Kwa nini vyakula vya Africa havisambai duniani au kupendwa kwenye mabara mengine?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Waafrika wanapenda na wanaona ufahari sana kula Mikate, Soseji, tambi, Sambusa, Pizza, Wali, biriani, Chips, crips, Shawarma na vyakula vingine vingi kutoka sehemu mbalimbali za dunia ila huko kwingine duniani hawana muda na ugali, githeri, jollof, fufu, injera, chips mayai na vyakula vingine vya asili ya Africa!
Tatizo ni nini? Vyakula vyetu vina shida gani?
 
Mbona Ethiopian food na Ghananian / Nigerian zimesambaa sana hata nje ya Africa.

Ukisafiri miji mikubwa hukosi mgahawa mmojawapo wa vyakula hivi, ila East African food bado sana, labda ni kwa sababu vyakula vyetu vingi maarufu ni vya mapokeo kutoka kwa wahindi na waarabu (pilau, wali, michuzi michuzi etc.).
 
Kwa Nini hatujifunzi Mambo ya asili tumeyaacha makumbusho hata dini zetu mitambiko na Mila hatujifunzi zetu...lugha zetu tu hatuzijui kuziandika au kuzisoma...
 
Waafrika wanapenda na wanaona ufahari sana kula Mikate, Soseji, tambi, Sambusa, Pizza, Wali, biriani, Chips, crips, Shawarma na vyakula vingine vingi kutoka sehemu mbalimbali za dunia ila huko kwingine duniani hawana muda na ugali, githeri, jollof, fufu, injera, chips mayai na vyakula vingine vya asili ya Africa!
Tatizo ni nini? Vyakula vyetu vina shida gani?
Ugali si chakula cha Afrika.

Mahindi yamekuja Afrika kutoka Amerika miaka ya karibuni tu hapa kwenye miaka ya 1500 tu.

Mahindi yamekuja Africa na biashara za Africa na America pamoja na utumwa (Transatlantic Slave Trade) na kuenezwa na ukoloni.
 
Mahindi ndio yalikuja Africa kutoka America ila ugali ni chakula cha Waafrika tena kusini mwa jangwa la Sahara, sijataka kujikita kuangalia maeneo ya asili ya mazao bali bidhaa za vyakula zinazotengenezwa na hayo mazao popote yanapizalishwa duniani leo hii.
 
Mbona Ethiopian food na Ghananian / Nigerian zimesambaa sana hata nje ya Africa.

Ukisafiri miji mikubwa hukosi mgahawa mmojawapo wa vyakula hivi ila East African food bado sana, labda ni kwa sababu vyakula vyetu vingi maarufu ni vya mapokeo kutoka kwa wahindi na waarabu (pilau, wali, michuzi michuzi etc.).
Customers wake wengi ni watu wa Africa.
Mfn: Mexican foods zinapendwa karibu na race zote duniani ila vyakula vyetu vinapendwa sisi tu black.
 
Mahindi ndio yalikuja Africa kutoka America ila ugali ni chakula cha Waafrika tena kusini mwa jangwa la Sahara, sijataka kujikita kuangalia maeneo ya asili ya mazao bali bidhaa za vyakula zinazotengenezwa na hayo mazao popote yanapizalishwa duniani leo hii.
Waafrika wametawaliwa, hawajatawala, ndiyo maana si vyakula tu, hata lugha zao hazijasambaa.

Kuna watu huko nje ndiyo kwanza wanaanza kugundua vyakula na mapishi ya Kiafrika.

Ukikaa majiji kama New York City kuna restaurants nzuri sana za Waafrika zinapendwa sana. Nishaenda restaurants za wa Senegal, Wa Ethiopia mpaka wa Kenya wanapika vyakula vyao vizuri sana vinapendwa ila kupata viungo kirahisi na kujua kupika kwa watu wa nje si rahisi. Pia kuna watu wengi hawana interest sana kujaribu vyakula tofauti.

Pia chakula kama ugali ni tasteless na nutritionless mimi huwa nakula ugali nikiwa na Watanzania kama wamepika wao ila kwangu sili ugali.

Sijawahi kupika ugali kwangu Marekani miaka yote niliyokaa.

Ushanielewa? Nimekaa Marekani tangu 1990s, sijawahi kupika ugali hata siku moja. Huwa nakula ugali nikitembelea Watanzania tu.

Hususan ugali mweupe ni chakula cha kijinga sana kwa sababu ni mahindi yaliyokobolewa na kuondolewa nutrients kama zote ukabakishiwa wanga tu.

Hivi ni vyakula vya watu wanaoangalia zaidi kushiba kuliko kupata virutubisho. Huko nje watu wanaangalia zaidi kupata virutubisho kuliko kushiba wanga tu.
 
We’ve been taught to admire imported culture" na kudharau vya kwetu. Hatujavipa hadhi ya kimataifa kama ambavyo wao huvipa vyao, yet our food tells richer stories, rooted in identity and resilience.
 
Waafrika wametawaliwa, hawajatawala, ndiyo maana si vyakula tu, hata lugha zao hazijasambaa.

