Kwa sasa Geita inachangia pakubwa kwenye pato la Taifa, “inastahili" kama Kilimanjaro enzi za kahawa!

Kwa sasa Geita inachangia pakubwa kwenye pato la Taifa, “inastahili" kama Kilimanjaro enzi za kahawa!

Ajabu wilaya ya Geita yenye madini(mgodi mkubwa wa 2 barani Afrika) imeachwa/imesahaulika. Si umeme(REA), Wakati wilaya za Mbogwe, Bukombe, Nyang'wale, Chato vijiji vyake vikiwa na coverage ya 90%+ ya umeme, wilaya ya Geita hata 50% haijafikiwa. Sijui shida ni nini.
Nachojua mimi Geita ni mkoa una wilaya zake kama hizo chato,geita vijijini geita mji mbogwe nyangwale sasa hiyo wilaya ya geita ni ipi mkuu?
 
Geita haijaumbwa ili iwe mashimo baada ya kuchimba madini bali inastahili maendeleo kama mikoa mingine.

Nimeona niseme hili maana ujenzi wa kimaendeleo wa uwanja wa ndege na hospitali ya Rufaa unawanyima usingizi Chadema ambao wamewahi kuwa na wabunge makini kutoka kanda ya ziwa.

Geita na mikoa mingine iliyosahaulika ni lazima ikumbukwe sasa kama kahawa ilivyoinufaisha Kilimanjaro.

Kupanga ni kuchagua.

Maendeleo hayana vyama!
Wee mburula Unazungumzia Geita au Chato? Maana watu mnaificha Chato chini ya mwanvuli wa Geita mjini.
 
Ajabu wilaya ya Geita yenye madini(mgodi mkubwa wa 2 barani Afrika) imeachwa/imesahaulika. Si umeme(REA), Wakati wilaya za Mbogwe, Bukombe, Nyang'wale, Chato vijiji vyake vikiwa na coverage ya 90%+ ya umeme, wilaya ya Geita hata 50% haijafikiwa. Sijui shida ni nini.
Hiyo si ndio Geita mkuu?

Au wewe unataka kusema Geita ni ipi
 
Nachojua mimi Geita ni mkoa una wilaya zake kama hizo chato,geita vijijini geita mji mbogwe nyangwale sasa hiyo wilaya ya geita ni ipi mkuu?
Hakuna wilaya inayoitwa Geita vijijini, bali wilaya ya Geita.

Sema hivi, kuanzia mwaka 2015, Jimbo la uchaguzi lililokuwa likiitwa Geita liligawanywa na kuwa Jimbo la Geita mjini na Geita vijijini

Pia, baada ya mji wa Geita kupewa hadhi ya mji, kukawa na halmashauri mbili ndani ya wilaya moja ambazo Ni
1. Halmashauri ya wilaya ya Geita ambayo ndani yake Kuna majimbo ya uchaguzi ya Geita vijijini(kwa Msukuma) na Jimbo la Busanda.
2. Halmashauri ya mji wa Geita yenye Jimbo la uchaguzi la Geita mjini.

Hivyo, wilaya ya Geita Ina halmashauri mbili na majimbo matatu.
 
Kuna haja ya kujengwa ikulu ya milele kwenye eneo hilo ili kuwakata ngebe hao Chadema , halafu kufanya mambo katika nchi kwa kuangalia yanayosemwa na chadema badala ya kufuata katiba ya nchi ni jambo la Aibu ya kiwango cha kijinga sana .
Kuna kipengele kipi cha katiba kimekiukwa?
 
KILA mkoa ungebaki na mapato yake kujiendesha tuone hata vyoo kama mngeweza jenga.
Ni wizi mtupu kuiba Kodi za mikoa mingine na kwenda kufurahisha mikoa mingine isiyozalisha
 
Ona ulivyolipumbavu! Hospital ya rufaa na uwanja wa ndege vimejengwa Geita? Sema tu ukweli kwamba viko Chato na ni maandalizi ya mkoa mpya wa Rubondo ambao tunaenda kutangaza 2023/24. Utajumuisha wilaya za Chato, Biharamulo, Ngara na Kakonko.
 
Geita haijaumbwa ili iwe mashimo baada ya kuchimba madini bali inastahili maendeleo kama mikoa mingine.

Nimeona niseme hili maana ujenzi wa kimaendeleo wa uwanja wa ndege na hospitali ya Rufaa unawanyima usingizi Chadema ambao wamewahi kuwa na wabunge makini kutoka kanda ya ziwa.

Geita na mikoa mingine iliyosahaulika ni lazima ikumbukwe sasa kama kahawa ilivyoinufaisha Kilimanjaro.

Kupanga ni kuchagua.

Maendeleo hayana vyama!
Nakubaliana nawe kwa asilimia kubwa, lakini kujenga uwanja wa ndege wa international- mmmm sijui kama utawasaidia wana Geita.

Ningependa hata bandari kuu Tanzania ijengwe CHATO - lakini!!!!!!!!!! Tunaweza kuorodhesha vingi tu vya ufahari vinavyoweza jengwa huko lakini swali hivyo vitu vitamsaidiaje mwana- Geita na mtanzania kwa jumla.
 
Yaani mmeshindwa kutumia madini yaliyopo hapo kuwapekea hao wananchi maendeleo sasa mnataka kupeleka maendeleo kwa kuwajengea hospitali?!

CCM ni mzigo kwa hili taifa.
Mimi sikubaliani na yanayoendelea Geita lakini Hospital ni maendeleo! Sijui wewe unaangalia kwa jicho lipi?! Sio inachangia ajira tu bali pia inavutia uwezekaji!
 
Back
Top Bottom