Kwa nini tuwaombee waliokufa?

Kwa nini tuwaombee waliokufa?

Kumbe wewe ni mbumbumbu tuuu....Kamauulize mkuu wa shule ya lessoni atakuambia alikovipeleka....

Unaijua historia ya Usabato na Mama Hellena White..?

Huna haja ya kutukana we toa elimu alivipunguza lini na akavipeleka wapi mbona swali jepesi kama una taarifa
 
Historia ya ukusamyaji wa Biblia ni moja katika historia ya Mambo makubwa yaliyofanywa na kanisa Katoliki..

Unajua historia ya Usabato na Mama Hellena White..?

Kuhusu ukatoliki we ni cadaver wakatoliki biblia waikusanye ili iweje ? sala kuu ni ya mama maria ambayo kwenye bible haiko na wala yesu hakuagiza tukitaka kusali tumuombe mamake.
 
Hizo ni ibada zilizoanzishwa na shetani.Mungu yupo wazi katika maandiko kwamba shida zetu tuzipeleke kwake aidha mojakwamoja au kwa sisi wakristo kupitia kwa Yesu Kristo kwani imeandikwa 'kila mtakaroliomba kupitia kwangu Baba yenu aliye mbinguni atawatimizia" Lakini kwa mapungufu yetu tunashika njia zisizofaa.Lakini pia ujue mtu akisha kufa ni hukumu tu hata ukishinda makanisani na misikitini unamuombea hakuna litakalobadilika
 
Kuhusu ukatoliki we ni cadaver wakatoliki biblia waikusanye ili iweje ? sala kuu ni ya mama maria ambayo kwenye bible haiko na wala yesu hakuagiza tukitaka kusali tumuombe mamake.

Ume-panic kama magamba ya CCM...

Hahahahahaha....Hujui biblia uliyoishika ni Mapokeo ya Kanisa Katoliki...hahahaha..hebu nieleze Biblia imekusanywa na nani..???Daaaah

Zingine hizo ni porojo...


Hujanijibu...Unajua historia ya Mama Hellena na Usabato...? Nijibu fasta...
 
Hizo ni ibada zilizoanzishwa na shetani.Mungu yupo wazi katika maandiko kwamba shida zetu tuzipeleke kwake aidha mojakwamoja au kwa sisi wakristo kupitia kwa Yesu Kristo kwani imeandikwa 'kila mtakaroliomba kupitia kwangu Baba yenu aliye mbinguni atawatimizia" Lakini kwa mapungufu yetu tunashika njia zisizofaa.Lakini pia ujue mtu akisha kufa ni hukumu tu hata ukishinda makanisani na misikitini unamuombea hakuna litakalobadilika
Unapingana na maandiko..?

Au unatumia biblia iliyopunguzwa ikabakiwa na vitabu 66..?
 
Tunawaombea hasa waliokua Toharani,waende kwenye uzima wamilele.Tunawaombea watoke huko ili tuongeze waombezi wengi zaidi.
 
Tunawaombea hasa waliokua Toharani,waende kwenye uzima wamilele.Tunawaombea watoke huko ili tuongeze waombezi wengi zaidi.

Kivipi ndugu...toa utetezi wako vizuri nielewe nipate darasa,sijakuelewa
 
Ndio maana mtakatifu Paulo katika barua yake kwa Wafilipi 1:21 anatushawishi kuwa tujirudi na kuikubali maana sahihi ya kifo, kwamba kifo hakitutenganishi na wenzetu katika Kristu, wala na Kristu mwenyewe, na kwamba sisi tukifa tunakufa katika Kristu na tutaishi naye, kumbe baada ya ubatizo wetu hakuna kinachoweza kututenganisha katika umoja aliotuombea Kristu kwamba tuwe na ?umoja kama wao UTATU MTAKATIFU walivyo wamoja?.

Tunaalikwa kuona kuwa kifo si mwisho wa maisha bali ni mwanzo wa maisha mapya katika Kristu, maisha ambayo sina shaka kila mwanadamu mwenye akili timamu anayatamani kuyarithi. Sala zetu na sadaka zetu zina thamani ya pekee mbele za Mungu na kwa ajili ya ndugu zetu waliotoharani. Hatuzungumzii kuyabadili mawazo ya Mungu au kumhonga Mungu kwa sadaka na sala zetu kama wengine wanavyotufikiria katika siku hii tunapowaombea ndugu zetu marehemu, kitu cha msingi na cha uhakika ni nia yetu njema katika sala, sadaka na maombezi kwa ajili ya ndugu zetu.

Ni ukweli usiopingika kwamba katika umoja wetu na ndugu zetu marehemu na watakatifu Mungu anakuwepo kati yetu, anazibariki na kuzikubali nia zetu. Kumbe kuwaombea marehemu ni tendo la kiimani, na tunapaswa kufanya kwa imani na kwa hakika itazaa matunda mema katika imani, tusonge mbele na nia yetu njema katika hili, bila aibu na hofu yoyote, sisi tunaamini na tunajua kwa nini tunafanya hivyo.

