Kwa nini wanawake wa kiafrika hawapendi nywele zao?

Kwa nini wanawake wa kiafrika hawapendi nywele zao?

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2016
Posts
2,536
Reaction score
4,621
Hapo vip!

Nimejiuliza sana hili swali muda mrefu, miaka na miaka ila nimekosa jibu sahihi.

Wanawake wengi wa kiafrika wameamua kukana na kukataa asili yao na kuidharau kabisa tofauti na wanaume..nikimaanisha wapo tayari kununua nywele za bandia hata za marehemu wa kizungu wavae kichwani...Inaamaana hii asili yetu kuanzia rangi mpaka nywele haina uzuri yeyeyote.......?

Siku hizi unaweza ukamaliza mji mzima ukamkosa mwanamke mwenye nywele zake za asili... Nina imani kungekuwa na dawa ambayo haina madhara kama hizi zilizopo, wanawake wote wangebadilisha rangi zao kuwa nyeupe... Inamaana Mungu alikosea kutuumba hivi ama vipi?

Lingine kama kufanya tendo hili ni dhambi..sasa wanawake wengi wakiafrika si wataaishia motoni....


Embu dada zetu tuambie shida nini?
 
Labda Kipilipili Pro Max. Zikijisokotoka Zinakuwa Kama Spring.

NB: Kutothamini Vya Kwao Kila Kitu Ni Bora Kulingana Na Taifa/Asili Husika.
 
Binafsi mimi ni low cut , tena naona low cut napendeza sana kuzidi nikisuka au kuvaa ka wigi.

Ila ndio vile siku moja moja kubadili muonekano kwa kuzitreat na karikiti au kuzitia kawigi.

Umesema kwamba siku hizi unaweza kuzunguka mjini ukakosa watu walio na nywele zao?

Acha uongo braza maana mimi tu hapa ofisini kwetu ndio sometimes natupia kawigi ila wengine wote wako na nywele zao natural
 
Binafsi mimi ni low cut , tena naona low cut napendeza sana kuzidi nikisuka au kuvaa ka wigi.
Ila ndio vile siku moja moja kubadili muonekano kwa kuzitreat na karikiti au kuzitia kawigi.

Umesema kwamba siku hizi unaweza kuzunguka mjini ukakosa watu walio na nywele zao? Acha uongo braza maana mimi tu hapa ofisini kwetu ndio sometimes natupia kawigi ila wengine wote wako na nywele zao natural
Jamaa muongo sana. Siku hizi wanawake wengi tu hawaweki dawa kwenye nywele zao
 
Nenda kwenye makambi ya wasabato..hizo wigi na nywele feki..utazitafuta kwa tochi.

Kimsingi wanawake wengi wa kiafrika ni brainwashed na hawajitambua ujinga umetawala hadi kwa wasomi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwahio anaevaa soksi au viatu hapendi nyayo zake ?

Au mvaa Kofia ?

Sio kwamba natetea mtu but I understand (to each his / her own) na anayekula nyama leo sio kwamba hapendi samaki na kesho atakula samaki (ni katika kubadilisha badilisha)

To each his/her own...., Kuna vitu kama uniqueness, fashion, convenience n.k.
 
Back
Top Bottom