Kwa njia za kawaida, uwezo huo hauna. Ila kiheshima, eti unao….

Kwa njia za kawaida, uwezo huo hauna. Ila kiheshima, eti unao….

Samia kafanya nini kwenye uchumi?

GDP yetu kaikuza kwa kiasi gani?

Kipato cha mwananchi kimeongezeka kwa kiasi gani?

Kaiondoa nchi kwenye utegemezi wa wafadhili?
Hutendi haki mkuu tusubiri angalau amalize miaka 5 ili tuweze kumlinganisha na Magufuli au amalize miaka 10 ili tuweze kumlinganisha na Mwinyi, Mkapa na Kikwete. Ni mapema mno.
 
Ni watu ambao wamewahi kuandika makala zilizochapishwa na magazeti na majarida mbali mbali duniani. Ni watu ambao wameshaahiriki kwenye mijadala mikubwa ya kimataifa na kutoa, kujenga, na kutetea hoja zao kwa umahiri mkubwa sana huku wakiwa na ‘command ya facts’ isiyo na mashaka.
Nyerere alijua kujenga hoja,lakini pia kubomoa. Hoja aliyoijenga kuibomoa ilikuwa shughuli
Mfano, alikuwa mmoja wa viongozi 6 Duniani walioaminiwa kushughulikia suala la ''Disarmament' wakati wa cold war
Nyerere akachaguliwa kuwa mwenyekiti wa south south commission
Vitu hivi tu viwili vinaonyesha Dunia ilijua kuna mtu inayoweza kumtumia, Udaktari wala haukuhitaji kusoma tena

Mkapa: Alijenga hoja kuhusu Wakimbizi wa Rwanda na Burundi na namna ya kutatua tatizo, Dunia ikamsikiliza
Mkapa alisimama peke yake katika common wealth na kuitetea Zimbabwe kama msemaji wa Afrika. Peke yake

Niishie hapo tu
 
Sasa mtu form tu hapo alifaulu kibahati huko mbeleni PhD ya class angemudu kweli, muache bhn apewe hiyohiyo ya mchongo/fake ndio size yake!.
Ukweli ni kwamba PhD aliyopewa Rais Samia sio feki na wala sio ya mchongo, kapewa na maprofesa kutoka chuo kinacho tambulika, hadharani na mchana kweupee!
 
Ukweli ni kwamba PhD aliyopewa Rais Samia sio feki wala ya mchongo, kapewa na maprofesa kutoka chuo kinacho tambua, hadharani na mchana kweupee!

..mtoa mada anadai aliyepewa ndio feki, hana uwezo wa kupata PhD kwa kuisomea.

..je, wewe unaamini Maza ana uwezo wa kielimu na kitaalum kupata PhD?

..Maza amewahi kuandika makala yoyote ktk maarifa ya kitaalam?

..Maza amewahi kuandika kitabu chochote kudhihirisha usomi wake?

..Maza amewahi kualikwa popote na wasomi kutoa mhadhara na kuulizwa maswali kutokana na mada aliyowasilisha?
 
Naona kama vile kuna watu hapa nchini waonao mtu kupewa ule udaktari wa heshima ni sawa na ule wa kuusomea.

Ukweli ni kwamba, si sawa hata kidogo.

Juzi hapa Rais wenu kapewa tena udaktari wa heshima huko India.

Tayari sasa katika utambulisho wake, watu wameshaanza kumwita eti Dr. Samia Suluhu Hassan.

Naye kwa kupenda ujiko, hata hagomi kuitwa hivyo.

Yupo tu anachekelea na kufurahia.

Now let’s face it. Katika hali ya kawaida, Samia hana uwezo wa kusoma na kufaulu mpaka kiwango cha PhD.

Kuna watu unaona kabisa huyu ana uwezo huo. Mfano Julius Nyerere au Benjamin Mkapa.

Hao ukiwasikiliza tu hata vile waongeavyo kuhusu mada mbali mbali, unauona kabisa uwezo wao.

Ni watu ambao wamewahi kuandika makala zilizochapishwa na magazeti na majarida mbali mbali duniani. Ni watu ambao wameshaahiriki kwenye mijadala mikubwa ya kimataifa na kutoa, kujenga, na kutetea hoja zao kwa umahiri mkubwa sana huku wakiwa na ‘command ya facts’ isiyo na mashaka.