Tunapowakumbuka ndugu zetu marehemu, tukumbuke kwamba na sisi ni marehemu watarajiwa ili tufe katika hali ya neema inayotakiwa katika kuurithi uzima wa milele. Kama kuna jambo tunalopaswa kuwa na uhakika nalo ni kufa, kumbe tunapaswa daima kuwa tayari, kwa sababu hatujui siku wala saa atakapotuita Mungu toka maisha haya.

Ni bahati mbaya hatupendi kusika neno kufa katika maisha yetu licha ya kulizungumzia, lakini cha kushangaza ukimwuliza mtu kama anapenda kwenda kwa Mungu kila mmoja anapenda awe ya imani gani, tunasahau kuwa hatuwezi kurudi kwa Mungu bila kufa, na kufa ni mabadiliko ya ghafla ya maisha ya sasa na kuingia katika maisha ya milele tukifa katika neema ya Mungu.
 
Nimekua najiuliza ni kwa nini mala nyingi hasa mwisho wa mwaka utasikia watu wengi wanakimbia majumbani mwao hasa vijijini na lengo ni kwenda kuwaombea ndugu walioishatangulia kwa maana ya kufa.

Wanaenda mbali na kupeleka maombi yao juu ya maisha yanayowazunguka kwa hao waliokufa,ni kweli kuna maana yoyote au kuna ulazima wa kufanya hili?kama ni kweli MUNGU tunaemuabudu na kuamini kua yupo na ndiyo alietuumba anapata nafasi ipi iwapo tutafikia kupeleka shida zetu kwa wafu?
Yohana 11:11-45
 
Nimekusoma mkuu,nakua nafikili sana jambo hili na tena wafanyao haya ni wale wale tunaowaona wanaingia kwenye nyumba za ibada kila mala,mizimu ni kitu gani?

Na kama ni wafu nini kinachofanya kazi kwao juu walio hai, iweje babu wa babu alikua mzinzi, mlevi, mchawi na kila aina ya dhambi na mtu anajua lakini anaenda kumuomba makaburini amsaidie,napata shida hapa labda nielimishwe vyema
muzimu ni ibada asilia walizotumia mababu toka enzi.na wanaamini zinawasaidia.tofauti na dini mapokeo zielezeazo jambo lenye utata liitwalo mungu.
 
Duh! Mkuu sio makabayo ni Matayo labda kama ulimaanisha kitabu nisichokijua lakini kama ni Matayo 12:43 hapa Yesu alikua anazungumzia pepo wachafu.tena anazungumzia pepo saba walio waovu,sasa ukweli tunaoutafuta wa kuwaombea wafu na kupeleka shida zetu kwa wafu upo wapi katika mistali hii?au umechukua kitabu kingine cha Mungu nisichokijua ndo maana nilitaka kusaidiwa kujua umaana wa kuwaombea wafu,bado hujanijibu nikakuelewa ndugu!
makabayo ni sura inayopatikana kwenye agano la kale la mwanzo kabla
Ya kuchakachuliwa mkuu.
 
na utajuaje ikiwa wanafanikiwa?
ndo pakuwaliza mkuu.mtu hawezi fanya kitu kisicho faida.maana wengine ni watu maarufu wenye uwezo na heshima kubwa kwenye jamii.wasomi waluotukuka.nafikiri kuwauliza ndio jambo stahiki zaidi
 
Bibilia yenyewe ni mapokeo hivyo hakuna sababu ya kukataa mapokeo.. Kuhusu kuombea wafu someni makabayo wa 2 utaona hiyo habari kwa ukamilifu wake.. Pia Yesu mwenye alisema kuwa mwanadamu atasamehewa dhambi katika ulimwengu huu au ule ujao. Isipokuwa dhambi ya kumkufuru roho mtakatifu.. Je ulimwengu ujao ni upi?? Tafakari.. Kuombea marehemu kinachofanyika ni kumuomba Mungu mwingi wa rehema awasamehe makosa yao kama alivyofanya Yuda makabayo katika kitabu cha makabayo wa 2...
 
Watu walio kufa hawana tofauti na kiumbe mnachokiita mungu.......kwasababu wote hawa exists...

Na hivyo vitabu mnavyo viita vitabu vitakatifu.....mmeaminishwa tuu...so sion tofaut na wanao tambika au mizimu.....


#godless and happy#
Blv in good not god
 
Hizo ni Ibada za Matambiko, wanaposema wanaenda kuwaombea marehemu basi ujue wao ndo wanapeleka hoja kwa marehemu ili wasafishiwe mambo yao.

Ni inahusu na Ibada za Mizimu, ni somo pana sana kuhusu Mizimu, hii huwa inaabudiwa kizazi hadi kizazi. Mungu alieumba Mbingu na Nchi kamwe hasikilizi maombi ya Wafu na kupitia Biblia Mungu hajaruhusu maombi ya Wafu.


Hivi kwani Lazaro alifufuliwaje?
 
Kiukweli wanadamu wengi hupenda kujiliwaza moyo na hii huenda mpaka kuwaombea marehem zao wakidhani bado wanawaskia au hata kudhani maombi yao yanaweza kuwapeleka peponi. ukweli ukishakufa na lako limeisha. Tuache kujiliwaza kwa uongo na imani zisizo na ukweli
 
Back
Top Bottom