Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Nimeangalia conventions mbili za vyama vya siasa Marekani na pia huwa naangalia mara kadhaa mikutano yao ya kisiasa, kinachonishangaza ni kama huwa hakuna kauli za hamasa za ki-vyama kwenye mikutano ya chama au kampeni. Amsha amsha za vyama vyote huwa wanaimba tu USA USA USA.
Hakuna mambo ya protocol imezingatiwa, mtu akipanda jukwaani anaenda moja kwa moja kwenye mada.
Hawasali, hawafungui mkutano kwa maombi au kuombewa. Wanaimba wimbo wa taifa tu.
Hakuna nyimbo za kuwasfia wagombea na vyama.
Hawajali sana rangi za vyama na hakuna mavazi ya chama. Kwenye mkutano wa Democrats rangi nyekundu ipo ya kutosha, kwenye mkutano wa Republicans blue ipo ya kutosha.
Muda mwingi wanautumia zaidi kwa watu kuzungumza speech badala ya burudani na kuhamasisha.
Tumechelewa sana.