GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
- Thread starter
- #21
Nashukuru kwa jibu lako mkuu🙏Kwanza umeuliza kwanini watu wananawa kabla ya kula. Kwa Waislam ni mafundisho ya mtume wao kuwa wanawe kabla ya kula, japo unawaji wao hasa ule wa watu wote kunawa kwenye chombo kimoja chenye maji yasiyotiririka sivyo inavyopaswa kuwa. Kiujumla ni jambo la usafi kwa watu wa dini zote na wasio na dini.
Pili umeuliza je, alichofanya bidada ni sahihi? Jibu si sahihi.
Siku nyingine mind your business unless wewe ni detective au undercover.
Lakini kuhusu kumind my own business, sidhani kama hilo ni sahihi. Naona kama huo mtazamo una kasumba ya ubinafsi. Wanaojua wasipowafahamisha wasiofahamu, ujinga utaendelea kutamalaki.
Mimi nafikiri ungekuwa umefanya vizuri zaidi kama ungenikosoa kwa kutokumshauri huyo dada ili pengine asirudie siku nyingine kufanya kosa kama hilo.