Kwa nini watu maarufu upendelea Range Rover na G-Wagon?

G wagon kimbaumbau sana, inaonekana wametumia utaaamu wa hali ya juu ili capability iendane na hizi zingine ambazo zimejaa kama range etc.
 
Mkuu samahani hivi kati ya G Wagon na Range Rover SVA ipi Ina stability nzuri?!
Ukiangalia reviews nyingi za magari mwaka huu... G-wagon imescore marks ndogo sana.

Wakati huo huo Range Rover imechukua marks nyingi kiasi cha kupewa "Editors Choice" kuanzia Top Gear,Car Connection na Car and the Driver.

Hii ni kwa kuwa Range Rover imekua stable On and Off-road... Na lile tatizo la kuwa eti Range Rover haidumu bila kwenda Garage limeshachimbiwa kaburi.

Tatizo pekee sasa la Range Rover ni sky high price... Bei yake kweli ni nondo.

G-wagon imekuwa stable off-road but sio stable on-road pia imekuwa na fuel economy mbaya zaidi yani inakula mafuta sio mchezo.

Pia comfort na handling ya gari ni nzuri sana kwenye Range Rover kuliko G-wagon.

So Range Rover ndio mshindi hapo.
 
G wagon kimbaumbau sana, inaonekana wametumia utaaamu wa hali ya juu ili capability iendane na hizi zingine ambazo zimejaa kama range etc.
Yeah Mkuu...

G-wagon ni Military Grade Vehicle yenye S-Class interior... Hutajuta Kuwa nayo.

Na imekaa kiume kwelikweli.
 
Upo sahihi mkuu...nikiangalia trend ni SUV tu...natamani kuiona hiyo BMW x7....
Then discovery waki pimp no.6 nitauza roho yangu
 
samahani mkuu siyo kwamba uwezo wako umefika hapo ?..... jirani yangu kanilazimisha kuandika
Liko wazi kua uwezo wangu upo hapo na hicho ndo nachokikubali ndo mana nkasema hunitoi hapo kwenye rav4
 
Liko wazi kua uwezo wangu upo hapo na hicho ndo nachokikubali ndo mana nkasema hunitoi hapo kwenye rav4
asante mkuu nilidhani unauwezo wa range nijisogeze uje uninunulie zawadi ya birthday li range natamani kulisukuma hili zigo
 

Hivi ni Sport utility vehicles au ni Suburban vehicles? Au mimi ndio nachanganya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…