Kwa Pesa wanazoiba, inanivunja moyo kulipa kodi

Kwa Pesa wanazoiba, inanivunja moyo kulipa kodi

Nimeamua sasa rasmi.

Kunikamata hawatoweza milele na nasema wazi kuanzia sasa sitolipa tena kodi wala tra hawatoniona tena kwenye makadirio.

Kwa sisi mabingwa uhangaikie kodi ulipe halafu watu wamekaa ofisini wanajipigia wakati mvua na jua linatupata sisi mahustler hapana.

Nasema tena hapana, nilikua Raia mwema kwa sasa imetosha hapa nilipofika ndio mwisho na sirudi tena nyuma
Watu waibe mabilioni halafu bado wako kazini, niunguzwe na makemikali, niangukie na magogo ya timba, nilale kwenye turubai kesho nilipe kodi halafu kodi yenyewe inapigwa hivyo.

Uzalendo bora ufie hapa potelea pote, tujenge nchi kwa jasho wengine wajilie haiwezekani.

Nasema huo ndio msimamo wangu, hali labda ikibadilika mbeleni huko nitaanza kulipa tena lakini kwa sasa hapana hapana.
Usisahau kwenda kufunga biashara yako TRA,maana unaweza kwenda 2030 ukakuta deni ambalo utashangaa
 
Hii ni aibu sana kwa nchi, kiongozi analalamika badala ya kuchukua hatua kweli? Huku mikopo kila uchwao, halafu watu wanajichukulia fedha tu kama shamba la bibi na wahusika wapo? Mabenki yetu pia ndio kusema hayana mifumo ya kuangalia mkopaji kama anadaiwa kwingineko kweli? Hapo kuna watu wakubwa wanahusika katika hilo.
 
Una haki mkuu,kwa jinsia mambo yalivyo una haki.Samia kazi imemshinda aachie ngazi,hang'ati kabisa.Sijui nani kamng'o meno,waliomnanii Magufuli nini.Yetu macho.
Mama kaanza kutukana tena mwezi mtukufu,tunapoelekea atawaja tu.
 
Watanzania muelewe kinachoibwa ni mali ya umma, umma maana yake ni wewe mwananchi wa Tanzania, hata mtumishi wa serikali ambae anakatwa kodi na haongezwi mshahara nae ajue pesa na haki yake inapigwa na wahuni,
 
Anatembea na panic button yake ready.ready[emoji1787]
Mashirika yanajiendesha Kwa hasara miaka yote halafu anakuja mjuaji analazimisha kwamba yamejiendesha Kwa faida kipindi chake anapokea na gawio[emoji23][emoji23] nenda kwenye ripoti ya CAG sasa[emoji1787][emoji1787][emoji1787] halafu CAG akionyesha haya wanatokwa povu eti marehemu anaonewa Kwa kuwa Hana uwezo wa kujibu tena
 
Watanzania muelewe kinachoibwa ni mali ya umma, umma maana yake ni wewe mwananchi wa Tanzania, hata mtumishi wa serikali ambae anakatwa kodi na haongezwi mshahara nae ajue pesa na haki yake inapigwa na wahuni,
Wizi upo tu miaka yote jichunguze hata wewe kwenye mishe zako Kuna maeneo unapiga sema kinachokusumbua ni Kwa kuwa wenzio wanapiga ndefu kuliko wewe sasa Cha kufanya tafuta fursa ya kupiga kikubwa Ili upunguze wivu na makasiriko
 
Kwakweli wanazingua sana,hela zinaibiwa za kutosha tu alafu bado Raisi wetu yupo kimya na kesho yake utasikia tumepewa mkopo wenye mashart Nafuuu,hizo hela zinazoibiwa akiweza kuzisimamia vizuri si tutapunguza kiasi cha kukopa nje?.
Ila mama wacha jasho limtoke tulimwambia umeachana na Uliowakuta unaingiza waliotolewa watakutia aibu wale ni majambazi sio wezi tu,akashupaza shingo leo kaishia kusema tu Pumbavuuuu,stupid haisaidiii.
Naskia jamaa kaagiza mabasi 100 na basi moja mln 300.
Wapya wote alioingiza Samia ni wapigaji mkuu,sijui naye mpigaji.Maana ndege wanaoruka pamoja lazima wafanane.Tanzania tuna kazi na huyu mama.Yaani kuwa karibu na Marekani kiasi hiki ujue nchi imeuzwa.Yaani such an evil nation tunakuwa karibu nayo mpaka Makamu wao wa Rais anatutembelea!!!!! Tumekwisha,tumekwisha,tumekwisha.

Halafu kwa ujinga was Watanzania wengine eti wanakesha mpaka usiku wanamsubiri Kamala Harris,representative wa Lucifer.How can we be so close to such an evil nation.Very disgusting.
 
Na wasivo na aibu unaona mara OSHA, tbs, zimamoto, halmashauri, ulinzi shirikishi, TRA, watu wa mazingira, yaani unakiofisi chako wote hao wanataka pesa halafu maskini ya mungu pesa utoe na hazina usimamizi mzuri hapana hapana sio sawa
 
Back
Top Bottom