Kwa nini vyakula vya Africa havisambai duniani au kupendwa kwenye mabara mengine?

Kwa nini vyakula vya Africa havisambai duniani au kupendwa kwenye mabara mengine?

Wafrika wanakula vyakula vikiwa na asili yake ya uzalishwaji/uvunwaji (raw food), huku wenzetu wakila vyakula vilivyoogezewa thamani kutoka kuvunwa kakwe (processed food).
Swali, kwanini wenzetu hawali?
Jibu, kwa nini sisi hatuli mapumba ya kuku?​
Vyakula vyetu ni ghalama sana kuandaa na upatikanaji sisi kufuga mifugo na kilimo chetu ni cha kujikimu na siyo Biashara. Mfano Tanzani tungekua tuna ongeza thamani mazao yetu tungeuza ulaya na wenzetu wangekula tu. Ulaya utumbo hakuna na ndizi hizi za kupiga kule hakuna wao wanajua ndizi mbivu tu, Mzungu alishangaa kuniona namenya ndizi nakuzipika akauliza kumbe ndizi zinapikwa wao wamezoa ndizi mbivu ndizo zinaliwa, na kingine kila nchi inatamaduni wa vyakula vyake, Mfano Waitaliano wao wanapenda Tambi na makolonya ndiyo chakula chao kikuu na Samaki laki sijui uwapikie Wali, Nyama, Pilau. maini hawapendi.
 
Wewe unaweza kula chakula Cha mbwa?

Unataka wadumae akil na miili kama sisi?
Kwenye miili, Afrika ndio inaongoza kua na watu wenye stature kubwa kuliko mabara mengine Duniani.

Udumavu za akili kwa afrika sio wa chakula kwa sababu chamula tunachokula ndio kinacholiwa Duniani, tofauti ni namna ya kuandaliwa. Udumavu wa kiakili unatokana na mchanganyiko wa mambo mbalimbali bila kusahau madhara ya ukoloni na vitu kama hivyo. Mathalani, ugali ni wanga sawa sawa na wanga nyingine za wali, mikate, tambi, viazi, ndizi, mihogo nk. Wanga haijawahi kua sababu ya udumavu wa akili.

Kwa mfano, 90% ama zaidi ya waafrika hujifunza ama huenda shule kujifunza kwa kutumia lugha za watu wengine wakati Dunia nyingine watu wote husoma na kujifunza kwa lugha zao wenyewe.
 
Kwenye miili, Afrika ndio inaongoza kua na watu wenye stature kubwa kuliko mabara mengine Duniani.

Udumavu za akili kwa afrika sio wa chakula, ni mchanganyiko wa mambo mbalimbali bila kusahau madhara ya ukoloni na vitu kama hivyo.

Kwa mfano, 90% ama zaidi ya waafrika hujifunza ama huenda shule kujifunza kwa kutumia lugha za watu wengine wakati Dunia nyingine watu wote husoma na kujifunza kwa lugha zao wenyewe.
Afu nyie hamjui TU....ivi unajua Elimu yetu ngumu kuliko ya ulaya
Kuna dogo wa darasa la 5 juzi alienda Germany akashangaa wenzake bado wanafundishwa kuganwanya double digits wakati huku yeye alisoma ayo darasa la 3
 
Mkuu umeuliza swali unalolijua,
Africa ni Dunia ya tatu

Hakuna bidhaa yoyote itakuwa international, zaidi bidhaa zetu zitawekwa
Kwenye Museums siyo kwenye masoko
 
Mahindi ndio yalikuja Africa kutoka America ila ugali ni chakula cha Waafrika tena kusini mwa jangwa la Sahara, sijataka kujikita kuangalia maeneo ya asili ya mazao bali bidhaa za vyakula zinazotengenezwa na hayo mazao popote yanapizalishwa duniani leo hii.
Mahindi yaliletwa africa na wafanya biashara wa kireno na wamisionari
 
Waafrika wametawaliwa, hawajatawala, ndiyo maana si vyakula tu, hata lugha zao hazijasambaa.

Kuna watu huko nje ndiyo kwanza wanaanza kugundua vyakula na mapishi ya Kiafrika.

Ukikaa majiji kama New York City kuna restaurants nzuri sana za Waafrika zinapendwa sana. Nishaenda restaurants za wa Senegal, Wa Ethiopia mpaka wa Kenya wanapika vyakula vyao vizuri sana vinapendwa ila kupata viungo kirahisi na kujua kupika kwa watu wa nje si rahisi. Pia kuna watu wengi hawana interest sana kujaribu vyakula tofauti.

Pia chakula kama ugali ni tasteless na nutritionless mimi huwa nakula ugali nikiwa na Watanzania kama wamepika wao ila kwangu sili ugali.

Sijawahi kupika ugali kwangu Marekani miaka yote niliyokaa.