Hao hata wakipewa udaktari wa heshima, mtu unaona kweli wanastahili maana hata wangeamua kupitia mkondo wa elimu, huo udaktari wangeupata tu.

Ila huyu tuliyenaye sasa, hana uwezo wa kupitia mkondo wa elimu na kuipata Phd.

Huo udaktari wake wa kupewa, unatokana na yeye kubahatika tu kuwa Rais.

Hana uwezo wa kuwa PhD wa ukweli…..
Anahongwa ili atoe raslimali bure. Kilaza wahead tarishi aliyefeli form iv. Aliyebahatika kuwa rais WA nchi
 
Ila huyu tuliyenaye sasa, hana uwezo wa kupitia mkondo wa elimu na kuipata Phd.
Na yule wa awamu ya 4 pia hana huo uwezo. Labda akiamua kupata hizi za mtaani za kughushi kwa kununua.
Ila yule mtaalamu wa kemia yeye uwezo alikuwa nao 100%. Anaungana na akina Nyerere na Che-Nkapa.
 
..Maza alitakiwa awe muungwana kwa kukataa kuitwa Dr.

..Wanaoitwa Dr ktk mazingira ya kawaida ni Madaktari wanaouguza hospitalini.

..Wenye shahada za Uzamifu / PhD huitwa Dr wakiwa miongoni mwa wanataaluma wenzao ktk shughuli zao za kitaalamu. Wakiwa ktk shughuli nyingine yoyote ile hawatumii utambulisho huo.
Lakini ni watu wenyewe wanamuita
Hajiiti yeye mwenyewe.

Anyway,hongera kwake.
 
Lakini ni watu wenyewe wanamuita
Hajiiti yeye mwenyewe.

Anyway,hongera kwake.
Anna, yeye mwenyewe akiwa discourage watu kumwita hivyo, na wao wataacha.

Nadhani Nyerere na Mkapa walikataa kuitwa watukufu na tokea hapo sikusikia tena wakiitwa watukufu!

Anna, yeye mwenyewe akiwa discourage watu kumwita hivyo, na wao wataacha.

Nadhani Nyerere na Mkapa walikataa kuitwa watukufu na tokea hapo sikusikia tena wakiitwa watukufu!

Anapenda kuitwa ndio maana anakaa kimya.

Toka wampe ile UD,ghafla wakaanza kumuita Dr...
Naye hata hashtuki😆
 
"PhD ya heshima ni bora kuliko PhD ya darasani" Profesa Palamagamba John Kabudi
 
Naona kama vile kuna watu hapa nchini waonao mtu kupewa ule udaktari wa heshima ni sawa na ule wa kuusomea.

Ukweli ni kwamba, si sawa hata kidogo.

Juzi hapa Rais wenu kapewa tena udaktari wa heshima huko India.

Tayari sasa katika utambulisho wake, watu wameshaanza kumwita eti Dr. Samia Suluhu Hassan.

Naye kwa kupenda ujiko, hata hagomi kuitwa hivyo.

Yupo tu anachekelea na kufurahia.

Now let’s face it. Katika hali ya kawaida, Samia hana uwezo wa kusoma na kufaulu mpaka kiwango cha PhD.

Kuna watu unaona kabisa huyu ana uwezo huo. Mfano Julius Nyerere au Benjamin Mkapa.

Hao ukiwasikiliza tu hata vile waongeavyo kuhusu mada mbali mbali, unauona kabisa uwezo wao.

Ni watu ambao wamewahi kuandika makala zilizochapishwa na magazeti na majarida mbali mbali duniani. Ni watu ambao wameshaahiriki kwenye mijadala mikubwa ya kimataifa na kutoa, kujenga, na kutetea hoja zao kwa umahiri mkubwa sana huku wakiwa na ‘command ya facts’ isiyo na mashaka.

Hao hata wakipewa udaktari wa heshima, mtu unaona kweli wanastahili maana hata wangeamua kupitia mkondo wa elimu, huo udaktari wangeupata tu.

