GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Kwa wengine inawezekana ni mazoea tu. Lakini kwa upande wangu mimi, ni kwa sababu za kiusafi.
Leo, nikiwa mji fulani, niliingia kwenye mghahawa mmoja ambao kwa mji huo, ni miongoni mwa mighahawa ya hadhi, kwa ajili ya mlo wa Mchana. Mwonekano wake, huduma, bei na wateja wake inaakisi nilichosema. Ni mghahawa wa hadhi kubwa.
Nikiwa mghahawani hapo, aliingia dada mmoja kupata huduma. Aliagiza ugali na samaki, nafikiri, samaki choma.
Nilijikuta namfuatilia tokea aliponawa mpaka alipoanza kula.
Kilichonifanya nimfuatilie ni baada ya kumwona, alipomaliza kunawa mikono, aliendelea kushika vitu vingine visivyohusiana na chakula kwa kutumia mkono wake wa kulia.
Kwanza, alishika kiti chake na kukiweka vizuri kwa kutumia mikono yote miwili.
Pili, alichukua mkoba wake kwa kutumia mkono wa kulia na kufanya alichokusudia.
Tatu, aliendelea kutumia simu yake ya mkononi, nafikiri kwa kuchati, kwa kutumia mkono wa kulia.
Na ugali "wake" ulipowasili, aliendelea kula bila kunawa kwa mara nyingine.
Labda wajuvi wa masuala ya afya wanikosoe! Ni sahihi alivyofanya?
Mimi, kwa mtazamo wangu, alipaswa kutokushika tena simu, mkoba, viti, n.k. kwa kutumia mkono wa kulia kabla ya kumaliza kula kwa sababu huenda vitu hivyo vikawa na "vibakteria" hivyo kuwa hatarini kuambukizwa.
Nipo sahihi?
Nini lengo la watu kunawa kabla ya kula? Ni mazoea tu au sababu za kiafya?