GuDume
JF-Expert Member
- Jan 18, 2015
- 6,651
- 14,337
Pendaeli ibada za wafu ni totally ibada za shetani kibiblia hamna hicho kitu. Ukisema hivyo vitabu vingne vya makabayo n.k nmevisoma. Si vitabu vya kiuungu. Ni vitabu vilivyokosa upako wa Mungu ni vya kihistoria zaidi na si vya kusifu,kutukuza matendo ya Mungu. Kufa ni mara moja tu na baada ya kifo hukumu. Kama kungekuwa na suala la kuweka watu toharani basi kulikuwa hakuna haja ya kuja Yesu. Unakumbuka hadithi ya Lazaro? Mungu alimwambia walioko dunian wawasikilize mitume na manabii walioko huku dunian. Mtu akifa hata aombewe na mapadre,maaskofu na wachungaji wote it wont help. Binadamu unapaswa utengeneze maisha yako ukiwa hai. Usidanganyike kuna kuombewa na sadaka zitakusaidia...hakuna neno la namna hiyo na huo ni upagan. Kama ambavyo pia hakuna watakatifu wanaoweza kutuombea. Yesu alisema yeye ndiye njia ya kweli na uzima na mtu haend kwa Mungu bila kupitia yeye. So hamna kona kona wala short cut hapo. Si mama,baba ndugu za yesu wanaoweza kukusaidia zaidi ya baba yake wa kiroho yaani Mungu.