Ushanielewa? Nimekaa Marekani tangu 1990s, sijawahi kupika ugali hata siku moja. Huwa nakula ugali nikitembelea Watanzania tu.

Hususan ugali mweupe ni chakula cha kijinga sana kwa sababu ni mahindi yaliyokobolewa na kuondolewa nutrients kama zote ukabakishiwa wanga tu.

Hivi ni vyakula vya watu wanaoangalia zaidi kushiba kuliko kupata virutubisho. Huko nje watu wanaangalia zaidi kupata virutubisho kuliko kushiba wanga tu.
Sidhani kama ugali (especially Dona) ni nutritionless kama ulivyosema hapo juu.

Pia katika paragraph yako ya Mwisho umesema huko nje watu wanaangalia zaidi virutubisho kuliko kushiba lakini hao hao ndo wanaongoza kwa kula vyakula vya hovyo (junk foods) kama vile pizza, burger, broiler na vinginevyo vingi.
Pia hao hao ndo wanaongoza kwa magonjwa yanayotokana na ulaji mbaya kama vile kisukari, magonjwa ya mfumo wa moyo na mishipa pamoja na miili ya kizembe (overweight).
 
Kwanza kabisa nimeeleza kwa kirefu sana kwamba ugali usio na nutrition ni uliokobolewa (Sembe) si usiokobolewa (Dona). Nimeeleza kirefu mpaka kwamba kukoboa mahindi kunaondoa protein nyingi zilizo katika pumba.

Pia nimeeleza ugali ni tasteless. Ni vigumu watu kupenda chakula cha kigeni kama chakula ni tasteless ambacho kinaliwa kushibisha tu. Suala si kukosa nutrition tu, kuna vyakula vingi vinakosa nutrition lakini vinapendwa kama ulivyosema, suala ni kwamba ugali hauna nutrition wala taste. It's a double whammy.
 
Kwanza kabisa nimeeleza kwa kirefu sana kwamba ugali usio na nutrition ni uliokobolewa (Sembe) si usiokobolewa (Dona). Nimeeleza kiregu mpaka kwamba kukoboa mahindi kunaondoa protein nyingi zilizo katika pumba.

Pia nimeeleza ugali ni tasteless. Ni vigumu watu kupenda chakula cha kigeni kama chakula ni tasteless ambacho kinaliwa kushibisha tu. Suala si kukosa nutrition tu, kuna vyakula vingi vinakosa nutrition lakini vinapendwa kama ulivyosema, suala ni kwamba ugali hauna nutrition wala taste. It's a double whammy.
Nimekuelewa mkuu, mazoea tu yanatuponza pia.
Siku VISA ya states ikitiki lazima nitue Tacoma hapo Washington state nikapige ugali na wajaluo wa Kenya.
 
[quote[Ukikaa majiji kama New York City kuna restaurants nzuri sana za Waafrika zinapendwa sana. Nishaenda restaurants za wa Senegal, Wa Ethiopia mpaka wa Kenya wanapika vyakula vyao vizuri sana vinapendwa ila kupata viungo kirahisi na kujua kupika kwa watu wa nje si rahisi. Pia kuna watu wengi hawana interest sana kujaribu vyakula tofauti.

Mimi hizo jollof rice na injera zilinishinda aisee. Huwa nawacheki washikaji wakitambiana nani anapika jollof kali kumzidi mwenzie kati ya Wanaija, Waghana, na Wasenegali.

Jollof mbele ya pilau hamna kitu kabisa. Pilau inalika hata yenyewe tu kavukavu bila mboga.

Kwa Wahabeshi napenda zaidi sambusa zao tu!
Pia chakula kama ugali ni tasteless na nutritionless mimi huwa nakula ugali nikiwa na Watanzania kama wamepika wao ila kwangu sili ugali.

Sijawahi kupika ugali kwangu Marekani miaka yote niliyokaa.

Ushanielewa? Nimekaa Marekani tangu 1990s, sijawahi kupika ugali hata siku moja. Huwa nakula ugali nikitembelea Watanzania tu.

Hususan ugali mweupe ni chakula cha kijinga sana kwa sababu ni mahindi yaliyokobolewa na kuondolewa nutrients kama zote ukabakishiwa wanga tu.

.
Dah! Kumbe siyo mimi tu ambaye huwa naona ugali ni bland sana.

Sijawahi kuelewa kwa nini watu wanaupenda ugali.

Ladha hauna! Virutubisho vyake ni hafifu.

Lakini kibongobongo ukiwaambia watu kuwa wewe hupendi ugali, hususan ukiwa ni Msukuma, watakushangaa sana.

Kuna wengine ukiwaambia wewe hupendi ugali, wanachukulia kama vile unajidai 😀.

Kama najinunulia chakula changu kwa hela zangu, ubaya uko wapi nikinunua vile ambavyo ninavipenda mimi?

Akili za baadhi ya Watanzania zimedumaa sana aisee.
 
Back
Top Bottom