Kwa njia za kawaida, uwezo huo hauna. Ila kiheshima, eti unao….

Mkuu kwanza tukubaliane kuwa Rais Samia ametunukiwa PhD ya udaktari wa heshima sio wa kusomea.

Walio mtunuku waliamua wenyewe, kwa hiyari yao na kwa vigezo vyao kumpa kwa sababu ya heshima yao kwake, sio kwa sababu ya uwezo wake wa kusoma, hapana.

Pili, nilitaka kuweka kumbukumbu sawa kwa sababu ndugu Goodluck5 alipotosha kuwa ile PhD aliyopewa Rais Samia ni feki/mchongo.

Tatu, Rais Samia ametunukiwa heshima hiyo na watalaamu wa nchi ya nje bila Rais Samia kuwalazimisha.

Ninaami wao kwa utalaamu wao wameona jambo adhimu kwa Rais Samia kiasi cha kustahili hiyo heshima!

Kama mashaka ni uwezo basi wakutiliwa mashaka kuhusu uwezo ni hao maprofesa kwa kumpa heshima ambayo wengi wetu tu naona hakustahili.

Kimsingi kama tunafikira hasi namna hii juu uwezo Rais na kiongozi wetu, basi tujue yeye ni true reflection ya jinsi tulivyo! Maana hajashuka kutoka mbinguni!

Nne, kuhusu kuandika Makala au kitabu, ni mapema mno kusema hata weza kuandika. Kwa maoni yangu, jinsi ambavyo ameweza kuongoza nchi kwa utulivu akiwa mwanamke amedhihirisha uwezo wake kiasi cha a
Kustahili heshima hiyo!

Ukweli usio na shaka ni kuwa ameingia madarakani katika mazingira magumu, hatari na ya pekee. Kaingia baada ya Rais kufa akiwa madarakani, umbi la uchaguzi mkuu halijatulia na bado korona ikiwepo.

Pamoja na hayo amepambana mno hadi nchi sasa ni tulivu, uchumi unatengamaa na kuinukia vizuri, uhuru na demokrasia ya wananchi imetamalaki ilihali uwekezaji umeongezeka miongoni mwa machache

Mkuu waswahili husema, mnyonge, mnyonge ila haki yake mpenzi.
 
You nailed it
 
Nyerere aliwahi kuwa na PhD ya darasani?

Ilimchukuwa Nyerere miaka mingapi ya Urais kabla ya chuo kikuu chochote duniani kumpa "Honoris causa"?

Imemchukuwa mama Samia Suluhu Hassan chini ya miaka mitatu ya Urais kupata "honoris causa" ya Kimataifa.

"naona donge mie".
 
Ukiifatilia historia ya PhD, ilianzia kwenye zote kuwa ni za heshima, PhD baadae sana ndiyo zikaja kutolewa kwa "kusoma".

Zote msingi wake ni heshima, hakuna zaidi.

Nafahamu huu uzi lengo lake ni jaribio la "character assassination" lakini mleta mada anasahau kuwa kuna hata academically failures" wametunukiwa Honoris Causa.

Ma shaa Allah Mama Samia hana historia ya kufeli. Nanihii je?
 
JK alipewa Uprofesa wa heshimu Kule China

Napendekeza Hamas waliopenya Ndani ya Israel na kumfanya Biden atokwe machozi Wapewe PhD ya Ubunifu Mpya kabisa Duniani 😂😂

Hamas Ndio wamefanya maajabu
Maajabu yasiyotarajiwa
 
Ulinganifu babaifu.
 
Wahindi,waarabu na wachina... na hata wazungu ni wajanja sana. Wakisikia raia wa kiafrika anafanya ziara kwenye nchi zao huwa wanapelelezi weakness zake na kuzitumia kumfurahisha. Bila shaka wahindi wameshajua viongozi wa Tanzania wanapenda kusifiwa na kupewa degree za heshima hivyo wamaamua kutumia nafasi...
 
Huo siyo "ulinganifu" huo ni ukweli.

Ukweli unasumbuwa akili yako?
Mazingira ya wakati, historia binafsi, changamoto za kidunia kwa kipindi Cha kila mmoja ni tofauti...hivyo hata ulinganifu kati yao hauwezi kuwa sawa
 
Swadakta!
 
Form tu alishindwa kupata D 3 huko pHd si atapauona kama jahanam sasa
 
Kabisa! Viongozi wanafuja mambo sana mfano Magufuli akiwa waziri alifanyiwa PhD na mhadhiri mmoja (jina nalihifadhi) pale chemistry department UDSM. Tulimwona Magufuli akija mara moja moja na kuonana na Dr huyo na kuondoka mda mfupi baadaye. Lab technicians walichakarika na baadaye kidogo tulisikia Magufuli ametunukiwa PhD ya chemistry!

Ben Saanane alipotezwa hadi leo hii kwa kuhoji uhalali wa hiyo PhD feki niliyoshuhudia mwenyewe! Okay

Magufuli alipokuwa rais yule mhadhiri alipewa cheo kuwa Katibu Mkuu wizara flani hadi leo!

Ukiwa kiongozi nchi hii utakuwa multibilionare, professor, generali, chifu na budget ya nchi nzima watasema umetoa wewe na utashukuriwa sana kwa miradi mbali mbali ya kitaifa kwa nyimbo na picha yako itabandikwa kwa lazima kila ofisi na katika mabango barabarani!
 
sasa ukishakuwa CCM lini unaruhusiwa kutumia akili? unatakiwa kutumia tu tumbo kufikiria. hayo mengine ya vyeti ukishakuwa CCM damu si jambo linalohitajika. hutakiwi kutumia akili kuwa ccm damu ama sivyo hautakuwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…