Kwa nini wanawake wengi wanapenda kusema, "NILIKUWA NA...", hata kama kitu wanachokisema kiko kwenye wakati uliopo?

secretarybird

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2024
Posts
23,984
Reaction score
51,055
Kwa mfano, ukiwa unaongea na mwanamke utasikia akisema, 'nilikuwa naomba' unisaidi buku tano.

'Nilikuwa nauliza' kwamba mandazi shilingi ngapi.

'Nilikuwa naomba' uniruhusu kwenda nyumbani.

Je, huu ndio mtinfo mpya wa wanawake mjini ama vipi?

Baadhi ya vijana wa kiume nao wameshaanza kutumia mtindo huu.
 
Wakitaka kukuchezesha kizinga lazima wazunguke.

Lugha nyingi zinatumika...
 
Wakitaka kukuchezesha kizinga lazima wazunguke.

Lugha nyingi zinatumika...
Basi jana nimemkosa mtoto mkali kisa lugha gongana, nilikuwa tayari kupigwa kizinga tatizo sikuelewa alichokuwa anamaanisha 🥲
 
Mbona iko sawa tu kwenye Lugha
Inaonesha unyenyekevu kwenye ombi lako badala ya kusema kitu directly

I was wondering ..... if I could have permission to go home.
Nilikuwa

Ngoja niwaachie wenye weledi na umahiri wa lugha, yamkini uelewa unaweza kuwa umekengeuka
 
Sidhani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…