Kwa nini Watanzania wengi wapo upande wa Lissu?

Kwa nini Watanzania wengi wapo upande wa Lissu?

Najiuliza sana hili swali. Wengi wanasema Lissu anaonewa na kuteswa bure. wamama, wazee na vijana mitaani wapo upande wa Lissu.

Why?
Tundu Antiphas Mughwai Lissu is a prominent Tanzanian lawyer, human rights activist, and the current National Chairman of CHADEMA, the country's leading opposition party. He is widely recognized for his fierce criticism of government corruption and human rights abuses. 📌🔨✌🏿
 
Kiasili mwanadamu aliumbwa kuipenda haki, (japo kuna watu wanaharibu asili yao, kwa sababu shetani huwa amefanikiwa kuwaweka upande wake). Kutokana na ukweli huo, watu wakiona mtu anaonewa, husimama na anayeonewa. Na kwa upande wa Lisu, yeye ndiye anaonekana ni mtetezi mkuu wa wanaodhulumiwa. Kwa upande wa wadhulumu haki, inakuwa kinyume chake. Ndiyo maana unashuhudia, kwa kadiri Lisu anavyozidi kupendwa zaidi na wananchi, ndivyo hivo hivo watawala wadhulumu haki wanavyozidi kuchukiwa na umma mkubwa wa Taifa.
 
Mbona unauliza swali ambalo jibu lake lipo wazi; nia yako ni nini hasa?
 
"Toa neno wengi" comments 2000 zisikutishe ukadhani ndio wengi 😄😄 kumbuka tz ina population zaidi ya m60
Najuwa utasema katika hao milioni 60, asili mia 98 yao wanamkubali Samia; ndiyo maana walimpa ushindi mkubwa kuliko kiongozi mwingine yeyote aliyewahi kuongoza nchi hii!
Akili zenu zinafanya kazi kipekee sana.

Ni hivi, mkuu 'Palestine will be free'; nenda kamuulize Samia jibu la swali linaloulizwa kwenye mada hii, atakueleza kila kitu.

Unajuwa kwa nini hata Luhaga Mpina alionekana kuwa tishio kubwa kwa Samia aliyepata kura milioni 31 za misukule aliowatengeneza mwenyewe?

Sasa fikiria ingekuwaje kama lissu angekuwepo kwenye zoezi hilo!

Usisahau kwenda kumuuliza Samia sababu za kumweka ndani Tundu Lissu ili asishiriki uchafuzi uliompa Samia ushindi feki.
 
Back
Top Bottom