Kuna watu huko nje ndiyo kwanza wanaanza kugundua vyakula na mapishi ya Kiafrika.

Ukikaa majiji kama New York City kuna restaurants nzuri sana za Waafrika zinapendwa sana. Nishaenda restaurants za wa Senegal, Wa Ethiopia mpaka wa Kenya wanapika vyakula vyao vizuri sana vinapendwa ila kupata voungo kirahisi na kujua kupika kwa watu wa nje si rahisi. Pia kuna watu wengi hawana interest sana kujaribu vyakula tofauti.

Pia chakula kama ugali ni tasteless na nutritionless mimi huwa nakula ugali nikiwa na Watanzania kama wamepika wao ila kwangu sili ugali.

Sijawahi kupika ugali kwangu Marekani miaka yote niliyokaa.

Ushanielewa? Nimekaa Marekani tangu 1990s, sijawahi kupika ugali hata siku moja. Huwa nakula ugali nikitembelea Watanzania tu.

Hususan ugali mweupe ni chakula cha kijinga sana kwa sababu ni mahindi yaliyokobolewa na kuondolewa nutrients kama zote ukabakishiwa wanga tu.

Hivi ni vyakula vya watu wanaoangalia zaidi kushiba kuliko kupata virutubisho. Huko nje watu wanaangalia zaidi kupata virutubisho kuliko kishiba wanga tu.
Mkuu ebu toa ushauri nini kifanyike ili ugali uwe na virutubisho.
 
Shusha nondo zaid na zaid
 
Mkuu ebu toa ushauri nini kifanyike ili ugali uwe na virutubisho.
Ugali wa dona ule wa mahindi yasiyokobolewa, yaliyosagwa tu, una virutubisho vingi tu.

Kwa mfano, ugali wa dona una protini nyingi tu zinakaa kwenye pumba.

Ukisaga mahindi bila kukoboa ugali wake una protini nyingi tu.

Tatizo tunataka ugali uwe mweupe, bila kujua kuwa ule weupe maana yake ni kwamba ugali hauna virutubisho una wanga tu.
 
Ugali si chakula cha Afrika.

Mahindi yamekuja Afrika kutoka Amerika miaka ya karibuni tu hapa kwenye miaka ya 1500 tu.

Mahindi yamekuja Africa na biashara za Africa na America pamoja na utumwa (Transatlantic Slave Trade) na kuenezwa na ukoloni.
Kwa hiyo sisi chakula chetu kilikua nini mkuu kabla ya kuletwa kwa mahindi ?
 
Mbona Ethiopian food na Ghananian / Nigerian zimesambaa sana hata nje ya Africa.

Ukisafiri miji mikubwa hukosi mgahawa mmojawapo wa vyakula hivi, ila East African food bado sana, labda ni kwa sababu vyakula vyetu vingi maarufu ni vya mapokeo kutoka kwa wahindi na waarabu (pilau, wali, michuzi michuzi etc.).
Au Michuzi blog haitangazi misosi yetu kwenye account yake
 
Ugali wa dona ule wa mahindi yasiyokobolewa, yaliyosagwa tu, una virutubisho vingi ymtu.

Kwa mfano, ugali wa dona una protini nyingi tu zinakaa kwenye pumba.

Ukisaga mahindi bila kukoboa ugali wake una proymtini nyingi tu.

Tatizo tunataka ugali uwe mweupe, bila kujua kuwa ule weupe maana yake ni kwamba ugali hauna virutubisho una wanga tu.
Wapenda Sembe siku hizi wanajitetea wanasema mahindi yanapigwa sumu sana kuhifadhiwa kwa hiyo ndio maana wanayaosha na kukoboa kuondoa sumu, wafanyabiashara wanasema Dona inaharibika mapema kuliko sembe!
 
Wafrika wanakula vyakula vikiwa na asili yake ya uzalishwaji/uvunwaji (raw food), huku wenzetu wakila vyakula vilivyoogezewa thamani kutoka kuvunwa kakwe (processed food).
Swali, kwanini wenzetu hawali?
Jibu, kwa nini sisi hatuli mapumba ya kuku?​
 
Ugali wa dona ule wa mahindi yasiyokobolewa, yaliyosagwa tu, una virutubisho vingi tu.

Kwa mfano, ugali wa dona una protini nyingi tu zinakaa kwenye pumba.

Ukisaga mahindi bila kukoboa ugali wake una protini nyingi tu.

Tatizo tunataka ugali uwe mweupe, bila kujua kuwa ule weupe maana yake ni kwamba ugali hauna virutubisho una wanga tu.
Mkuu vijana hawajui inabidi Wizara ya Elimu iweke Somo la vyakula Secondari mpaka chuo kikuu, Yani niaibu msomi wa Elimu ya juu kutokuja gani vina faida gani. Nilishangaa sikuhizi wajawazito wakienda clinic wakipimwa wingi wa damu wanaambiwa wanaupufu wa damu na wanapewa vidonge, yani hawajui wale mboga gani ili waongeze damu mwilini. Huyu hajui faida ya Mahindi na atakua kama ana mtoto au nyumbani kwao walikua hawanyi uji wa ndona na ulezi.
 
Back
Top Bottom