Ila huyu tuliyenaye sasa, hana uwezo wa kupitia mkondo wa elimu na kuipata Phd.

Huo udaktari wake wa kupewa, unatokana na yeye kubahatika tu kuwa Rais.

Hana uwezo wa kuwa PhD wa ukweli…..
Ila watu mna chuki..Sasa ndio nini hii umeandika..yeye ndiye rais wako..unafikiri hiyo nafasi ameipata kwa upendeleo...acha chuki..pambana na Hali yako..
 
Wewe mwaka huu utaugua kwa chuki zako kwa mh Rais. Najuwa kinachokutesa sana ni chuki zako binafsi kwa mh Rais,ukabila uliokujaa akilini mwako na ukipofu wako wa akili na mawazo ambao umekufanya ugote na kufika mwisho katika kufikiri.wewe ni wale mliokuwa hamtaki Rais wetu awe Rais.wewe ni wale mliooedelea kukesha usiku na mchana kutaka kuona Rais wetu anashindwa kuongoza Taifa letu.wewe ni wale mliokuwa mkiomba dua mbaya kwa Rais wetu ili asifanikiwe katika mpango wa aina yoyote ile wa kiuchumi na kimaendeleo kwa Taifa letu.

Sasa baada ya kuona mmeshindwa katika Dua zenu zote,baada ya kuona Rais samia anaendelea kukubalika na kupendwa na watanzania,kukubalika nje ya nchi,kutambulika mchango wake kimataifa katika ustawi wa Taifa letu na kuifanya Tanzania kuwa kimbilio la wengi,baada ya kueleweka na kupongezwa na jumuiya za kimataifa kutokana na utawala bora wenye kuheshimu haki za binadamu na kuzingatia haki na usawa katika kuendesha nchi yetu mmebakia mnaumia sana,mnateseka sana na hamuelewi mfanye nini ,maana mnaona Rais samia akiendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya watanzania na kuendelea kupata heshima na uungwaji mkono kutoka kila kona ya dunia.

Kaeni tu kwa kutulia maana Rais samia ni mpango wa Mungu na ameimulika na Mungu na siyo na mkono wa mwanadamu na hivyo hawezi kushushwa na mwanadamu aina yako mwemye chuki binafsi na ubaguzi wa kijinga.watanzania Tupo bega kwa bega na Rais wetu na tunaendelea kumuunga mkono usiku na mchana,maana kupitia yeye tumepata matumaini ya kila mtu kutimiza ndoto zake.

Watanzania tunajionea kwa macho yetu namna uchumi wetu unavyokua kwa kasi na namna kila mmoja wetu anavyoguswa na ukuaji huo wa uchumi, tunashuhudia namna huduma za kijamii zinavyoboreshwa na kusogezwa jirani ya watanzania.

Wenye akili wametambua uwezo wa Rais samia na mchango wake katika ustawi wa watu,sasa wewe na umbumbumbu wako ni nani ubishane na wenye akili? Una akili gani hapo ulipo? Kipi ulichokifanya kwa Taifa letu cha kumzidi Rais wetu? Zaidi ya kupiga soko lako la kibaguzi ni nini cha mafanikio chenye kugusa maisha ya watu ulichokifanya na unachoweza kukionyesha kwa watanzania?

Tuondolee mikosi na nuksi zako hapa.Tuachie Rais wetu na uwe na adabu kwa Rais wetu.wewe endelea kuhangaika huko huko nje ya nchi wakati sisi tunaendelea kulijenga Taifa letu kwa mikono yetu kwa kushirikiana na Rais wetu aliye mstari wa mbele katika kulitumikia Taifa letu kwa uzalendo uliotukuka.
Ahsante umempa vidonge vyake.. Watanzania tupendane na tumuunge mkono rais wetu...hakuna mwenye hati miliki ya nchi hii..nchi hii ni yetu sote na tuipende na kuilinda..tuwakatae kwa nguvu zetu zote watu wote wanaotaka kupanda mbegu za chuki za kikabila, kidini, kirangi,kikanda na hata kijinsia..Shime Watanzania tupendane na kuvumiliana kwa misingi ya tofauti zetu.
 
Back
Top Bottom