Kwa Rais Samia nchi inakwenda bila makelele

Kwa Rais Samia nchi inakwenda bila makelele

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Mtu anaejiamini anamfukuza mwizi kimyakimya bila kupiga kelele, hata wanyama wanaojiamini habweki sana wakiona adui yao.

Kuna wakati Watanzania walitaka kuaminishwa kuwa makelele mengi hadharani ni dalili njema za kujiamini na uongozi bora, lakini sasa imedhihilika kuwa sio kelele nyingi zinazoleta matokeo chanya kwenye kila jambo. Watu tumeanza kumuelewa mama Samia, Rais wa Jamhuri ya Tanzania na ametufundisha somo kuwa mbwembwe nyingi sio sehemu ya uongozi bora.

Viongozi wote hata wa kwenye ngazi ya familia tumepata kiigizo chema na somo kuhusu uongozi. Sisi tunahitaji kuona matokeo maji yakitiririka kwenye mabonda, umeme ukiwaka nchi nzima, barabara zikijengwa, watoto wanakwenda shule na majambazi wakinyang'anya silaha zao hukohuko vichakani walikojificha na sio makelele ya kuyataja majina yote ya Rais mara 100 kwenye kila mkutano wakati output hakuna.

Wanawake jamaniee hawana mambo mengi, wana aibu, hawahongi na wanapenda sifa, hivyo sio wezi kama mijianaumeeee.

Tumechelewa wapi sie kuchagua wapiga dili miaka yote hiyo?? Mungu atusamehe ssi kwa dhambi hiyo.

Mwaka 2025 sintapepesa macho.
 
Wala majigambo,vitisho,kutekana na uporaji yaani mambo ni ♨️♨️🔥🔥..

Hivi 2025 nani atagombea nae? Gaidi Mbowe, Gwajiboy au yule mke wa Amsterdam?

Si tutakuwa tunaharibu pesa za walipakodi wakati mshindi anajulikana?
Nchi inaenda kwa PGO tu.
 
Ukitaka kujua magenge ya wahuni wasaka vyeo no vi thread vya hovyo. Mpaka mmemchukua kijana wa hovyo jamhuri ya Twitter!
 
Uvccm lugha gongana. sijui mmedhulumiana huko.
Hakuna anaetamani kelele za kila kona tena, hata ukinunua kijiko cha kukorogea chai unataka lazima mama na watoto wote wakupigie makofi hadi mikono iote malengelenge wakati ni kazi yako.
 
Atupatie katiba mpya basi na tume huru ili tuone uzalendo wake
 
Hakuna anaetamani kelele za kila kona tena, hata ukinunua kijiko cha kukorogea chai unataka lazima mama na watoto wote wakupigie makofi hadi mikono iote malengelenge wakati ni kazi yako.
Kinachoshangaza ni kujaribu kumpaisha mama kwa kuwashusha wengine.

Nijuavyo, mama ana mazurii yake na aliyepita ana mazuri yake pia

Nakushauri kama lengo ni kumsifia mama, msifia bila kumlinganisha na watu wengine

usijeumbuka.
 
Tunataka Tume mpya ya Uchaguzi na Katiba mpya,muhimu ni Tume huru ya Uchaguzi kwanza.
Tume mpya haiji bila katiba mpya. Ukawa walikwamisha ujio wa tume mpya kwa kukwamisha mchakato wa katiba mpya kwa sababu za kipuuzi kabisa za kung'ang'ania Muungano wa Mkataba sijui wa serikali 3 sijui nini. Jamani Muungano huu ni kama jina lako, kama wazazi wako walikosea wakakuita Nyani basi walikosea kwa niaba yako.

Wazee wetu walikosea kwa niaba yetu kuweka muungano wa serikali mbili, wamarekani walikosea kuwa na muungano ule wa USA baadhi ya majimbo yanalalamika chinichini, waingereza walikosea muungano wao, wa Ireland wanalalamika chinichini bila mafanikio. Tukitaka tume huru ya uchaguzi tuachane na serikali 3 maana agenda haitafika mwisho.

Wahuni wa UKAWA walijiona wameupiga mwingi kumbe hamna kitu kabisa, ndio walikosea kila kitu. wao wangekubali serikali 2 kwanza wakiingia ikulu ndio walete muungano wa mkataba, yaani walijifungia nje wenyewe.
 
Naona Team Lumumba mnafanyia kazi vibahasha vya khaki!
Vibahasha gani mkuu,hata huko Lumumba sijawahi fika,mimi ni mzalendo tuu namkubali mama na Kwa hiyo Niko tayari kutangaza mafanikio yake.

Kwani wewe unapenda uongo na kuporwa pesa? Kwani hayo mafanikio huyaoni?

Au mkuu na wewe unateseka mama akisifiwa anapostahili?
 
Vibahasha gani mkuu,hata huko Lumumba sijawahi fika,mimi ni mzalendo tuu namkubali mama na Kwa hiyo Niko tayari kutangaza mafanikio yake.

Kwani wewe unapenda uongo na kuporwa pesa? Kwani hayo mafanikio huyaoni?

Au mkuu na wewe unateseka mama akisifiwa anapostahili?
Mie siteseki ila mwanaume lazma ujifunze kubalance shobo
 
Back
Top Bottom