:
MAANDIKO KUHUSU DIVAI/POMBE:
Hesabu 15: 4 ndipo yeye atakayetoa matoleo yake na amtolee Bwana sadaka ya unga ya sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba uliochanganywa na robo ya hini ya mafuta;
5 na divai kwa sadaka ya kinywaji, robo ya hini, utaiandaa pamoja na sadaka ya kuteketezwa, au kwa dhabihu ya kuchinjwa, kwa ajili ya kila mwana-kondoo.
7 na kwa sadaka ya kinywaji utasongeza sehemu ya tatu ya hini ya divai, kuwa harufu ya kupendeza kwa Bwana. 10 Tena utasongeza nusu ya hini ya divai kwa sadaka ya kinywaji, kwa sadaka iliyosongezwa kwa moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana.
Hesabu 28:7 Na sadaka yake ya kinywaji itakuwa robo ya hini kwa mwana-kondoo mmoja; hiyo sadaka ya kinywaji, ya kileo, utammiminia Bwana katika mahali hapo patakatifu.
Hesabu 28:14 Tena sadaka zake za vinywaji zitakuwa nusu ya hini ya divai kwa ng'ombe, na sehemu ya tatu ya hini kwa kondoo mume, na robo ya hini kwa mwana-kondoo; hii ndiyo sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi katika miezi yote ya mwaka.
15 Tena mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi kwa Bwana itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.
Mhubiri 10:19 Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; Na fedha huleta jawabu la mambo yote.
Mhubiri 9: 7 Wewe enenda zako, ule chakula chako kwa furaha, unywe mvinyo yako kwa moyo wa kuchangamka; kwa kuwa Mungu amekwisha kuzikubali kazi zako.
1Timotheo 5:23 Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara.
Luka7:33 Kwa kuwa Yohana Mbatizaji alikuja, hali mkate wala hanywi divai, nanyi mwasema, Ana pepo.
34 Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa; nanyi mwasema, Tazama, mlafi huyu, na mnywaji wa divai, rafiki wao watoza ushuru na wenye dhambi.
Yohana 2:7 Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu.
8 Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka.
9 Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi,
10 akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa.
Mathayo 15:11 Sikilizeni, mfahamu; Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho mtu unajisi.
17 Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni?
18 Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.
19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;
Mithali 23: 20 Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo;...
31 Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu; Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;
32 Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama ----.
Mithali 31:4 Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo?
5 Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.
6 Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.
7 Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake.
Wagalatia 5:19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
21 husuda,
ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo,
katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
KUHUSU TORATI
Mathayo 5:17 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
18 Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka, hata yote yatimie.
Luka16:17 Lakini ni vyepesi zaidi mbingu na nchi vitoweke, kuliko itanguke nukta moja ya torati.
KUHUSU AINA ZA DHAMBI
1Yohana 5:15 Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.
16 Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo.
17 Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.
BAADHI YA MAANDIKO MENGINEYO YENYE UTATA
Mhubiri 7: 16 Usiwe na haki kupita kiasi; Wala usijiongezee hekima mno; Kwani kujiangamiza mwenyewe?
17 Usiwe mwovu kupita kiasi; Wala usiwe mpumbavu; Kwani ufe kabla ya wakati wako?
Mhubiri 3:19 Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili.
20 Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena.
Hii nakataa Biblia haijipingi, ila inatokana na jinsi gani ya watu wanavyofasiri maandiko na uelewa wa maandiko... Biblia haijipingi... labda ulete maandiko yanayojipinga halafu tujadili tuone kama ni kweli...
kwanza hayo maelezo yako unatakiwa uelewe Biblia ni nini!? Unatakiwa uelewe ni kwanini vitabu vya Aprokifa havikuwekwa, Halafu na kina nani walioandika Biblia kama unavyosema... lakini naona
Utingo amejitahidi kuelezea lakini sijui haujasoma maelezo yake...
Hapo nilipoweka red, Unaanza kuongelea habari za Joseph Smith nabii wa Wamormons kanisa lake alilolianzisha mwaka 1827, kwa kifupi unaanza kuingiza imani za ajabu, tunapokuja katika neno la Mungu inabidi tuangalie neno linasemaje na sio kuanza kuingiza mafundisho ya watu, msingi wetu ni neno la Mungu... ukweli huwa una njia yake, na sio kubuni vitu na kuanza kuvisapoti kuvitengenezea njia...
Yohana 8:32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
Hapo nilipoweka blue ni kama nilivyosema mwanzo ni namna gani ya kuelewa scripture... kwa hiyo bado kuna shida hapo
Hapo nilipoweka purple, Labda ungeleta maandiko hapa tunaruhusiwa kuoa wake wengi hapa mke mmoja ndio tunaweza tukajadili, lakini vinginevyo naona ni mafundisho ya watu tu, kama kina Joseph Smith...
Nani alikwambia baraza limeandika vitabu vya kwenye Biblia!? huoni kama unachokisema sio kweli!? sidhani hata kama unajua unachokizungumza... Yaani na mafundisho ya Wa Mormons unataka yafuatwe na watu, chukua hii verse inavyosema...
2 Timotheo 3:16
Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; KWA HIYO TORATI SIYO ANDIKO LENYE PUMZI YA MUNGU?
Labda nikuulize swali, tunaishi kipindi cha torati au!? nani alikwambi kuna dhambi kubwa na dhambi ndogo!?
Warumi 5:20 Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi;
Warumi 3:20 kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.
Warumi 6:14 Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.