ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,030
- 61,298
Ukikaa muda bila kufanya mazoezi halafu siku ukirudi kukimbia ukaanza kuhisi kuwasha tumboni au kifuani mara nyingi ni mwili wako una-react na kitu kinaitwa histamine. Hii ni chemical ambayo mwili huwa nayo naturally na huwa inahusika kwenye allergy au kuwashwa kwa ngozi. Unapoanza kukimbia baada ya muda mrefu, moyo unapiga faster, damu inaanza kutembea kwa nguvu na mishipa ya damu inapanuka, hivyo mwili unaweza kutoa histamine zaidi kuliko kawaida. Ndiyo maana unahisi ngozi inawasha hasa tumboni, kifuani au hata mgongoni. ila hali itapungua kadri mwili unavyoanza kuzoea mazoezi tena.